zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,035
- 28,669
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo maana inagusa moja ya topic zenye utata katika ulimwengu wa imani ila ningependa tusome kwa utulivu uzi wote alafu tujadiliane kwa hoja ili tuweze kusolve hili swali la karne nyingi sasa.
UTANGULIZI
Mwanzoni kulikuwa na agano kati ya wanadamu na Mungu kupitia Adam ila tunaona Adam analivunja agano hili
(Hosea 6:7)
Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu;
Hivyo Mungu alitaka kurudisha uhusiano tena na mwanadamu tunaona akapatikana Nuhu ambaye alimcha Mungu sana na akachaguliwa kuianza dunia upya baada ya gharika. Sasa baada ya gharika dhambi ilirudi tena kupitia Ham ambaye alipelekea Nuhu kumlaani mwana wake Ham yaani canaan kuwa atakuwa mtumwa wa kaka zake Ham yaani Shem na Yapheth (Hili la muhimu sana huko mbeleni) hivyo uzao wa Ham ukawa na watu waovu sana mfano Nimrod wa Babylon aliyeleta ibada za sanamu na dini za kipagani hadi kuleta machafuko kwenye ukoo wa Nuhu na kusababisha dunia nzima kumuacha Mungu wa Nuhu.
Katika sintofahamu hii aliyesimama imara alikuwa Shem/Melchizedek ndie aliendelea kushika wokovu na hata Abraham alipozaliwa aliendelea kumsimamia kiimani na hivyo hata alipokufa Abraham kati ya wanadamu wengi ndio aliendeleza imani ya kumuabudu Mungu wa babu zake (YAHWEH) hivyo baada ya Mungu kuona Abraham ana msimamo thabiti kwake akampa ahadi ya kuwa na uzao wa watu wengi kama nyota za angani lakini pia alimpa ahadi ya kumpa nchi hii ya canaan.
Mwanzo 15
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Hivyo ni kupitia ahadi hii ndipo taifa la Israel lilipotabiriwa rasmi kuwepo. Na ahadi hiyo itakuja kutekelezwa na mjukuu wake yaani Yakobo ambaye aliiba urithi wa mtoto wa kwanza hivyo hii baraka ya Abraham akairithi yeye na tunaona uzao wake kupitia Joshua na Caleb ndio wanaingia kwenye nchi hii ya canaan rasmi na kuasisi taifa la Israel.
Je Mungu aliichagua Israel??
Kumb. La torati 7:6
6 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.
Kupitia mstari huu tunaona Israel ilichaguliwa na Mungu lakini je kwanini aliichagua??
Kumb. Torati 7:7-8
7 BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;
8 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu.
Hivyo Mungu aliwachagua Israel sababu hiyo ya kutimiza uapo kwa mababu ikiwemo Nuhu + Abraham. Na hili ndio lilisababisha Israel wapewe nchi ya Canaan sababu ilikuwa inahitimisha unabii wa Nuhu kuwa Canaan atakuwa mtumwa wa shem (Babu wa Abraham) na sio kwa sababu nyingine yeyote.
Mwanzo 9
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake
Ramani ya canaan
Hivyo baada ya Agano hili na Israel ambalo kupitia wao ndio Mungu alipanga kuwaletea Messiah yaani Yesu ili aweze kurejesha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu kama wa kipindi cha Adamu lakini wayahudi walimkataa Yesu kwa sababu hawakujua kutafsiri unabii ulioandikwa kuhusu maisha ya Yesu kwenye agano la kale. Kwa kifupi maisha yote ya Yesu kuanzia kuzaliwa mpaka kufa yalikuwa yanaendana na unabii wa agano la kale 1 korinto 15:1-4 Mfano wa nabii zilizotimizwa kupitia maisha ya Yesu ni hizi. Kuanza mahubiri yake galilaya ulitabiriwa na Isaya 9:1-2 na ukatimia Mathayo 4:13, Pia Yesu kupanda Punda kuingia jerusalem ulitabiriwa na Zakaria 9:9 na kutimia Mathayo 21:1-9 n.k yaani kuna mistari zaidi ya 100 iliyotabiriwa kuonyesha Huyo Messiah ataishije.
Lakini wao wayahudi hawakuliona hili sababu walidhani Yesu atakuwa handsome boy, Damu ya kifalme,Mwanajeshi kama alexander the great n.k hivyo kwa jinsi alivyokuja "kimasikini" wakaona kama anakufuru mwisho wa siku wakamuua na yote ni kutokana na kushindwa kutafsiri maandiko ya unabii.
Matendo 13:26-27
27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.