Je hii inamaanisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hii inamaanisha nini?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kimbori, Sep 18, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikiapata ujumbe huu mara kadhaa huku nikiwa sijui maana yake.
  "Bandwidth Limit Exceeded The server is temporarily unable to
  service your request due to the site
  owner reaching his/her bandwidth limit.
  Please try again later.".
  Naomba kujua maana yake?
   
 2. N

  Nyasiro Verified User

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 1,286
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba kila website huwa ina kitu kinaitwa Bandwidth ambayo inakuwa measured in MBs or GBs. Kama website yako inatumika sana inamanisha kwamba inatumia nafasi kubwa kusafirisha vitu kwenye mtandao. Mfano. Website kama Facebook au JamiiForums inatumia bandwidth kubwa kuliko website kama NECTA. Unapofanya hosting ya website unalipia na bandwidth kulingana na mahitaji yako. Kama matumizi ya website yako yatazidi bandwidth uliyopewa na ISP wako hiyo website haitapatikana manake imeleta Jam kwenye mtandao mpaka mwenye website alipie kiwango ambacho kimezidi. Ni kama barabarani kadri gari zinavyokua nyingi na foleni inaongezeka na website inapokuwa na watumiaji wengi na bandwidth inaongezeka na inabidi ilipiwe ili huduma iendelee. Ni hayo tu. Wataalam wengine watakuja....
   
 3. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Ahsante kwa maelezo. Je hiyo Website itakuwa imefungwa mpaka mwenye nayo alipie kiasi cha matumizi kilichozidi?
  Au traffic jam ikipungua website itarudi kwenye hali yake ya kawaida?
  Kama "NDIYO", traffic jam itapunguaje ikiwa mtu anaambiwa Bandwith limit kila anapotaka kuifungua?
   
 4. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,760
  Likes Received: 7,045
  Trophy Points: 280
  Hosting zinapimwa kwa mwezi ina maana itafungwa mpaka mwezi mwengine ndo ataanza upya.

  Ngoja nkupe mfano mdogo.

  Mi nimefungua website ina page 1 hio page ukubwa wake ni kb500 na hosting wangu kanipa bandwitch gb 1 kwa mwezi ina maana akija mtu mmoja kufungua ile page ndani ya mwezi ntakua nimetumia bandwitch kb 500 so wakija watu 2000 ndani ya mwezi itakua exactly nimetumia gb 1 kuanzia mtu wa 2001 kuja ataambiwa bandwitch imefika limit. Mpaka mwezi ujao anaanza upya

  Hapo itabidi webmaster afanye upgrade ya hosting plan ili apewe bandwitch kubwa zaidi na kuweza kusatisfy visitors wake.

  Bandwitch maana yake ni rate ya kutransfer data
   
 5. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,566
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  somo zuri hili sikua nafahamu
   
 6. N

  Nyasiro Verified User

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 1,286
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hili tatizo limeikumba HESLB tangu juzi.

  Bandwidth Limit Exceeded

  The server is temporarily unable to service your request due to the site owner reaching his/her bandwidth limit. Please try again later.
   
 7. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,760
  Likes Received: 7,045
  Trophy Points: 280
  Dah sisi wabongo wezi sana huyu webmaster anatikwa awe responsible ni aibu website kama hii inatakiwa iwe unlimited bandwitch kwa miez kama hii kila mtu anataka habari ya mkopo lazima bandwitch iende sana
   
 8. N

  Nyasiro Verified User

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 1,286
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wanafanya ujanjaujanja hadi kwenye mambo ya msingi. Kama wanashindwa kulipia bandwidth nna mashaka kama huo mkopo wangu watanipa tena kwa wakati.
   
Loading...