Je, JamiiForums itafunguliwa Tarehe 6 Desemba?

Je, JamiiForums itafunguliwa Tarehe 6 Desemba?

Ma mbwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
1,386
Reaction score
3,451
Wakuu kama mna kumbukumbu ni kwamba tarehe 6 sept 2025 mamlaka ya mawasiliano iliifungua JF kwa siku 90 kutokana na makosa walioona wao kuwa JF wamekiuka.

Na kwa siku 90 ni kwamba zinaisha kabla ya tarehe 6 DEC.

Je, kwa fukuto hili la Dec 9 mamlaka watairudisha kweli hewani JF yetu pendwa?
 
JF ni kama mvua ,hauwezi kuzuia mvua ikiamua kunyesha inanyesha tu. #JF MOTO CHINI.
 
Je, 9D tutaandamana kweli au tunadanganyana huku mtandaoni??

Kama hatuandamani mseme wengine tuache kujiandaa.
Maandalizi yanaendelea na yamepamba moto..Tik tok kuna Jamaa anaitwa Habil ndiye architect wa hayo maandamano na ameanza kuandika barua kwenda taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo vyombo vya habari..

Itakua ni mshikemshike kwelikweli.
 
Iwe, isiwe hawana ubavu wa kupitisha muda, la sivyo meno yatawadondoka kwa mdomo kama siyo kupukutika.
 
Hivi ilifungiwa?

Wote walioua watanzania nao watakufa kifo kibaya cha maumivu makali
 
walifungua siku chache baada ya uchaguzi, wakafunga tena baada ya uzi huu kupamba moto
 
Duh! Kumbe waliwahi kuufungua? Sema wanaotumia opera mini browser wenyew wanajiachia tu bila wasiwasi
 
Kuna namna najiona saana mkosaji ndani ya nafsi yangu kwa maana namna moja au nyingine nimeshiriki uchaguzi huu😭😭
 
Back
Top Bottom