Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,852
Unakuta mtu ana wafanyakazi wa ndani yani (House girls) wawili na watoto wake. Anatoka nao kwenda kwenye mgahawa kupata chakula na kinywaji kidogo!
Kwanza anapofika ktk mgahawa haongozani na hao wafanyakazi wake! Anatangulia yeye na mke wake na watoto wake wa kuzaa then hao wafanya kz wanakuja wanachungulia chungulia kwa woga na kukaa pembeni umbali wa hatua 30 kutoka meza ya mabwana zao! Na hawaruhusiwi kuagiza chochote mpaka agizo litoke kwa Bwana.
Na wanakaa wametulia na kujalibu kuwatuliza watoto wa Boss wao ambao wanaonekana ni watundu na wanaokimbiakimbia hovyo ktk mgahawa!
Then baada ya hapo Bwana na bibi wanaagiza chakula na kinywaji na kula wao tu peke yao huku wale wafanyakazi wamekaa pembeni tena ktk viti vya wageni ktk mgahawa huku hawatumii chochote!
Je huu ni uungwana kweli kwa mtu anaekutunzia na kukuangalizia watoto wako wakati wewe ukiwa ktk mapilika ya maisha yako? Na hii mpaka nje km kwenye migahawa mtu anaweza kuwafanyia hivi wafanyakazi wake wazi wazi, je huko ktk familia yake majumbani si ndio balaa kabisa?!!
Maana huko inaonekana ni marufuku mfanyakazi kula chakula km anachokula bwana! Bwana km anakula chips kuku, mfanyakazi anakula ugali Dagaa au maharagwe. Boss km anakunywa maji ya kwenye Fridge yaliyopowa basi mfanyakazi anakunywa ya kwenye ndoo! Na huenda ni marufuku kukaa sebuleni kuangalia Tv au kuwasha tv na redio!
Nauliza jee huu ni UUNGWANA KWELI?