Je kamati za Bunge kupewa posho na MASHIRIKA ni kosa?

The question should be - kwa nini wabunge walipw posho! Cynic, Mtanzania wakuu, mmezungumzia hili suala na hi ndo fundamental.
Tuanze culture ya kufanya kazi kwa mshahara - sijawahi kuona posho zinatolewa kiholela kama ktk nchi zetu za kiafrika lakini Tanzania tunatia fora!
Mbunge anapokaa katika kamati asipewe posho maana yuko kazini, full stop!
 
MKJJ kama umesikiliza BBC jana jinsi wazir wa Fedha wa Kenya anavyoongea na mipango yao juu ya Hili Tatizo la Uchumi wao wanajiandaaje,,,Bahati mbaya TZ Wazir wetu fedha kalala hata kusema kajiandaaje kashindwa,,,

Posho wanazopewa wabunge ni kero, wakati mwingine hata kikao hakai ila anasign na kuchuku bahasha yake,,,na sometimes wanalazimisha kupewa pesa, na wanalipwa kama wanavyolipwa wakurugenzi,,,min 500,000 per day,,,,wakati mwingine kikao kinasogezwa makusudi,,,wabunge wetu bado MAFISADI tu na wao, na piga debe pale tu mchongo unapokwenda kwa wengine,,,,Hata pale wanapokwenda Nje ya nchi,,,wakipewa pesa zikibaki hawarudishi,,,,,,wanazikwapua!!!! sasa watu kama hao huwezi fikiria wana guts na Hali za watanzania,,,,

Mapambano bado kabisaaa,,,,,ndio yale ya BOT watu wapo kazini na bado vikiwekwa vikao wanalipwa,,,,Ajabu sana,sasa wajiuliza wao kazi zao ni nini Hasa?
 
Mnanikumbusha enzi za shirika la mecco, auditor anatumwa mbeya kwenda kufanya audting, anashukia mbeya peak, anapelekewa bahasha pale, pamoja na vifurushi vya mchele wa kyela , anaandika ripoti akiwa hotelini!!!
 
Posho wanazolipwa wabunge kwenye mashirika ni nono na ndio sababu wanagombania kwa namna mbalimbali kuwa wajumbe katika kamati za bunge.Kinachosikitisha ni pale wanapopokea posho nono hata kwenye shirika lililotaabani kama Tanesco.
 
Nadhani hapa tunaruka hatua:

Kwanza, Je Kamati za Bunge huwa zinalipwa posho wanapofanya vikao hivi na taasisi mbalimbali wakitekeleza majukumu yao?

Pili, je posho hizo hulipwa na chombo wanachokichunguza, kutembelea au kukagua?

Tatu, utaratibu huo wa posho umewekwa kwa msingi wa sheria au taratibu gani?


Tuyajue hayo kwanza; kwa sababu; kama kamati zote zinalipwa posho kwa utaratibu unaikubalika kisheria basi hoja inakufa pale pale kwa sababu kama kinachofanywa ni ndani ya sheria (hata kama sheria ni mbaya) basi mjadala wa hii kamati moja haupo.

Kama kamati nyingine zote hazilipwi posho na taasisi wanazozichunguza isipokuwa hii PAC basi kuna maelezo yanahitajika.

Mwanakijiji,

Sio kila jambo linalofanywa kulingana na sheria zilizopo ni sawa. Hata kama sheria inawaruhusu kulipwa posho lakini huu unaweza kuwa mwanzo wa conflict of interest.

Pia pesa badala ya kuwafikia walengwa zinaishia kwenye matumbo ya waheshimiwa.

Mtu yeyeote anastahili kulipwa allowance kama anatumwa kufanya kazi nje ya kituo chake ili aweze kuishi huko alikoenda. Sioni sababu ya kumlipa mtu posho pale anapotimiza majukumu yake ya kila siku ya kazi yake.

Hizi posho ndio zinawafanya wabunge wengi hata wasipite kwenye majimbo yao. Hakuna cha uhalali au sheria, ni wizi mtupu!
 
Ninavyoelewa mimi, kamati zote za Bunge zinapotembelea mashirika, (sijui Wizara!) hulipwa posho, including kamati ya Nishati na Madini. Utaratibu huu ni wa kawaida ingawa haumo katika kanuni za Bunge au za mashirika ya Umma. Kama shirika "likipitiwa" kulipa posho, basi mjumbe wa Secretariat ya Bunge ambaye huwa anafuatana na kamati, "huikumbusha" management kuhusu posho hiyo.

Malipo ya posho ni ziada ya chakula/vitafunio na vinywaji ambavyo pia hutolewa wakati wa mikutano.

Nina hakika Dr. Mwakyembe anaujua utaratibu huo na ndio maana akaulizia kama posho hiyo ilitolewa kwa kamati ya Zitto, si kwa nia ya kuchunguza jambo jipya, ila ku push home the point kuwa kamati hiyo haitilii maanani hasara ya Tanesco, ama sivyo ingekataa kupokea posho toka kwenye shirika linaloendeshwa kwa hasara.

Kamati ya Zitto isilaumiwe peke yake kwa kupokea posho, kwani utaratibu huu hata Spika Sitta anaujua na kuuidhinisha ama sivyo angekwisha "fyatuka" kama ilivyo kawaida yake ya "kufyatukia" mambo yanayo mkera.

Ni bahati mbaya sijamuona Mh. Mwakyembe akichangia katika forum hii ama sivyo ningemuomba athibitishe haya nianyoyasema.

TK,

Hata kama ni utaratibu ambao unafanywa na kila kamati, bado ni utaratibu mbovu ambao inatakiwa tuupigie kelele.

Posho zinaweza kuwa chanzo cha conflict of interest na pia kuwafanya waheshimiwa wajadili jambo moja kwa muda mrefu badala ya kutoa maamuzi mapema.

Mimi niliwahi kuomba tender sehemu huko mikoani, nikashangaa kuambiwa inatakiwa nigharamie posho za wajumbe wote wa kikao. Nikauliza kwanini? Wakasema ndio utaratibu
na usipolipa hilo suala lako halitajadiliwa.

Obvious hapo kulikuwa na conflict of interest iliyo wazi. Mimi ambaye naomba tender, ndio tena niwalipe hao wanaojadili tender yangu? Sikuamini hilo jambo hata baada ya kuambiwa ni utaratibu.

Niliwalipa lakini moyoni niliamini kabisa hiyo pesa haina tofauti na kulazimishwa kutoa rushwa ili upate huduma. Tena wanahitaji pesa nyingi mno. Sasa je mtu ambaye hana hizo pesa za ziada kweli ataweza kushindana kihalali katika tenda za namna hiyo?

Hizi posho zilizo nyingi ni uwizi mtupu na ifike mahali zipigwe marufuku ili kuondoa uwezekano wa waheshimiwa wetu kuwa influenced kupitia hizi posho.
 
:(
Kamati zote hupewa posho na taasisi husika kila wanapozitembelea. Posho hii ni halali na hulipwa kwa kiwango cha sitting alowance wanayolipwa viongozi wa taasisi husika /QUOTE]

Kamati ya Bunge kupewa posho na mashirika ya Umma si vizuri na hasa posho inapotolewa na kila Shirika kwa kila kikao cha Kamati inapojadili. Tukichukua mfano wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma hupewa posho na kila Shirika wanalolijadili. Kwa siku hujadili takribani mashirika sita. Ingawa inasemekana kuwa Shirika halilazimiki kutoa posho lakini ukweli ni kwamba Shirika hushinikizwa kwa namna mmoja au nyingine kutoa posho kwa kiwango kisichopungua Sh. 80,000/= kwa kila mjumbe (Imagine ni kiasi gani Wajumbe wananufaika tena bila kukatwa kodi = 6 x 80,000/= x Idadi ya mashirika yanayojadiliwa). Inasemekana Jumla ya mashirika ya umma hayapungui 188. Ni vizuri swala hili Waheshimiwa Wabunge wakafikiria kuachana nalo.
 
Mwanakijiji,

Sio kila jambo linalofanywa kulingana na sheria zilizopo ni sawa. Hata kama sheria inawaruhusu kulipwa posho lakini huu unaweza kuwa mwanzo wa conflict of interest.

Pia pesa badala ya kuwafikia walengwa zinaishia kwenye matumbo ya waheshimiwa.

Mtu yeyeote anastahili kulipwa allowance kama anatumwa kufanya kazi nje ya kituo chake ili aweze kuishi huko alikoenda. Sioni sababu ya kumlipa mtu posho pale anapotimiza majukumu yake ya kila siku ya kazi yake.

Hizi posho ndio zinawafanya wabunge wengi hata wasipite kwenye majimbo yao. Hakuna cha uhalali au sheria, ni wizi mtupu!

Mtanzania, wala hilo halina mjadala. Unachozungumzia ni principle inayotakiwa kuwa, hilo haliendani na ukweli au habari iliyotolewa hapa. Kama sheria inaruhusu kulipwa posho, na hakuna kitu kinachokataza conflict of interests au kanuni za wazi za nini conflict na jinsi ya kuiresolve basi hakuna mjadala.

Hatuwezi kusema tu "wizi mtupu" tukimaanisha kuwa kuna makosa wakati hakuna; hakuna makosa hakuna wizi! It is as simple as that. Tukitaka tuseme wizi, tutengeneze makosa. Sivyo?
 
Back
Top Bottom