Je, kanisa la mhubiri Christopher Mwakasege liko wapi?

huwa sio fan wa makanisa ya kiroho, but Mwakasege yuko level nyingine:

hata kama anahubiri kuhusu pesa; ila anakuwa na back up inayoeleweka, he talks sense mara nyingi.

Kitu nisichoelewa huwa ni kutoa mapepo.
Hapana ilikuwa kabla ya hilo ni wakati wa mahubiri ya jangwani. Mwakasege anaijua vizuri bible so anaona akichomekea maombi ya pesa kupitia hiyo atapata na kweli anapata. Atakapobadilika arudi kufundisha watu neno la Mungu ili waache mabaya ndipo nitamrejelea tena.
 
Kama u mfuasi wake nazidi kumchukia mwakasege pia.

Mmmmmh wajameni,chonde chonde chonde!!msiwachukie wala kuwasema.....kila mtu atasimama kizimbani kujibu kwa sehemu yake mbele za Muumba, kama alikua anahubiri vizuri na kwasasa anakosea anahubiri ela basi naye atajieleza kwa Mungu kwa nini ame deviate, we chukua zuri analokufundisha nenda nalo litakusaidia kushi huku ukingojea kujibu sehemu yako nawewe unayokosea kutokana na vile ulivyopaswa kuishi.

Plizzzzzzz,msinishambulie ni mtazamo wangu tu!
 
Mbinguni utaenda a jf?? Embu wahi haraka ukaponye roho yako ndugu
 
Kwa nini hizi movement za kiroho ziko mijini mijini tu? Ambako watu wanakuja na magari, watumish na wafanyabiashara? Nina sababu ya kuhoji, mbona Yesu alikuwa anatembea kwa wavuvi na watu wasio na hata mia, lkn hawa watumishi wanakuwa tofauti?

Ukiona mtumishi anataja mapepo na uchawi lazima uweke shaka hasa kwa siku hizi (Isaya 8;20). Then mbona huku Ulaya nimekaa mda tu hawa ndio wameshiba neno la Mungu? Nina walakini sana na hizi huduma
 
Najua mtanichana. pamoja na kuwa mwakasege ni mlutheri mwenzangu mi simkubali kabisa toka alipoingiza somo la uchumi kwenye mahubiri yake. Before he was good. alipoijua shilingi mmmmh.
unajua mtu akiwa tu anaunganisha matukio ya mambo ya fedha tu anaonekana yeye ni Mgalatia,jamani dunia imebadilika sana sana,lazima injili iunganishwe na fedha,kuwa na fedha sio dhambi,dhambi ni umezipataje,na unazitumiaje,Injili bila fedha haiendiiiii.
wamissionary wanaweza kuwa wanachangia kutuingiza umaskini wa fikra....
Economics/Uchumi ulikuwepo tangu enzi hizo....sema tu ulikuwa haujapata mtu wa kuunganisha na imani....
Kiimani tunaamini katkika kutoa ndo tunapokea.....kutoa kwa asiejiweza na kutoa kwa dhamira.....
Zamani uchumi ulikuwa ni mali,kama mifugo,shamba,yaani butter trade....siku hizi Money ndo imekuwa na engine ya Uchumi,ambao huongoza idara nyingine/kuwezesha matukio yafanyike.sasa huwezi kuacha kuunganisha Watu kujua uchumi ili wazidi kupata maarifa ya kutafuta fedha na kutoa,fedha hizi husaidia pia wengine kwa njia mbalimbali kama kukuzwa kiimani,kupona,kuunganishwa nk.
Mamndenyi Habari za Mafinga.....
 
Bado tu mnataka kwenda kuliwa hela zenu na wajanja wakaendeshee Hummer?
Ama kweli bora uwe maskini kihali lakini usiwe maskini wa kujitambua kifikra.

Huyu ni mwalimu sio nabii, muhubiri au mtume kama wanavyojiita hao wengine, ni msomi wa maswala ya uchumi na ndiyo anayofundisha kwenye mikusanyiko yake, sadaka sio kipaumbele kikubwa sana kwake.

Kama unataka kuona maajabu hudhuria kwa hao manabii kina Geo Davie.........uone haswa akina mama wanavyoshindana kumkusanyia jamaa mihela a.k.a fungu la kumi walizosotea wiki nzima kwa kukaanga samaki, yaani inapofika muda wasaidizi wake wanaandaa makapu shughuli nyingine zote zinasitishwa kwa jinsi wadau wanavyopigania kuzitumbukiza.

Alafu kumbuka ni TAX FREE.

Kweli kuna watu wana bahati dunia hii, wao wanaishi maisha ya kifahari, majumba na magari ya kifahari...watoto wao ukiwasikiliza hata kwenye vyombo vya habari utawasikia wanavyojinadi "nyumbani tunaishi kama ikulu, tuna kila kitu" huku hao wanaochangishwa wako radhi familia zishindie mihogo kuliko akose pesa ya kupeleka kwenye kapu kila mwisho wa wiki.
 
Jamaa hana shida ya hela alikuwa mshauri wa uchumi wa mkapa enzi za uraisi wake, Pia alishawahi kuwa afisa mipango wa wilaya ya Arumeru na ana NGO yake inayojihusisha na masuala ya kiuchumi!
Na kufundisha neno la Mungu ameanza miaka ya 1980's hadi leo!
Ni mwalimu wa neno la Mungu na ni mwalimu mzuri pia wa masuala ya uchumi!
Kuna kanisa moja kutoka marekani lilishamwambiaga awe askofu wao masuala ya hela hayatamsumbua akakataa akasema hayuko kwa ajili ya hela!
 
Mwakasege anajiita mwalimu wa biblia,lakini kwa ufupi ni kwamba ni muongo anaezusha aliwahi kudai eti alitaka kuuwawa,mara katakiwa kuwa askofu zote hizi ni uongo.cha mwisho ni kwamba yeye na mke wake wanatumia miujiza ya uongo kama kawaida ya walokole.
 
Mwalimu Mwakasege yuko juu sana huwezi kumlinganisha na watumishi wengi kwasababu moja kubwa,hafungwi na minyororo ya madhehebu.Nimewahi kuhudhuria semina nyingi za Bwana Mwakasege sikuwahi kumsikia hata siku moja akiwaelekeza watu waende kwenye dhehebu fulani fulani.

Kuna kasoro moja kubwa ambayo nimeiona kwa Bwana Mwakasege siku za karibuni amejikita sana kuwahimiza watu kwenda Israel.Amefikia hatua ya kuandaa safari za kwenda Israel kwa wanandoa as if uponyaji unapatikana unapokwenda Israel.Bwana mwakasege ndiye aliyemshauri E Ngoyai Elowassa kwenda Israel mara baada ya kuitia hasara kubwa nchi yetu na mkataba wa RICHMOND badala ya kumshauri aombe radhi watanzania kwa uzembe anamshauri aende Israel.
Hata mimi namkubali Mwl. Mwakasege lakini huwa simwelewi anapofanya huduma mara nyingi mikoa ya Arusha, Dsm,Dom & Mwanza zaidi ya mara moja kwa mwaka na kila semina huchukua siku 7. Lakini mikoa kama Kigoma, Shinyanga, nk. anafanya semina mara moja kwa mwaka halafu inakuwa ya siku 3.
 
Christopher Mwakasege is a true servant of God. Mtawatambua kwa matunda yao. Matunda yake kwa muonekano na kwa malisho ni upendo, uvumilivu, utu wema, upole, kiasi, fadhili, unyenyekevu,amani na uaminifu.
Sasa kama haya yote tunayaona kwa mtu si ndio tunda la roho hilo, kwani tangu lini mbuyu ukazaa maembe?

Kuna mtu aliuliza sehemu kwa nini anahubiri mikoa hiyohiyo tu: Dar, Arusha, Mwanza, Dodoma, Moshi, sijui na Mbeya, na USA? Je mikoa na sehemu zingine?
 
Hizi siku za mwisho ngumu sana kujua who is who, afu hawa wachungaji mbona huku sumbawanga vijijini hawaji? Mwanza,arusha, dar jmn dhambi zikl na huku

Sumbuwanga hapaingiliki hivi hivi! Unataka waje huko kuumbuliwa matunguli yao eeeh? Si unajua tena wachungaji wa siku za mwisho kuwa ni mabingwa wa mazingaombwe makanisani!
 
Huyu ni baraka kwangu na kwa taifa langu. Najivunia kuwa na mtanzania mwenzangu kama huyo.
Kwa yule ndugu aliyesema ameona 'kasoro' ya yeye kutuhimiza kutembelea Israeli, namshauri awe anachunguza ni faida zipi huwa anatueleza za kuitembelea Israeli, kisha na wewe mwenyewe zichunguze hizo anazozisema kwa kutumia Biblia uone kama ni vyema au sivyo. Kwa maana hiyo siyo kasoro bali jambo lingine jema.

Naona watu wamekuwa wema kwa kuweka mawasiliano yake hapa, namimi nakuongezea 0713511633, hii ni namba kwa ajili ya wewe kutuma SMS na kueleza una jambo gani wataka kuombewa. Hairuhusiwi kupiga namba hii, ni SMS tuu, na kama walivyosema wengine, ni bure kabisa.

Upo mkoa gani uliyeleta mada? Wiki hii Mwakasege ana semina Arusha, kama sijakosea kuanzia tarehe 8 Sept atakuwa na semina pia Dar, so kama upo Dar unaweza kuhudhuria kabisa na huyo ndugu yako.

Halafu, hongera kwa kuja hapa kutafuta msaada zaidi kwa ajili ya ndugu yako. Keep it up.
 
Back
Top Bottom