Je kamati za Bunge kupewa posho na MASHIRIKA ni kosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kamati za Bunge kupewa posho na MASHIRIKA ni kosa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Mar 13, 2009.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Je kupewa posha na tanesco kwa kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma ya bunge ni kosa????

  Je hili halikuingiliana na interest za tanesco na kuinfluence maamuzi.

  Dowans kipimo cha utaifa mwanzo wa uzalendo. Tuvunje katiba na kanuni tumbebe Dowans.Mitambo michakavu itawaka tuu ikifa tutanunua mingine hasara ya muuza karanga faidi ya wanasiasa na wafanyabiashara matepeli na mafisadi.

  Kamati ya mahesabu ilikuwapi wapi siku zote isione tunalipa fedha nyingi agreco, iptl, songas nk. kwanini kwa dowans ndiyo ilete shida. Mtetea utawala wa sheria anapotaka sheria zivunjwe anakueleza nini???
  Tuache ushabiki tujadili mada.
   
  Last edited by a moderator: Mar 13, 2009
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Nadhani haijakaa vizuri kwa kamati kupewa posho hasa kama si kamati zote zilipewa posho. Inaelekea ile ya Shelukindo haikupewa posho!

  Hata hivyo, kwa jinsi mambo yanavyokwenda (i.e. wanakamati wamemruka Mh Zitto!) inaelekea posho haiku-influence maamuzi labda kama mwenyekiti wa kamati alipewa posho kubwa zaidi:)!
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Suala zima la waheshimiwa kupewa posho wanapokaa vikao kwenye kamati naona lina walakini mkubwa sana.

  Kama kuna haja ya posho basi inatakiwa ilipwe na bunge na wala sio watu wenye interests na vikao vya kamati.

  Tanzania conflict of interest inanuka kila sehemu. Njia ya kukwepa vishawishi na pia kutokututia sisi wananchi wasiwasi ni kwa bunge kutokukubali posho yoyote mbali ya ile wanayopewa na bunge.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,216
  Trophy Points: 280
  Kamati zote hupewa posho na taasisi husika kila wanapozitembelea. Posho hii ni halali na hulipwa kwa kiwango cha sitting alowance wanayolipwa viongozi wa taasisi husika.

  Posho sio ajabu, hata rais, makamo, PM na viongozi wowote na ujumbe wake wote, huwa wanalipwa posho anapoitwa kufungua mkutano wowote. Marupurupu ya uongozi ni posho na ndizo zinazojenga mahekalu bila mikopo. Hata EPA ilikuwa ni posho fulani hivi ila deal ilibumbuluka.
   
 5. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Posho waliyopewa rasmi ilikuwa cha mtoto hata kama ni millioni mbili! Kwanza hakuna ushahidi kama walipewa kwa sbabu hakuna sehemu walikoweka sahihi kukiri kupokea wao walipewa bahasha tu kiasi hakina mjadala ndiyo mazoea kwenye BODI nyingi za haya mashirika na ndio maana hizi BODI zinazoteuliwa kisanii bila hata kujali taaluma ni Mafisadi per se! ZZK alipewa dola za Kimarekani na Dr. Idris. Kwani wakati Dowans wanakopa pesa Stanbic na Barclays Dr.Idiris akiwa kama mweyekiti wa ACB ndio waliowadhamini. Baadaye alihamishiwa tanesco kuwa bosi kwa maslahi ya taifa(Rostam and Co Ltd.) .Kwa hiyo basi alipoona dili linanyambulika akajua mabenki watakuja moto kukamata mitambo alikimbilia Mahakamani kuzuia kisanii ili uchorwe mkakati wa kuokoa
  jahazi. Kutishiwa giza ni mbinu na mashine zitabaki hapo mpaka ukame uchongwe kama kuna mwenye ubishi aje tupambane kama marehemu Idd Amin DADA alivyomwambia marehemu Julius Nyerere miaka ile ya sabini. Hataondoka mtu hapa sio Ngeleja wala Idris Rashid wala Masha mpaka kieleweke.Hukuna mwenye ubavu sio PINDA wala JK mwenye ubavu hajitaki nini? Nilishasema Dowans(Ufisadi) ni sera ya CCM usicheze na ilani ya uchaguzi tutailinda kwa nguvu zote.
   
 6. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna ushahidi wowote kuwa waheshimiwa wanakula vya wanaotakiwa kuwashughulikia? Mh. Zitto unaweza kututhibitishia haya?
   
 7. m

  mutua12 Member

  #7
  Mar 13, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamati ya bunge kulipwa posho na shirika au wizara au Idara ya serilkali ni makosa kwa kuwa shughuli zote za kamati za bunge huratibiwana ofisi ya bunge kwa maana kwamba wanapokwenda kutembelea ofisi zingine tayari huwa wamakwisha lipwa posho zote na ofisi yao .Hivyo kulipwa kwenye vikoa hivyo ni kulipwa mara mbili kwa kazi moja hivi ni kujipatia fedha kinyume cha taratibu yaani kuiibia serikali fedha za walipa kodi.Pia ni kosa kwa shirika kulipa posho hizo na ni kuliingizia shirika ua taasisi hasara.

  Hii inonekana ni karibu kamati zote ndio maana kunakuwa na maamuzi ya hovyo kwa kuwa tayari wajumbe wame weka kitu kidogo mfukoni.

  Kinacho kubalika ni kwamba kwa kuwa vikao hivyo wakati mwingine huanza saa nne , lazima ofisi husika itayarishe breakfast na kama vitaendelea hadi mchana wajumbe lazima wapewe chakula (lunch) ili kuondoa usumbufu wa kwenda kutafuta chakula. Kwa kutumia kigezo hiki mara nyingi wanapewa fedha badala ya kupelekwa kula.Lakini si walipwe posho na chakula pia

  Hawa ni wawakilishi wetu lazima tuwape heshima inayotakiwa.
   
 8. A

  Audax JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Posho ni utaratibu wa kawaida kwa viongozi au mtu yeyote anayehudhuria semaina au mkutano.Lakini za wabunge zilipaswa kulipwa na bunge c taneco.Cna uhakika kama walilipwa ,lkn kama ni kweli walilipwa hiyo ili influnce kamati hiyo kuunga mkono maamuzi ya TANESCO .Katika njia za utojai rushwa zinazobainishwa na PCCB na hiyo ni mojawapo pia.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini posho hii ilipwe na shirika wakati wao wapo kwenye kazi ya Bunge? Kwa nini Bunge lisiwalipe?
   
 10. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mpitanjia,
  Mshahara wanaolipwa wabunge si ni kwa ajili ya kufanya hizi hizi kazi za kuiangalia serikali na mashirika yake? Kwa nini walipwe tena iwe ni na TANESCO au Bunge kwa kufanya kazi ambayo ndio inayolipa mshahara wao?
   
 11. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mishahara ya wabunge ni kwa ajili ya kazi hiyo hiyo ya kuishauri serikali. Malipo mengineyo yoyote uhalali wake ni matatani, kama sio hongo kabisa, na Bunge linatakiwa kutoa maelezo kwa wananchi.
   
 12. K

  Kasanga Member

  #12
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HIzi kamati za bunge ni wizi mtupu! Huko wanakotoka Ogsi ya bunge wanalipwa posho na ofisi ya bungekwamba wako kazini! Wakitembelea mashuirika nako wavuta tena! Jamani hii ndio Tanzania
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Pasco,

  Maneno yako hapo juu ni tatizo kubwa mno, kama hulioni hilo basi kazi ipo.

  Kama wabunge wanahitaji posho basi hiyo posho ilipwe na bunge na wala sio taasisi nyingine yeyote.

  Mfano mdogo, kama mbunge analipwa kila akijadili mambo ya Tanesco, kwanini asiidhinishe mtambo ununuliwe kwa mategemeo kwamba vikao vitaendelea kupitia maamuzi mbalimbali kuliko wakikataa ambapo zoezi litakuwa limeisha?

  Binadamu wote ni Manyang'au, kuwepo kwa sheria na utii wa sheria ndiko kunatutofautisha.
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Audax,

  Huo utaratibu wa wapi? Nini maana ya mshahara?

  Wengine tunahudhuria mikutano kila siku mbona hakuna posho?

  Nitaelewa kama mbunge analipwa allowance kuhudhuria vikao vinavyofanyika nje ya kituo chake cha kazi. Lakini hizi posho za kuhudhuria mikutano na semina ni WIZI MTUPU. Waheshimiwa wanaenda kwenye mikutano ya UKIMWI nako wanachukua posho wakati semina hizo ni muhimu kuwawezesha kupata elimu nzuri ya kupambana na hilo gonjwa.

  Tusiporekebisha haya mambo ya posho posho, pesa zote zitaendelea kuishia kwenye ulaji badala ya kwenda kwa wahusika.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nadhani hapa tunaruka hatua:

  Kwanza, Je Kamati za Bunge huwa zinalipwa posho wanapofanya vikao hivi na taasisi mbalimbali wakitekeleza majukumu yao?

  Pili, je posho hizo hulipwa na chombo wanachokichunguza, kutembelea au kukagua?

  Tatu, utaratibu huo wa posho umewekwa kwa msingi wa sheria au taratibu gani?


  Tuyajue hayo kwanza; kwa sababu; kama kamati zote zinalipwa posho kwa utaratibu unaikubalika kisheria basi hoja inakufa pale pale kwa sababu kama kinachofanywa ni ndani ya sheria (hata kama sheria ni mbaya) basi mjadala wa hii kamati moja haupo.

  Kama kamati nyingine zote hazilipwi posho na taasisi wanazozichunguza isipokuwa hii PAC basi kuna maelezo yanahitajika.
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Lakini pia tunatakiwa tuangali kuna kamati za ki-sector kama ya Madini, na hii ni ya Mahesabu( Whatch Dog) wana mashirika mangapi ya kuyapitia ? nearly yote wakichukua poshao say 100 mashiraka ya Umma Vs kamati ya ki-sector sema hiyo sector ina mashirika 10. Yupi atakuwa ina a more compromising situation especially ukiwa ndio watch Dog. Sasa hapa hata kama sheria au kanuni za Posho zinaruhusu, ukija kwenye profession ya PAC hii inaitwa Conflict of Interest, ku-neutralise this unatakiwa u-declare kama fulani bin fulani nilipopitia kampuni au shrika lake alinipa XXXX, sasa Bosi wao anaweza kusema rudisha au akaona haikuharibu kitu, kwa hiyo wanaweza kukaa nayo.
   
 17. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Dawa kwa siku zijazo ni kurekebisha utaratibu huu mbovu wa posho TZ. Watu wafanye kazi kwa mishahara yao, na wagharamiwe tu direct expenditures wanapokuwa nje ya vituo vyao (kwa maana ya halisi ya kuwa nje ya kituo).
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yeyote anayejustify kwa kamati zetu za bunge, ziwe za kudumu ama maalumu kupokea posho kutoka kwa wale wanaokutana nao kama akamati ama warsha wakati ambapo ia pia wanapokea posho kutka ofisi ya bunge/serikalini ni kwamba hana taarifa za kutosha ama ni mmoja wa wale wanaoamini kuwa rushwa na ukiukaji wa maadili ni sehemu ya utamaduni wa mtanzania.

  Kamati za bunge huwa wanapewa posho na ofisi ya bunge/serikali kila wanapokaa kama kamati nyakati ambazo bunge halipo katika kikao na mara nyingi kamati hizo hukaa wakati wa siku za kazi.

  Tayari kuna tamko la serikali kupitia kwa katibu kiongozi Luhanga kuwaonya wabunge kuwa kupokea posho mara mbili , yaani kutoka ofisi ya bunge na pia kutoka kwa asasi ama wizara za serikali ni makosa na hivyo waache kufanya hivyo.

  Tatizo ni kuwa suala hili limezoeleka kiasi cha wabunge wengi kuona kuwa ni kitucha kawaida hivyo ni halali na wakti mwengine hufikia kulazimisha kupewa posho hizo kama haki yao.

  Wapo wabunge ambao ama kwa kuwa wanaona hali yao kiuchumi ni nzuri hivyo hawahihitaji kupanga foleni kupewa vijisenti ama kwa kuwa wanaamini suala hilo linakingana na dhamira zao kama viongozi waadilifu huwa wanaepuka kupokea posho hizo.

  Wapo ambao hupokea posho hizo pale vikao hivyo vinakuwa siku za jumamosi, jumapili ama sikukuu ambako kwa kawaida huwa hawapewi posho na ofisi ya bunge kwa kuhudhuria vikao ma warsha mbalimbali.

  Hata hivyo wakati mwingine posho hizi hupokelewa na wasaidizi wao, madereva wao na wakati mwengine hata wafanyakazi wa ofisi za bunge kama vile makatibu wa kamati zao. Hapa inakuwa ngumu kusema kuwa wabunge hao wanakosea kuwaacha wasaidizi wao kufaidika na hizo posho ama wako justify na wanatenda wema.

  Wapo wabunge ambao wametokea kuthubutu kupinga suala hili la kupewa posho kutoka kwa mawizara, asasi am mashirika ya umma na yale ya kijamii wanapokutana nao katika nyaklati za kawaida za kazi ambazo pia hupewa posho na ofisi ya bunge. Wapo ambao wamejaribu kuwashawishi wenziwao kukubaliana kubadili tabia hiyo kama kamati kwa ujumla lakini ukweli hilo limeshindikana hadi sasa. Wakati mwengine suala hilo limepelekea chuki binfsi miongoni mwa wabunge kwani wengi wao wanaona suala la kupewa posho hizo ni haki yao na muhimu kwao kuwaongezea kipato kumudu maisha yao binafsi na pia kama wabunge.

  Nijuavyo mimi Zitto amekuwa akijaribu kupambana na tatizo hili tangia alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma. Hata hivyo amekuwa akikumbana na upinzani kubwa na wa wazi kutoka kwa miongoni mwa wanakamati wenzake na hata wabunge katika kamati zingine wa kutoka katika vyama vyote ambao kwaowao msimamo huo ni kujifanya "kimbelembele".

  Nijuavyo kuwa Zitto aliamua kuepuka kupokea posho hizo haswa kama vikao hivyo hufanyika katika siku za kawaida za kazi. Lakini wakati mwengine hutokea ama wasaidizi wake ama wasaidizi wa bunge ambao humuona Zitto kama mshikaji wao kupokea posho hizo, wakati mwengine wamekuwa wakimuomba kufanya hivyo na wakati mwengine kupokea bila ya kumueleza. Nijuavyo kuwa kwa kutumia moral persuasion strategy aliweza kumuinspire Makamu Mwenyekiti wake na baadhi ya wanakamati kumuunga mkono katika kuepuka kupokea posho hizo. Ni wazi kuwa kama kiongozi ni muhimu kutafuta suluhu ya tatizo ukitilia maanani ya hisia na misimamo ya wenzako unaofanya na kazi hivyo ni vigumu kulazimisha kila kitu hasa misimamo yako kukubalika na wenzako. Kumbukeni kuwa hata bungeni kuna peer values and rules ambazo ili kuwa kiongozi bora/effective one unahitaji kuziheshimu.

  Kwa ujumla suala hili ni muhimu na tete mno na tunahitaji kulijadili kwa mapana yake. Lakini pia ni muhimu kuangalia hali ilivyo katika kamati zingine nini kinaendelea hasa ile kamati ya nishati na madini ambako Mwakyembe ambaye aliamua kuspin suala hili ili kuhalalisha madai yake na kikundi chake kuwa msimamo wa Zitto ama wa yeyote mwengine anayeamini kuwa kuna umuhimu wa kuliongela suala la unuzi mitambo ya umeme ya DOWANS kwa mapana zaidi ni lazima amepewa rushwa.

  Haya ni maoni yangu binafsi...

  omarilyas
   
 19. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukimsikiliza mwakyembe utaona kuwa wao walipokuwa pale tanesco wao hawakupewa posho na dr. idrisa yaani tanesco. Na kaisema hii ya kamati nyingine kupewa posho kwa msahangao. ni vizuri tukapata taratibu za kamata za bunge zikoje.

  halafu tujue je ni kosa kupewa posho au ni utaratibu usio rasmi. na kama sio sheria zanchi au bunge kuchukua posho kutoka kwenye mashirika , hatuoni hizi kamati kuchukua fedha kinyemela ni ajabu, hasa pale kamati ya mahesabu inapokuwa inaangalia mahesabu kama yamekwenda sawa.
   
 20. t

  tk JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ninavyoelewa mimi, kamati zote za Bunge zinapotembelea mashirika, (sijui Wizara!) hulipwa posho, including kamati ya Nishati na Madini. Utaratibu huu ni wa kawaida ingawa haumo katika kanuni za Bunge au za mashirika ya Umma. Kama shirika "likipitiwa" kulipa posho, basi mjumbe wa Secretariat ya Bunge ambaye huwa anafuatana na kamati, "huikumbusha" management kuhusu posho hiyo.

  Malipo ya posho ni ziada ya chakula/vitafunio na vinywaji ambavyo pia hutolewa wakati wa mikutano.

  Nina hakika Dr. Mwakyembe anaujua utaratibu huo na ndio maana akaulizia kama posho hiyo ilitolewa kwa kamati ya Zitto, si kwa nia ya kuchunguza jambo jipya, ila ku push home the point kuwa kamati hiyo haitilii maanani hasara ya Tanesco, ama sivyo ingekataa kupokea posho toka kwenye shirika linaloendeshwa kwa hasara.

  Kamati ya Zitto isilaumiwe peke yake kwa kupokea posho, kwani utaratibu huu hata Spika Sitta anaujua na kuuidhinisha ama sivyo angekwisha "fyatuka" kama ilivyo kawaida yake ya "kufyatukia" mambo yanayo mkera.

  Ni bahati mbaya sijamuona Mh. Mwakyembe akichangia katika forum hii ama sivyo ningemuomba athibitishe haya nianyoyasema.
   
Loading...