Je, huwa unafikiria kuhusu mifumo ya usalama kwenye gari kabla ya kununua gari?

Tungoje Majibu!!
Hata Vitu Kama Simu Sasa Hivi Ni Kununua Huko Ulaya
Jibu lipo post namba #19.

Kwa upande wa simu inategemea ni simu gani Mfano Samsung first grade ambazo ndio zina processor ya SD zinauzwa China na US tu. Hata ukinunua ulaya ni kazi bure utapata Exynos version.
 
Umeuliza swali zuri na la akili. Asilimia 95 ya magari yetu ni used from Japan. Sasa tunaposema kuwa wanatengeneza gari ambazo si viwango kwa ajili ya soko la Afrika. Lakini unajiuliza haya magari mbona wanayatumia huko kwao ndo wanakuja yauza kwetu? Je nao hawajali safety katika magari yao isipokuwa tu yale yanayoenda uzwa kwa wazungu? Je wajapan hawaogopi kufa au nao hawajali? Hongera sana. Akikujibu ni Tag na mimi. Bila shaka atakuwa anaulizia ulizia kupata majibu.
Jibu lipo post namba 19.
 
Swali langu, hizi gari tunazomudu sisi kununua, Siyo mpya kabisa, tunanunua zikiwa zimetumika kiasi, je Nchi zinazotengeneza hizo gari nao wanatumia gari hizo, katika hali ambayo tunaletewa Afrika, ama baada ya kutembelea, wanapotaka kuziuza kwetu, hondoa baadhi ya vitu.
Naomba elimu hapa
Gari ambazo naweza sema labda wametengeneza kwa mazingira ya africa labda yutong, zhongtong ..na hizi boda boda toyo...

Lkn magari ni hayo hayo wanayotumia japan ndo tunanunua used kwa hio sio soko la africa nj kwa ajili ya soko lao
 
Kuna mambo mawili makubwa ambayo yanaamua upate madhara kiasi gani pindi unapopata ajali ya gari.

1. Speed
Hili ndio watu wengi wanalifahamu. Kikawaida unapoendesha gari, uwezekano wa kupata majeraha makubwa au kifo huongezeka mara dufu unapovuka 70Km/h. Sitajikita sana katika kueleza hili. Nitajikita zaidi kueleza jambo lifuatalo ambalo wengi hawalifamu.

2. Mifumo ya usalama ya gari lako

Magari yanakuwa na mifumo mingi ya usalama. Lakini mifumo yote ya usalama inagawanyika katika makundi mawili ambayo ni

(a) Active Safety Systems
Hii ni mifumo ya usalama ambayo inaweza kukupunguzia uwezekano wa kupata ajali. Yenyewe mara nyingi huwa inaact kabla ajali haijatokea. Mfano wa mifumo ya usalama ambayo ni Active ni ABS, Stability control, Cruise control, TPMS, n.k. Mfano ukiikuta gari iko equiped na cruise control maana yake gari hiyo inaweza kujipunguza speed endapo itakaribia kugonga kitu chochote ambacho kiko mbele yake bila wewe kukanyaga brake. Pia endapo utakata kona kali huku speed ikiwa juu basi tairi za nyuma zitafunga brake ili steering angle ifananane na speed unayotembea. Hii inasaidia sana kupunguza madhara yanayoweza kupatikana kwenye ajali.

Kwa gari za Japani hasa Toyota ambazo ndio hasa huku kwetu watu wengi wananunua zinakuwa na ABS tu au wakijitahidi wanaongeza na Stability control kwa ajili ya utelezi. Tofauti na gari ambazo zinauzwa Ulaya na Marekani ambapo wenzetu kigezo cha usalama kinazingatiwa mno kwa gari zinazoingia kwenye nchi zao.

(
b) Passive Safety systems
Mifumo ambayo ni passive yenyewe huwa inaact wakati tu ajali inapotokea. Mfano wa mifumo ambayo ni Passive kwenye gari ni Airbag, Seatbelt, Child safety systems n.k. Lengo langu lilikuwa kupagusa hapa kwenye Passive safety systems.

Asilimia kubwa ya gari hasa za Toyota ambazo tunauziwa huku Tanzania zinakuwa na Passive safety systems ambazo ni basic yaani Seatbelts pamoja na Airbag mbili ambazo moja hufungwa kwenye usukani na nyingine sehemu anayoiface abiria wa mbele. Hizi hulinda kichwa pamoja na kifua tu.

Gari kuwa na airbags mbili tu za mbele ambazo zinalinda kichwa na kifua tu haitoshi, Je vipi kuhusu ulinzi kwenye sehemu zingine za mwiili kama Miguu n.k.?

Je vipi kuhusu ajali ambazo zinatokea kwa gari kugongwa kutokea upande wa kutokea upande wa kushoto, kulia au nyuma? Je abiria waliokaa seat za nyuma wanasalimika vipi?

Kwa mfano gari nyingi za toyota zinazouzwa ulaya na marekani zinakuwa na Airbag 7 mpaka 9 tofauti na hizi toyota tunazonunua huku Tz ambazo nyingi zinakuwa na Airbag mbili. Hizo airbag zingine zimeongezwa maeneo kama milangoni, kwenye collars, unapoweka miguu n.k. ili kuwalinda walioko ndani na ajali za kutokea upande wowote. Mfano katika speed 50Km/h gari yenye airbag mbili na yenye airbag 9 zikipata ajali katika mazingira yanayofanana, madhara kwa walioko ndani hayatofanana. Gari yenye airbag 9 itakuwa unafuu.

Kwa kifupi Africa tunauziwa magari kulingana na kile kidogo tulichonacho mkononi ndio maana gari nyingi tunazouziwa zinakuwa vifaa vya usalama ambavyo ni basic tu pia hata vitu vingine kama Bodi vinakuwa ni vyepesi. Kuna msururu wa gari nyingi ambazo zinauzwa huku kwetu lakini baadhi ya nchi za ulaya hawaruhusu kabisa gari hizo kukanyaga kwenye nchi zao.

Ndio maana watu wengi wanaziogopa sana gari za Ulaya, zinauzwa gharama lakini wenzetu wamezingatia sana suala la usalama gari inapotembea barabarani, building quality n.k. Pia kitu kingine kinachofanya gari za ulaya ziuzwe gharama ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa vipuri feki. Tofauti na gari za Japani ambazo vipuri feki ni vingi. Hata hizi gari za Japani kununua vipuri original siyo bei rahisi.

MWISHOWewe
Wewe ni marketing manager wa vw, audi, mbenz, ford, vauxhall, gm, etc. Tuacheni sisi wa gari toyota
 
Umewahi kuisikia Toyota Avensis kuanzia T25?

Hiyo gari ina 9 airbags na watu wanazo humu mjin. Sisi sijui niendelee kutaja zingine au niache?

Utofauti no kwamba mifumo ya usalama ni kama mandatory kwa mzungu wakati kwa wajapani ni option.

Kanunue gari za Japan ambazo zinauzwa European Market. You will feel the difference.
 
Nilinunua carina E , Belgium mwaka wa 2000 sikuona tofauti na carina my road ya japan ya 2003
 
Kuna mambo mawili makubwa ambayo yanaamua upate madhara kiasi gani pindi unapopata ajali ya gari.

1. Speed
Hili ndio watu wengi wanalifahamu. Kikawaida unapoendesha gari, uwezekano wa kupata majeraha makubwa au kifo huongezeka mara dufu unapovuka 70Km/h. Sitajikita sana katika kueleza hili. Nitajikita zaidi kueleza jambo lifuatalo ambalo wengi hawalifamu.

2. Mifumo ya usalama ya gari lako

Magari yanakuwa na mifumo mingi ya usalama. Lakini mifumo yote ya usalama inagawanyika katika makundi mawili ambayo ni

(a) Active Safety Systems
Hii ni mifumo ya usalama ambayo inaweza kukupunguzia uwezekano wa kupata ajali. Yenyewe mara nyingi huwa inaact kabla ajali haijatokea. Mfano wa mifumo ya usalama ambayo ni Active ni ABS, Stability control, Cruise control, TPMS, n.k. Mfano ukiikuta gari iko equiped na cruise control maana yake gari hiyo inaweza kujipunguza speed endapo itakaribia kugonga kitu chochote ambacho kiko mbele yake bila wewe kukanyaga brake. Pia endapo utakata kona kali huku speed ikiwa juu basi tairi za nyuma zitafunga brake ili steering angle ifananane na speed unayotembea. Hii inasaidia sana kupunguza madhara yanayoweza kupatikana kwenye ajali.

Kwa gari za Japani hasa Toyota ambazo ndio hasa huku kwetu watu wengi wananunua zinakuwa na ABS tu au wakijitahidi wanaongeza na Stability control kwa ajili ya utelezi. Tofauti na gari ambazo zinauzwa Ulaya na Marekani ambapo wenzetu kigezo cha usalama kinazingatiwa mno kwa gari zinazoingia kwenye nchi zao.

(
b) Passive Safety systems
Mifumo ambayo ni passive yenyewe huwa inaact wakati tu ajali inapotokea. Mfano wa mifumo ambayo ni Passive kwenye gari ni Airbag, Seatbelt, Child safety systems n.k. Lengo langu lilikuwa kupagusa hapa kwenye Passive safety systems.

Asilimia kubwa ya gari hasa za Toyota ambazo tunauziwa huku Tanzania zinakuwa na Passive safety systems ambazo ni basic yaani Seatbelts pamoja na Airbag mbili ambazo moja hufungwa kwenye usukani na nyingine sehemu anayoiface abiria wa mbele. Hizi hulinda kichwa pamoja na kifua tu.

Gari kuwa na airbags mbili tu za mbele ambazo zinalinda kichwa na kifua tu haitoshi, Je vipi kuhusu ulinzi kwenye sehemu zingine za mwiili kama Miguu n.k.?

Je vipi kuhusu ajali ambazo zinatokea kwa gari kugongwa kutokea upande wa kutokea upande wa kushoto, kulia au nyuma? Je abiria waliokaa seat za nyuma wanasalimika vipi?

Kwa mfano gari nyingi za toyota zinazouzwa ulaya na marekani zinakuwa na Airbag 7 mpaka 9 tofauti na hizi toyota tunazonunua huku Tz ambazo nyingi zinakuwa na Airbag mbili. Hizo airbag zingine zimeongezwa maeneo kama milangoni, kwenye collars, unapoweka miguu n.k. ili kuwalinda walioko ndani na ajali za kutokea upande wowote. Mfano katika speed 50Km/h gari yenye airbag mbili na yenye airbag 9 zikipata ajali katika mazingira yanayofanana, madhara kwa walioko ndani hayatofanana. Gari yenye airbag 9 itakuwa unafuu.

Kwa kifupi Africa tunauziwa magari kulingana na kile kidogo tulichonacho mkononi ndio maana gari nyingi tunazouziwa zinakuwa vifaa vya usalama ambavyo ni basic tu pia hata vitu vingine kama Bodi vinakuwa ni vyepesi. Kuna msururu wa gari nyingi ambazo zinauzwa huku kwetu lakini baadhi ya nchi za ulaya hawaruhusu kabisa gari hizo kukanyaga kwenye nchi zao.

Ndio maana watu wengi wanaziogopa sana gari za Ulaya, zinauzwa gharama lakini wenzetu wamezingatia sana suala la usalama gari inapotembea barabarani, building quality n.k. Pia kitu kingine kinachofanya gari za ulaya ziuzwe gharama ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa vipuri feki. Tofauti na gari za Japani ambazo vipuri feki ni vingi. Hata hizi gari za Japani kununua vipuri original siyo bei rahisi.

MWISHO
Ziuzwe gharama wapi? Huko mitandaoni zipo kibao tu bei rahisi!

Gari ya ulaya gharama iko kwenye kulihudumia na watu kwa kutambua hilo hawayataki sababu magonjwa yake huwa ni ya kufululiza. Hasa hasa range rovers ni upuuzi. Bora hata mjerumani walau ila still zinataka preventive maintanance.

Mjapani kimsingi spea sio bei rahisi kama utanunua Original Parts. Kama utaweka za kubumba ndio huwa kitonga ila hazidumu na upatikanaji wa spea ni mrahisi kwa hapa nchini maduka ni mengi hata mikoani! Kingine kizuri zinaingiliana hata kwa wauzaji kwao ni nafuu sababu parts ziko interchangable across cars.

Mzungu kila edition na spare zake haziingiliani japo kwa macho unaweza ona ni gari hio hio! A4 ya mwaka 2004 na 2008 unakuta hazifungiani parts.

Au ya 1.8T na ile ya 2.0T parts haziingiliani 😅😅😅 uchawi unaanzia hapo.

Ila mjapan gari iwe ya 2003 mpaka 2005 parts zile zile tofauti engines tu.
 
Mjerumani sema ana hatua kadhaa mbele dhidi ya Mjapan. Ingawa crown ipo vizuri ila ukija tu pamabanisha na gari ambayi the same class the same mwaka na mjerumani ni 🔥🔥
Mjerumani ana over engineer ila hana precision😅 kama Toyota hapo ndipo tatizo linapoanzia!

Gizmos ni nyingi ila hazina uimara kama ambavyo anafanya Toyota.
 
Ziuzwe gharama wapi? Huko mitandaoni zipo kibao tu bei rahisi!

Gari ya ulaya gharama iko kwenye kulihudumia na watu kwa kutambua hilo hawayataki sababu magonjwa yake huwa ni ya kufululiza. Hasa hasa range rovers ni upuuzi. Bora hata mjerumani walau ila still zinataka preventive maintanance.

Mjapani kimsingi spea sio bei rahisi kama utanunua Original Parts. Kama utaweka za kubumba ndio huwa kitonga ila hazidumu na upatikanaji wa spea ni mrahisi kwa hapa nchini maduka ni mengi hata mikoani! Kingine kizuri zinaingiliana hata kwa wauzaji kwao ni nafuu sababu parts ziko interchangable across cars.

Mzungu kila edition na spare zake haziingiliani japo kwa macho unaweza ona ni gari hio hio! A4 ya mwaka 2004 na 2008 unakuta hazifungiani parts.

Au ya 1.8T na ile ya 2.0T parts haziingiliani uchawi unaanzia hapo.

Ila mjapan gari iwe ya 2003 mpaka 2005 parts zile zile tofauti engines tu.
Umemaliza mkuu

Sent from my Infinix X693 using JamiiForums mobile app
 
Mjerumani ana over engineer ila hana precision😅 kama Toyota hapo ndipo tatizo linapoanzia!

Gizmos ni nyingi ila hazina uimara kama ambavyo anafanya Toyota.
ukija ku balanace kati ya 10 hicho unachosema.. kati ya German na Japan machines, mtajikuta mnajivunia uimara.. ila cha kujua system kadri inavyokuwa complicate inakuwa vulnerable kuliko isiyo complicated.. sasa hivi Japana cars nazo zinakuwa na complications nyingi za kimifumo mtapata matokeo tu
 
Back
Top Bottom