Kwamba zilikuwepo silaha mpya na wapigaji waliopewa kuzijaribu kwenye miili ya watu? Je ulikuwa ufundi, umahiri ama mashindano ya kulenga shabaha?
Je ilikuwa ni kamari ya kubashiri nani ataketekeza roho nyingi kwa wakati mmoja? Ama je kulikuwa na silaha zinzokaribia kuisha muda wake wa matumizi hivyo inabidi zitumike haraka kabla ya muda wake kutimia ili zisilete hasara?
Maana roho nyingi zisizo na hatia ziliteketea nje ya maandamano .. Ilikuwa kama mchezo wa kuwinda.. Watu waliviziwa mitaani na majumbani, vichochoroni na hata kwenye veranda za majumba
Ilikuwa ni killing spree..
Karamu ya risasi.. Na kwakweli hazikubagua maana hakuna kundi ambalo halina kilio mpaka sasa.. Zile risasi hazikumuacha yeyote salama..
Wale wapigaji sijui walipewa nini huko.. Maana walichojua ni kulenga na kufyatua.. Na shabaha zao zilikuwa zimenyooka mno.. Majeruhi kidogo vifo vingi😭
Kuna damu bado hazijakauka
Vidonda vingi bado vinavuja damu vingine usaha.. Kuna majereha yameanza kutoa harufu..
Kuna miili imeanza kutoa uvundo mkali
Ardhi ya Tanganyika imenajisiwa.. Damu inanuka kila kona..!
View attachment 3498956