Kwa kweli kumzuia mke kufanya kazi eti atatongozwa au atacheat ni ushamba, ujinga, utovu wa nidhamu, ubinafsi na ni hasara kwa familia! Hasara katika maana gani? Mke ana akili, nguvu ana muda. Hivi vitu vitatu ni rasilimali(resources) za familia ambazo hazitumiki kuzalisha zinakaa tu. Lakini wakati huo huo mke anahitaji kula, kuvaa, kupewa huduma ya afya,kujipamba,kustarehe,nk. Hivi vyote vinahitaji hela, lakini rasilimali za mtu mmoja ndizo zinazotafuta mahitaji yote ya familia! Ebu tufikirie swali moja ni ofisi gani inayoweza kuajiri mfanyakazi ambaye hafanyi kazi lakini analipwa mshahara kila mwezi? Ofisi yoyote ambayo boss yuko makini na hataki hasara haiwezi kumlipa mfanyakazi asiye na kazi. Lakini familia nyingi ziko hivyo kutokana na wake kuzuiwa kufanya kazi kwa kisingizio hafifu kuwa watatoka nje ya ndoa. Lakini fuatilia nyendo za waume wa namna hiyo. Nyumba ndogo, mahawara, kwa kwenda mbele! Ndoa yoyote ili idumu katika furaha inahitaji kuaminiana. Kuaminiana kunahusisha mme kumruhusu mke achangie kipato cha familia ama kwa kufanya kazi au bishara. Kuna faida nyingine ya kudumu. Kuna usemi kuwa ni bora mtu akakufundisha kuvua samaki kuliko mtu kukuletea samaji aliovua ili ule tu. Huyo mtu akitoweka/kuhama nk ndio mwisho wa wewe kula samaki. Akikufundisha kuvua hutamtegemea yeye ili ule samaki, awepo asiwepo. Tumeona wake wa nyumbani ambao waume zao waliwazuia kufanya kazi yoyote. Akifamume anaweza akamwachia mke fedha na mali nyingi lakini kwa kuwa hana uzoefu wa kuzungusha hela atafuja zote zitaisha. Mwisho wa yote kuwa omba omba. Kwa hiyo waume ruhusuni wake zenu watumie rasilimali walizo nazo kuchangia kipato cha familia napia wajizoeze kchakarika kwa manufaa ya baadaye.