Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa?


zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo maana inagusa moja ya topic zenye utata katika ulimwengu wa imani ila ningependa tusome kwa utulivu uzi wote alafu tujadiliane kwa hoja ili tuweze kusolve hili swali la karne nyingi sasa.
images-72-jpg.929882

UTANGULIZI
Mwanzoni kulikuwa na agano kati ya wanadamu na Mungu kupitia Adam ila tunaona Adam analivunja agano hili

(Hosea 6:7)
Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu;

Hivyo Mungu alitaka kurudisha uhusiano tena na mwanadamu tunaona akapatikana Nuhu ambaye alimcha Mungu sana na akachaguliwa kuianza dunia upya baada ya gharika. Sasa baada ya gharika dhambi ilirudi tena kupitia Ham ambaye alipelekea Nuhu kumlaani mwana wake Ham yaani canaan kuwa atakuwa mtumwa wa kaka zake Ham yaani Shem na Yapheth (Hili la muhimu sana huko mbeleni) hivyo uzao wa Ham ukawa na watu waovu sana mfano Nimrod wa Babylon aliyeleta ibada za sanamu na dini za kipagani hadi kuleta machafuko kwenye ukoo wa Nuhu na kusababisha dunia nzima kumuacha Mungu wa Nuhu.

Katika sintofahamu hii aliyesimama imara alikuwa Shem/Melchizedek ndie aliendelea kushika wokovu na hata Abraham alipozaliwa aliendelea kumsimamia kiimani na hivyo hata alipokufa Abraham kati ya wanadamu wengi ndio aliendeleza imani ya kumuabudu Mungu wa babu zake (YAHWEH) hivyo baada ya Mungu kuona Abraham ana msimamo thabiti kwake akampa ahadi ya kuwa na uzao wa watu wengi kama nyota za angani lakini pia alimpa ahadi ya kumpa nchi hii ya canaan.

Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

Hivyo ni kupitia ahadi hii ndipo taifa la Israel lilipotabiriwa rasmi kuwepo. Na ahadi hiyo itakuja kutekelezwa na mjukuu wake yaani Yakobo ambaye aliiba urithi wa mtoto wa kwanza hivyo hii baraka ya Abraham akairithi yeye na tunaona uzao wake kupitia Joshua na Caleb ndio wanaingia kwenye nchi hii ya canaan rasmi na kuasisi taifa la Israel.

Je Mungu aliichagua Israel??

Kumb. La torati 7:6
6 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.

Kupitia mstari huu tunaona Israel ilichaguliwa na Mungu lakini je kwanini aliichagua??

Kumb. Torati 7:7-8
7 BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;
8 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu.

Hivyo Mungu aliwachagua Israel sababu hiyo ya kutimiza uapo kwa mababu ikiwemo Nuhu + Abraham. Na hili ndio lilisababisha Israel wapewe nchi ya Canaan sababu ilikuwa inahitimisha unabii wa Nuhu kuwa Canaan atakuwa mtumwa wa shem (Babu wa Abraham) na sio kwa sababu nyingine yeyote.

Mwanzo 9
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake

images-74-jpg.929883

Ramani ya canaan

Hivyo baada ya Agano hili na Israel ambalo kupitia wao ndio Mungu alipanga kuwaletea Messiah yaani Yesu ili aweze kurejesha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu kama wa kipindi cha Adamu lakini wayahudi walimkataa Yesu kwa sababu hawakujua kutafsiri unabii ulioandikwa kuhusu maisha ya Yesu kwenye agano la kale. Kwa kifupi maisha yote ya Yesu kuanzia kuzaliwa mpaka kufa yalikuwa yanaendana na unabii wa agano la kale 1 korinto 15:1-4 Mfano wa nabii zilizotimizwa kupitia maisha ya Yesu ni hizi. Kuanza mahubiri yake galilaya ulitabiriwa na Isaya 9:1-2 na ukatimia Mathayo 4:13, Pia Yesu kupanda Punda kuingia jerusalem ulitabiriwa na Zakaria 9:9 na kutimia Mathayo 21:1-9 n.k yaani kuna mistari zaidi ya 100 iliyotabiriwa kuonyesha Huyo Messiah ataishije.

Lakini wao wayahudi hawakuliona hili sababu walidhani Yesu atakuwa handsome boy, Damu ya kifalme,Mwanajeshi kama alexander the great n.k hivyo kwa jinsi alivyokuja "kimasikini" wakaona kama anakufuru mwisho wa siku wakamuua na yote ni kutokana na kushindwa kutafsiri maandiko ya unabii.

Matendo 13:26-27

27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
AFTERMATH
Hivyo basi kwa kuwa Mungu alikwisha dhamiria kurudisha uhusiano na mwanadamu ikabidi ageukie mataifa mengine ambayo ndio yangeendeleza agano lile na hapo ndipo likapatikana agano jipya ambapo neema ya wokovu haukuwa wa Wayahudi pekee sababu walimkataa bali ukawa wa mataifa yote as long as watamfuata Yesu (Yohana 1:11-12) pia Mathayo 21:42-43 ambapo tunaona ufalme wa Mungu umehamishwa kutola Israel kwenda kwa mataifa mengine.

42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?
43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.


images-73-jpg.929907


Swali linaibuka je Israel inabakia taifa la Mungu??

NDIO ni kweli Mungu aliendelea na agano na taifa la Israel ila tafsiri ya taifa la israel ni lipi limebadilika kupitia agano jipya.

Warumi 9
6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.
7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.


Na pia hapa ndipo tunaona kunazaliwa waisraeli wa kimwili (mashariki ya kati) na Israel ya Kiroho (wakristo)

Warumi 2:28-29
28 Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.


Hivyo kufikia hapa tunaona kuna wayahudi/waisrael aina mbili sasa je ahadi za ISRAEL ya agano la kale anarithi nani za kuwa taifa teule,chaguo la Mungu n.k

Galatia 3
6 Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu
.
.......................................
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.Ahadi kwa Abrahamu
..............................
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.


Kupitia mistari hii tunaona sasa ahadi zote walizopewa Abraham na Israel zinarithiwa rasmi na wale wote wamfuatao Yesu yaani wakristo ambao ndio wale paulo kawaita waisrael wa Kiroho sio kimwili. Hivyo ningependa nichukue fursa hii kutoa msimamo wangu kwamba Israel hii ya kimwili sio taifa la Mungu na halitokaa liwe unless na wao wamfuate Yesu hapo ndipo watakuwa NCHI YA AHADI na taifa la Mungu. Kwa kuhitimisha kupitia agano jipya ambapo sasa wanaomfuata wote Yesu bila kujali ni muisrael au lah ndio wanakuwa TAIFA TEULE ama ISRAEL hivyo baraka zote ahadi zote na unabii wote wa TAIFA LA ISRAEL sio tena wa hii Israel ya yakobo bali ni wote wamfuatao Yesu kristo na hii ni kwa mujibu wa Biblia.

However upande kinzani unasema Israel ya mashariki ya kati bado ni taifa teule kama zamani na hakuna kilichobadilika na wanatumia mstari huu.

Warumi 3:3-4
3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?
4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.


Nakubaliana na Mstari huu unaosema Mungu hajawaacha wayahudi licha ya kumkataa lakini bado msimamo uko pale pale kwamba ni lazima wamkiri massiah ndio wawe teule till then hawana tena hadhi ya kuitwa taifa teule kulingana na vifungu nilivyoweka.
images-71-jpg.929908


ANGALIZO
Kumekuwa na interpretation nyingi sana za unabii kuhusu Israel ya kimwili yaani hii ya mashariki ya kati na nina hofu kuwa na wakristo pia wameingia mkenge kama wa wayahudi wa kale kwa kutoelewa unabii na wakatafsiri kwa akili zao kiasi kwamba Yesu alipokuja hawakujua na wakamkataa. kuna wakristo wengi leo wanaamini vita na matetemeko yaliyotabiriwa kwenye ufunuo ni ya kimwili au hekalu litajengwa kimwili hivyo watashituka Yesu amekuja kivingine wao bado wanasubiri vita ya amragedon sijui kujengwa hekalu ilihali hizo mambo zina maana tofauti kabisa ingawa hii ni mada ya siku ingine ila nachoweza hitimisha ni kwamba Biblia imeandikwa kwa codes nyingi hivyo kuitafsiri inahitaji umakini na utulivu sana sio kwenda kichwakichwa mfano inapotabiri kuwepo kwa njaa na kiu haimaanishi njaa ya kimwili ila ukisoma Amos 8:11 utajua njaa inaongelewa ni ya kusikiliza neno la Mungu such phrases mtu akisoma kwenye ufunuo ana conclude kuwa kutakuwa na njaa,vita matetemeko,ukame huu wa kimwili kumbe zina maana nyingine kabisa hivyo nilitaka kuliweka hilo sawa. Kwa kusema hayo naomba kuwasilisha mada kwa ajili ya michango na maoni ya wanajukwaa letu pendwa.

Cc cc Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
 
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2008
Messages
3,011
Points
2,000
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2008
3,011 2,000
Katika mada zako nilizozipitia hii umeitendea haki, yaani umefanya uchambuzi wa kimwili na kiroho kama mkristo, maana mada zako nyingi sana naziona ukichambua unasahau kutizama upande wa kiroho.

Uko sahihi, zitto junior, watu wengi wanasahau laana aliyopewa kaanani na babu yake na kusema ni ugomvi ismail na isack wakati ni laana kwamba kaanani atatawaliwa na ndugu zake ambao ndio hao wakina Israel.

NB: Kuna mahali nimekusoma ukitoa baadhi ya references zako, naomba usikilize mahubiri ya jamaa anajiita Mwalimu mwakasege ni mzuri sana ukisiliza atakufanya utizame bibilia kwa utafauti kabisa.
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,063
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,063 2,000
Kuna mstari huu Roman 11:11~32 hapa kuna sababu na lengo la wokovu kuwafikia mataifa na bado hio nchi ya Israel kubakia kuwa nchi ya ahadi.Kilichoko pale ni kama equation iliobalance.

Kuna member nimesoma uzi wake mzuri wa "kuzaliwa kwa ndama mwekundu /red heifer"" utaona kwamba bado kuna unfinished business ilio chini kwa chini na ktk wakati itadhihirika tu.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Kuna mstari huu Roman 11:11~32 hapa kuna sababu na lengo la wokovu kuwafikia mataifa na bado hio nchi ya Israel kubakia kuwa nchi ya ahadi.Kilichoko pale ni kama equation iliobalance.

Kuna member nimesoma uzi wake mzuri wa "kuzaliwa kwa ndama mwekundu /red heifer"" utaona kwamba bado kuna unfinished business ilio chini kwa chini na ktk wakati itadhihirika tu.
Mkuu nafikiri nimeeleza vizuri kwenye uzi kuwa Israel ni nchi ya ahadi ila hyo Israel sio ile ya mashariki ya kati bali ni Israel ya kiroho yaani WAKRISTO labda unieleze mtume paulo alimaanisha nini kusema wayahudi wa kiroho ndio warithi wa ahadi za Abraham.

Kuhusu Huyo ndama nshaeleza siyo unabii kutimia bali watu wanapotosha mafunuo ya Biblia..... Hekalu litakalojengwa sio la kimwili wakuu ni la kiroho so hata huyo punda hana significance yeyote kwenye unabii bali watu wachache wanawachezea akili na nyie mnakubali.... Mfano hiyo Israel ya sasa iliamuliwa na wazungu wapagani na sio manabii wa Mungu sasa kivipi mnaihusisha na unabii hadi muwaite taifa la Mungu??

Je ina maana leo Trump akiitisha vita megido mtasema ndio Armageddon imefika?? Guys watch out.... Ufunuo inasema armageddon itapiganwa kwa mapanga na farasi je unaweza nisaidia vita za siku hizi zinatumia mapanga na farasi??

Msitafsiri maandiko kwa kuchagua kama hekalu litajengwa nisaidie na vita ya mapanga na farasi itawezekanaje ilihali kuna nuclear cku hizi!!!
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Katika huo mstari kuna mzabibu wa Asili (Israel) na mzabibu mwitu (mataifa) kwamba hata huu mzabibu asili una wakati wake na agano alilofanya Mungu na Ibrahim lilikuwa la milele lisilo na ukomo.
Mkuu hakuna aliyekataa kuwa agano ni la milele ila swali je huyo mrithi wa hilo agano ni Kina Netanyahu au wakristo??

Wagalatia mistari zaidi ya 6 nimeweka hapo inasema warithi wa Baraka na ahadi zote za Abraham ni WAKRISTO na sio wayahudi wa kimwili sasa ni wapi mnatoaga hizi mambo kuwa Israel ya kina netanyahu ni taifa la Mungu.

Kama una object nielezee paulo alimaanisha nini kwenye hiyo mistari
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Cc Son of Gamba Mnabuduhe SANCTUS ANACLETUS SALA NA KAZI mitale na midimu AROON lifecoded nasubiri michango yenu wakuu
 
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Messages
9,305
Points
2,000
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2015
9,305 2,000
propaganda...
Mkuu binafsi naunga mkono hoja Yako Yote na huo ndio ukweli.
Propaganda za kuwahusudu waisraeli wa tel aviv kudhani kuwa wanakitu cha ziada katika mpango wa wokovu wa mwanadamu baada ya Yesu ni Utovu wa uelewa wa maandiko na ni propaganda za kikristo.

Propaganda hizo waliendelea kuwa nao hadi wakristo wa kanisa la awali wenye asili ya kiyahudi. Ila Bibilia iko wazi Yesu alikuja kwa ajili Ya ulimwengu wote. Na Waefeso ikaweka wazi alikujq kuondoa kiambaza kilichotutenga, na warumi ikasema sisi tulio mzabibu mwitu tumenyiwa artificial grafting kwenyenmzabibu mkuu.

Kwa Sababu naunga mkono hoja, Nisinene Mengi labda kama kuna mawazo kinzani ya kujadilisha huko mbele ya mjadala.

Barikiwa
zitto junior
 
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
3,001
Points
2,000
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
3,001 2,000
Cc Son of Gamba Mnabuduhe SANCTUS ANACLETUS SALA NA KAZI mitale na midimu AROON lifecoded nasubiri michango yenu wakuu

Kijana nakushukuru sana kwa kunialika. Umejitwika suala jema sana kiimani.

1. Umeeleza vizuri historia ya Wayahudi toka wanachaguliwa kuwa Taifa sample kwa ajili ya ukombozi Wa mwanadamu. Mungu katika kumkomboa mwanadamu aliamua kuanza na Taifa fulani,Israeli,ili kwamba kutokea hapo kazi hiyo iendelee kwa mataifa mengine pia. Ukisoma Maandiko Vizuri utagundua kwamba Mungu anatushirikisha mambo mengi muhimu ya maisha yetu kuanzia uumbaji hadi ukombozi wetu. Alipotuumba alitupatia Kazi ya kuendeleza uumbaji. Na alipoamua kutukomboa aliamua kulitumia Taifa la Israeli kwamba kutokea kwao Kazi ya utume na ukombozi Wa watu wake uendelee kote duniani.

3. Taifa la Israel Leo limebakia na ile hadhi tu ya kwamba kwa njia yake kazi ya ukombozi iliwafikia wanadamu wote. Taifa jipya Leo ni Kanisa lake Kristu.

4. Wale wanaoamini kwamba Israeli ni Taifa Teule hata leo wanakosea. Ni Taifa teule kihistoria tu. Mungu Leo analo Taifa lake teule na Jipya ambalo ndio Kanisa.

5. Wale wanaoliona Taifa la Israeli kama Taifa la maana sana kiimani ni wale wanaosoma Biblia kwa kurukaruka.
 
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Messages
679
Points
1,000
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2012
679 1,000
Asante kwa bandiko zuri na hoja fikirishi. Kwa kiasi fulani nimekuelewa hiyo dhana ya Israel kiroho.

Halafu huyu Yakobo (Dotto) aliiba Baraka za pacha wake Essau (Kurwa) akaachwa hivi hivi tu.. Lengo lilikuwa nini? Mungu alibariki wizi? Yaani ina maana taifa la Israeli ambalo limetokana na Yakobo lilianzishwa kwa misingi ya wizi na utapeli?
Taifa teule ni taifa la kitapeli? Haki ya Essau iko wapi?
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Asante kwa bandiko zuri na hoja fikirishi. Kwa kiasi fulani nimekuelewa hiyo dhana ya Israel kiroho.

Halafu huyu Yakobo (Dotto) aliiba Baraka za pacha wake Essau (Kurwa) akaachwa hivi hivi tu.. Lengo lilikuwa nini? Mungu alibariki wizi? Yaani ina maana taifa la Israeli ambalo limetokana na Yakobo lilianzishwa kwa misingi ya wizi na utapeli?
Taifa teule ni taifa la kitapeli? Haki ya Essau iko wapi?
Nafikiri shida ilianzia kwa Esau alipokubali kuuza haki yake ya uzao wa kwanza ndio ikampa confidence Yakobo kuwa yeye ndio anastahili baraka za ''first born'' ikapelekea atumie ujanja mwingi ili aweze kutumia hiyo fursa aliyoachiwa na Esau.

Pili kwenye Biblia Mungu alikuwa anaheshimu sana maamuzi ya watu wake mfano Nuhu alimlaani Canaan kisa dhambi ya baba yake yaani Ham na Mungu aliitimiza laana hiyo kwa kuangamiza kizazi chote cha canaan kupitia Israel.....

So Mungu habariki wizi bali ametuachia free will ya kuamua hatma yetu yeye anasimamia tu.... Sasa Isaka ndio kambariki Yakobo hapo Mungu azuie tena ilihali ni maamuzi ya Isaka mwenyewe!!! Ila kama wamgemshirikisha Mungu kabla ya kutoa hizo baraka huenda ndio Mungu angeingilia na kumpa haki yake Esau!!

Muhimu hapa ni kumshirikisha Mungu mapema ndio hatoruhusu walaghai kama Yakobo kujipenyeza.
 
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Messages
679
Points
1,000
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2012
679 1,000
Nafikiri shida ilianzia kwa Esau alipokubali kuuza haki yake ya uzao wa kwanza ndio ikampa confidence Yakobo kuwa yeye ndio anastahili baraka za ''first born'' ikapelekea atumie ujanja mwingi ili aweze kutumia hiyo fursa aliyoachiwa na Esau.

Pili kwenye Biblia Mungu alikuwa anaheshimu sana maamuzi ya watu wake mfano Nuhu alimlaani Canaan kisa dhambi ya baba yake yaani Ham na Mungu aliitimiza laana hiyo kwa kuangamiza kizazi chote cha canaan kupitia Israel.....

So Mungu habariki wizi bali ametuachia free will ya kuamua hatma yetu yeye anasimamia tu.... Sasa Isaka ndio kambariki Yakobo hapo Mungu azuie tena ilihali ni maamuzi ya Isaka mwenyewe!!! Ila kama wamgemshirikisha Mungu kabla ya kutoa hizo baraka huenda ndio Mungu angeingilia na kumpa haki yake Esau!!

Muhimu hapa ni kumshirikisha Mungu mapema ndio hatoruhusu walaghai kama Yakobo kujipenyeza.
Ufafanuzi mzuri sana..

Hata hivyo hili suala la kuuza/kununua baraka kama korosho limekaa kinadharia sana..
 
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Messages
679
Points
1,000
Travic

Travic

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2012
679 1,000
Nafikiri shida ilianzia kwa Esau alipokubali kuuza haki yake ya uzao wa kwanza ndio ikampa confidence Yakobo kuwa yeye ndio anastahili baraka za ''first born'' ikapelekea atumie ujanja mwingi ili aweze kutumia hiyo fursa aliyoachiwa na Esau.

Pili kwenye Biblia Mungu alikuwa anaheshimu sana maamuzi ya watu wake mfano Nuhu alimlaani Canaan kisa dhambi ya baba yake yaani Ham na Mungu aliitimiza laana hiyo kwa kuangamiza kizazi chote cha canaan kupitia Israel.....

So Mungu habariki wizi bali ametuachia free will ya kuamua hatma yetu yeye anasimamia tu.... Sasa Isaka ndio kambariki Yakobo hapo Mungu azuie tena ilihali ni maamuzi ya Isaka mwenyewe!!! Ila kama wamgemshirikisha Mungu kabla ya kutoa hizo baraka huenda ndio Mungu angeingilia na kumpa haki yake Esau!!

Muhimu hapa ni kumshirikisha Mungu mapema ndio hatoruhusu walaghai kama Yakobo kujipenyeza.
Ufafanuzi mzuri sana..

Hata hivyo hili suala la kuuza/kununua baraka kama korosho limekaa kinadharia sana..
 
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
3,001
Points
2,000
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
3,001 2,000
propaganda...
ntapita mkuu
Hakuna cha propaganda. Unapaswa kuelewa kuwa ule uteule Wa Israeli kwa Mungu umebakia Wa kihistoria. Sasa Taifa teule ni Kanisa lake Kristu. Kwa njia ya Kanisa watu wake tunakombolewa kutoka dhambini kwa ubatizo kuondoa dhambi ya asili na sakramenti ya upatanisho kutuondolea dhambi zingine tunazozitenda baada ya ubatizo.
 
AlP0L0

AlP0L0

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2011
Messages
4,653
Points
2,000
AlP0L0

AlP0L0

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2011
4,653 2,000
Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

Hivyo ni kupitia ahadi hii ndipo taifa la Israel lilipotabiriwa rasmi kuwepo Na ahadi hiyo itakuja kutekelezwa na mjukuu wake yaani Yakobo ambaye aliiba urithi wa mtoto wa kwanza hivyo hii baraka ya Abraham akairithi yeye na tunaona uzao wake kupitia Joshua na Caleb ndio wanaingia kwenye nchi hii ya canaan rasmi na kuasisi taifa la Israel.
Mwalimu sijafahamu hapo.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Mwalimu sijafahamu hapo.
Huyo Esau baada ya kutoka kwenye "mishe" zake alirudi amechoka sana hivyo akaahidi kutoa chochote ilimradi Yakobo amuandalie chakula. sasa akaamua kutoa haki yake kma mzaliwa wa kwanza kwenda kwa Yakobo hivyo automatically ikawa Yakobo ndio mzaliwa wa kwanza.

Sasa wakati Isaka anakaribia kufa alimuita mzaliwa wa kwanza ila kwa kuwa Yakobo alishakuwa ameuziwa hiyo haki akatumia fursa kumrubuni Esau hadi yeye ndio akawekewa mikono ya baraka na kwakuwa Isaka alikuwa haoni vizuri basi akabariki tu bila kujua.

Hivyo kimaandiko ile baraka ya Abraham ambayo iliritihiwa na isaka sasa ikarithiwa na Yakobo ndio maana Mungu alipotaka kutimiza agano lake na Abraham akaenda kwa familia ya Yakobo na Sio Esau au ukoo mwingine yeyote.

I hope nimeeleweka kidogo
 
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Messages
9,305
Points
2,000
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2015
9,305 2,000
Hakuna cha propaganda. Unapaswa kuelewa kuwa ule uteule Wa Israeli kwa Mungu umebakia Wa kihistoria. Sasa Taifa teule ni Kanisa lake Kristu. Kwa njia ya Kanisa watu wake tunakombolewa kutoka dhambini kwa ubatizo kuondoa dhambi ya asili na sakramenti ya upatanisho kutuondolea dhambi zingine tunazozitenda baada ya ubatizo.
Hicho unachokisema ndio nakiita propaganda. Wale wanabaki kama Jumba la Makumbusho tu, Wanaoption Mbili waingie Kuwa wafuasi wakristo au wanganganie Judaism wapotee kama ndugu zao waliochinjwa 70AD.

Kuhusu sacrament, ubatizo, mara kikundi flani kinachodhani ni kanisa halisi la kristo hiyo ni mada nyingine maana, Wakristo wanatambuliwa kwa kufuata maagizo ya Kristo sio '' Kujiita wakristo''.
 

Forum statistics

Threads 1,295,462
Members 498,334
Posts 31,212,940
Top