NdasheneMbandu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 940
- 308
Wakuu,
Jana nilipata taarifa kupitia vyombo kadhaa vya habari kwamba miongoni mwa viongozi waandamizi walioshinda kinyang'anyiro cha ujumbe wa NEC-CCM ni Mhe. Prof. Mark Mwandosya. Awali ya yote, nampongeza sana mheshimiwa huyu kwa ushindi murua. Pili, namshukuru Mungu kwa kumjalia afya afya njema maana kwa jinsi hali ilivyokuwa imemwelemea, haikuwa rahisi kutofikiria kwamba siku zake zilikuwa zinahesabika tu.
Ninachojiuliza sasa ni je, kwa masahibu yaliyompata, Mhe. Mwandosya na neema ya kuponywa aliyopata kwa Mwenyezi Mungu, anaweza kuwa bado anauwaza urais? Na kama ni ndiyo, je, bado ana nguvu ndani ya chama inayompa moyo kwamba anaweza akateuliwa kupeperusha bendera ya CCM?
MY TAKE:
Hisia zangu ni kwamba kambi yake ilisambaratika baada ya kuona kinara wa kundi anaumwa na wajumbe walijiunga na makundi mengine ya akina EL, SIX, BM, n.k.