SI KWELI Je, hiki kirusi kweli kama media zinavoripoti?

SI KWELI Je, hiki kirusi kweli kama media zinavoripoti?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
JE NI KWELI HIKI NI KIRUSI CHA UKIMWI? KAMA BAADHI MEDIA ZINAPOST INSTAGRAM ZIKISEMA HIKI NI KIRUSI CHA UKIMWI KIKIWA KIMEKUZWA KWENYE ELECTRONIC MICROSCOPE BY ANOLD MEDIA
Kiwavi Aug 025.jpg

1755231753623.png
 
Tunachokijua
Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo huyu na huyu kwa nyakati tofauti walichapisha picha ya kiumbe kimoja na kudai kuwa huo ndiyo muonekano wa kirusi cha UKIMWI.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Kinachoonekana pichani kiwavi (Caterpillar) na siyo kirusi cha UKIMWI, kiwavi hakina uhusiano wowote na virusi vya ukimwi tofauti na ilivyoelezwa na Taarifa potoshi.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Wildlife Trust inatafsiri kiwavi (caterpillar) kuwa ni hatua ya mabuu ya nondo au kipepeo. Ni hatua ya pili katika mzunguko wa maisha yao wa hatua nne: yai, kiwavi, pupa, na kipepeo/nondo mzima.

Ufuatiliaji kwa njia ya google image reverse search, JamiiCheck imebaini kuwa picha iliyotumika katika taarifa potoshi imewahi kuchapishwa mtandaoni na ukurasa wa Ever greening alliance Juali 12, 2024 na kumtaja kuwa kiumbe huyo ni moja ya aina ya viwavi.

Aidha mtumiaji mmoja wa mtandao wa instagram Machi 18, 2025 alichapisha picha 15 kuonesha baadhi ya viwavi pekee na virembo/wazuri duniani ambapo pamoja na viwavi vingine ipo pia picha ya kiwavi ambacho taarifa potoshi inadai kuwa ni kirusi cha UKIMWI. Tazama picha ya 11

Utafutaji zaidi umebaini kuwa kiwavi huyo hujulikana kwa jina la Hickory Horned Devil.
Back
Top Bottom