Je, hili gonjwa lililompata mshikaji wetu ni karma au uchawi?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wana JF wenzangu,

Ama baada ya salam naomba nijielekeze kwenye mada husika. Kuna rafiki yang mmoja anaitwa J (nimekatiza jina lake kwa sababu ya heshima na usalama wake). Sasa huyo J na yeye anamshikaji wake ambae walipanga nae nyumba 1 mitaa fulani (jina kapuni) J aliowa mwaka uliyopita, akamleta mkewe hapa jozi ili waishi nae pamoja.

Kabla hata miezi 6 ya ndoa haijaisha, J akaanza kulalamika kuwa mkewe anaonekana hana uaminifu na ndoa yao. Kuja kuchunguza tukagundua kama kuna ukweli fulani, ikabidi mimi na yule rafiki yake na J tuwe kama wasuluhishi wa ugomvi wao mara kwa mara. J akaona hali inazidi kuwa mbaya ikabidi ampe talaka mkewe kwa kushauriwa na yule rafiki yake mungine, na kumrudisha nyumbani.

Kama walivyosema waswahili kuwa "kikulacho kipo nguoni mwako" baada ya miezi miwili ya talaka, yule rafiki yake na J akamchumbia yule aliekuwa mke wa J kimya kimya, na kufunga nae ndoa tena kimya kimya. Waswahili walishasema kuwa "la kuvunda halina ubani".

Baada ya ndoa kabla jamaa hajamfikisha hapa huyo mkewe ambae alikuwa shemeji yake, taarifa zikaanza kusambaa na kutufikia mimi na J mwenyewe. J alipomuuliza jamaa, akakataa akisema eti huo ni uzushi tu na kwamba kamwe hawezi kufanya uchafu kama huo katika maisha yake.

Ghafla jamaa akahama nyumba mpaka mtaa, yani akahamia mbali na mahali ambapo itakuwa ngumu kuonekana. Baada ya kuhama, mara mkewe akafika, kuchunguza ikaonekana kweli jamaa kamuowa shemeji yake aliekuwa mke wa J.

Jamaa siku ya kwanza katwanga kinu cha mkewe kwa masham sham na furaha tele kama kawaida, siku ya pili pia mchana na usiku inasemekana katwanga fresh, ya tatu mtwangio wa jamaa ukagoma, yani ukalegea ukawa hausimami hata ukiubust na jeki.

Jamaa amejitahidi kwa kadri awezavyo kurudisha uhai wa mtwangio wake imeshindikana. Sasa jamaa ameanza kulalamika kwa watu, kuwa eti aliekuwa rafiki yake kipenzi ndugu J amemroga ili kumkomoa, na kwamba atafanya kila awezalo kuujua ukweli na kulipiza kisasi kwa yeyote aliemsabishia yeye fedheha mbele ya mkewe.

Ila wenye kujua kinachoendelea tunahisi hii inaweza kuwa ni karma ya kujaribu kupindua meza ya mwenzake (J) na kwamba karma hiyo itamtafuna hadi aende kumuangukia muhusika, na kuomba msamaha.

Sasa wana JF wenzangu, nyinyi hili swala mnalionaje? Ni karma hii, au kuna uchawi umetumika hapo? Sababu J mwenyewe nikimuuliza, anasema binafsi hafahamu hata huo uchawi huwa unaptikana vipi na unatumikaje.

So wengi hatuelewi zaidi nini kinaendelea mpaka jamaa kuwa vile. Karibuni ndugu kwa michango yenu.

Ushauri: Wabongo wenzangu wa kiume tuachane tamaa, Mungu kaumba wanawake wengi kwa ajili yetu, kwahiyo tujiepushe kuchukuliana wanawake au wake wenyewe kwa wenyewe.
 
sio uyo jamaa ni wewe, hakuna ubaya kujiweka tu hadharani, wote hapa hatukujui na hautujui.

Wewe ulikuaje kama siku ya tatu alishindwa? jibu rahisi sana uyo jamaa ni wewe.


Pole mkuu, nenda kanisani.
Kweli kabisa, unawezaje kujua usiku na mchana hadi jogoo alivyolala.
Huyo ni rafiki yake j pole yake na iendelee kulala liwe fundisho kwa wengine.
 
Sio uyo jamaa ni wewe, hakuna ubaya kujiweka tu hadharani, wote hapa hatukujui na hautujui.

Wewe ulikuaje kama siku ya tatu alishindwa kumtomba mkewe? jibu rahisi sana uyo jamaa ni wewe.

Pole mkuu, nenda kanisani.
Hahahaha 😂😂😂 mkuu mimi nina mke na watoto wawili tayari. Siwezi kuvizia mke wa mwanaume mwenzang, kuja kumfanya kuwa mke wangu. Ila shukran kwa mchango wako mkuu.
 
Kweli kabisa, unawezaje kujua kwamba jamaa Kato.. mb usiku na mchana hadi jogoo alivyolala.
Huyo ni rafiki yake j pole yake na iendelee kulala liwe fundisho kwa wengine.
Si unaona nimesema kwamba jamaa ashaanza kulalamika kuwa karogwa na J. Kwahiyo yeye mwenyewe muhusika ndo anawambia watu na habari zinamfikia mlengwa J ambae ni rafiki yangu.
 
Back
Top Bottom