ndandambuli
JF-Expert Member
- Jul 2, 2017
- 973
- 665
Ulikuwa na mume/mke, akakuacha bila bila sababu yoyote ya msingi, baada ya miaka kadhaa kupita anakutafuta anakuomba mrudiane, kwakuwa ulikuwa unampenda sana unamkubalia mnaenda ANGAZA kucheki salio, huko angaza mnakutana na majibu mawili tofauti, majibu yako ni HIV-ya mwenzako HIV +.
Haya majibu yanaleta tafrani, unamuuliza mwenzako kumbe umekuja kuniua? Uliniacha ukiwa na afya njema miaka kibao imepita leo unataka turudiane kwasababu una maambukizi? Anaanza kujitetea hatimaye unakubali na unampa masharti, ni mwendo wa mpira maisha yetu yote.
Anakushukuru sana kwa kukubaliwa na anakuahidi atakuwa mwaminifu kwako maisha yake yote hataweza kukusaliti, anakula kiapo cha uaminifu anakwambia endapo itatokea amekusaliti Mungu ampe adhabu ya kifo bila kuchelewa, miaka mitatu baadae unamfumania live yuko na mpenzi wake wa zamani, kama kawaida yake anaendelea kuomba msamaha usimwache muendelee kuishi pamoja, je ukimsamehe mtu kama huyo itakuwa ni kwasababu ya mapenzi uliyonayo kwake ujinga ubwege au kitu gani?