Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,229
- 44,239
Skull canyon around dola 600 ambayo ni kama 1.5m ya kwetu,
Na kama unataka bei rahisi zaidi unanunua barebone pc na ryzen Apu. Barebone around $150 na Apu pia Around $150 ryzen 5 3400G. So inakuwa $300 + ram na HDD, hii itaangukia around laki 8 mpaka 9 hivi huko ughaibuni.
Hio ni cpu yenye core 4 na thread 8 inatosha kwa game lolote lile hasa ports za console.
Hapa kwetu mkuu ngumu kupata sababu sisi ni wazee wa used hasa kwenye desktop.
Ila intel CPU zake za Gen ya 5 zilikuwa na Gpu kali sana, hapa kwenye mitumba ukiibahatisha moja pia sio mbaya kuichukua, iris pro 6200 gpu ya ndani ya hio processor inahandle almost game zote kwa 720p.
Pia intel alidesign gen ya 5 kuingiliana na gen ya 4, mfano hicho kimini desktop cha gen ya 4 chenye i3 4130 theoretically ukiweka i5 ama i7 ya gen ya 5 inatakiwa ikubali, japo oems kama Dell ama Hp wanaweza kudisable kwa baadhi ya desktop, hivyo unaweza fanya utafiti wa model husika kama inakubali unanunua tu processor na ku upgrade desktop hio hio ndogo.