Je, Inawezekana Prof. Mwandosya Bado Anauwaza Urais Pamoja na Masahibu Yote Hayo?

NdasheneMbandu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
940
308
Wakuu,

Jana nilipata taarifa kupitia vyombo kadhaa vya habari kwamba miongoni mwa viongozi waandamizi walioshinda kinyang'anyiro cha ujumbe wa NEC-CCM ni Mhe. Prof. Mark Mwandosya. Awali ya yote, nampongeza sana mheshimiwa huyu kwa ushindi murua. Pili, namshukuru Mungu kwa kumjalia afya afya njema maana kwa jinsi hali ilivyokuwa imemwelemea, haikuwa rahisi kutofikiria kwamba siku zake zilikuwa zinahesabika tu.

Ninachojiuliza sasa ni je, kwa masahibu yaliyompata, Mhe. Mwandosya na neema ya kuponywa aliyopata kwa Mwenyezi Mungu, anaweza kuwa bado anauwaza urais? Na kama ni ndiyo, je, bado ana nguvu ndani ya chama inayompa moyo kwamba anaweza akateuliwa kupeperusha bendera ya CCM?

MY TAKE:
Hisia zangu ni kwamba kambi yake ilisambaratika baada ya kuona kinara wa kundi anaumwa na wajumbe walijiunga na makundi mengine ya akina EL, SIX, BM, n.k.
 
Yanatuhusu nini sisi? Kayajadili Lumumba haya maupuuzi yenu. Huu ni muda wa M4C bhaaaaasss!!!
 
Huyu nguli inaonekana atakuja kuibuka kidedea, ili mradi afya yake irudi.
Hao wote waliokujibu kwa kejeli wanajua hao vilaza wenzao wanaotaka wachukue nchi hawawezi kusimama jukwaa moja na Prof.
 
Urais mtamu jamani. Si mnaona vasco da gama wetu anavyopaa majuu kila kukicha! Yote hiyo ni kwasababu ya urais. Sina uhakika na Mwandosya lakini wengine wanauwinda urais ili wapate urahisi wa kujenga mambo yao na familia zao na siyo wananchi wanaowachagua.

Nina uhakika akiamua kikwelikweli ku-contest Mwandosya anaweza kuwagaragaza wakubwa wengi tu ikiwa ni pamoja na mbuyu EL.
 
Wakuu,

Jana nilipata taarifa kupitia vyombo kadhaa vya habari kwamba miongoni mwa viongozi waandamizi walioshinda kinyang'anyiro cha ujumbe wa NEC-CCM ni Mhe. Prof. Mark Mwandosya. Awali ya yote, nampongeza sana mheshimiwa huyu kwa ushindi murua. Pili, namshukuru Mungu kwa kumjalia afya afya njema maana kwa jinsi hali ilivyokuwa imemwelemea, haikuwa rahisi kutofikiria kwamba siku zake zilikuwa zinahesabika tu.

Ninachojiuliza sasa ni je, kwa masahibu yaliyompata, Mhe. Mwandosya na neema ya kuponywa aliyopata kwa Mwenyezi Mungu, anaweza kuwa bado anauwaza urais? Na kama ni ndiyo, je, bado ana nguvu ndani ya chama inayompa moyo kwamba anaweza akateuliwa kupeperusha bendera ya CCM?

MY TAKE:
Hisia zangu ni kwamba kambi yake ilisambaratika baada ya kuona kinara wa kundi anaumwa na wajumbe walijiunga na makundi mengine ya akina EL, SIX, BM, n.k.

Habari za kaaminika ni kwamba Mwandosya anataka kupumzika siasa kuanzia 2015. Ila tatizo ambalo limezuka kufuatia fununu hizo ni kwamba wakazi wa Busokelo (jimboni kwake) wamefadhaishwa na fununu kuwa kuanzia 2015 Mwandosya anataka kumrithisha nafasi yake kijana fulani ambaye ABC za siasa hanazo hata chenmbe, yaani hajui kabisa kichwa cha siasa kinakaa upande gani mkia unakaa upande gani.

Yaani inakuwa kama kutakuwapo uwezekano jimbo hili la Busokelo likatoa mwanya wa kuchukuliwa na vyama vingine ambavyo siyo CCM.
 
Back
Top Bottom