Je, ilikuwa ni karamu ya risasi?

Je, ilikuwa ni karamu ya risasi?

Kwamba zilikuwepo silaha mpya na wapigaji waliopewa kuzijaribu kwenye miili ya watu? Je ulikuwa ufundi, umahiri ama mashindano ya kulenga shabaha?

Je ilikuwa ni kamari ya kubashiri nani ataketekeza roho nyingi kwa wakati mmoja? Ama je kulikuwa na silaha zinzokaribia kuisha muda wake wa matumizi hivyo inabidi zitumike haraka kabla ya muda wake kutimia ili zisilete hasara?

Maana roho nyingi zisizo na hatia ziliteketea nje ya maandamano .. Ilikuwa kama mchezo wa kuwinda.. Watu waliviziwa mitaani na majumbani, vichochoroni na hata kwenye veranda za majumba
Ilikuwa ni killing spree..

Karamu ya risasi.. Na kwakweli hazikubagua maana hakuna kundi ambalo halina kilio mpaka sasa.. Zile risasi hazikumuacha yeyote salama..

Wale wapigaji sijui walipewa nini huko.. Maana walichojua ni kulenga na kufyatua.. Na shabaha zao zilikuwa zimenyooka mno.. Majeruhi kidogo vifo vingi😭

Kuna damu bado hazijakauka
Vidonda vingi bado vinavuja damu vingine usaha.. Kuna majereha yameanza kutoa harufu..

Kuna miili imeanza kutoa uvundo mkali
Ardhi ya Tanganyika imenajisiwa.. Damu inanuka kila kona..!View attachment 3498956
siku ya kwanza maandamano yakiwa mazuri , walipoanza tu kuchoma vitunna kuiba ? na kuuua polisi ndo nchezo ukabadilika, shaba shaba shaba
 
Kutoka kwenye ukurasa wa Sativa mtandao wa X;

Ushahidi mwingine wa POLISI na vyombo vya USALAMA wakiua watanzania.

Huyu ni kijana ambae alikamatwa 29 oktoba siku ya maandamano huko TUNDUMA MKOANI SONGWE. Hapo alishushwa kwenye Gari la Polisi baada ya kupigwa sana na kuambiwa AKIMBIE.

Alipokuwa akikimbia kama alivyoambiwa akapigiwa Risasi ya kwanza ikamkosa, ikapigwa Risasi ya pili ikampata akaanguka na kufariki punde.

Polisi wakachukua mwili wake na kuondoka nao, ndugu zake wametafuta mwili mochwari zote mkoa wa Songwe hawajafanikiwa.
 
siku ya kwanza maandamano yakiwa mazuri , walipoanza tu kuchoma vitunna kuiba ? na kuuua polisi ndo nchezo ukabadilika, shaba shaba shaba
Wafu wengi asilimia 98 ha wan yea wanandamanaji
 
Kutoka kwenye ukurasa wa Sativa mtandao wa X;

Ushahidi mwingine wa POLISI na vyombo vya USALAMA wakiua watanzania.

Huyu ni kijana ambae alikamatwa 29 oktoba siku ya maandamano huko TUNDUMA MKOANI SONGWE. Hapo alishushwa kwenye Gari la Polisi baada ya kupigwa sana na kuambiwa AKIMBIE.

Alipokuwa akikimbia kama alivyoambiwa akapigiwa Risasi ya kwanza ikamkosa, ikapigwa Risasi ya pili ikampata akaanguka na kufariki punde.

Polisi wakachukua mwili wake na kuondoka nao, ndugu zake wametafuta mwili mochwari zote mkoa wa Songwe hawajafanikiwa.View attachment 3508738
alikuwa msumbufu sana ngoja akasalimie mbinguni
 
Back
Top Bottom