Je, haya maisha yanaweza kuwa chanzo cha kuvuruga akili yangu?

Passed

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
561
156
Nilimlazimisha mzazi kwenda shuleni ada anatoa vizuri ila ya matumizi changamoto. Naweza nikala siku moja kwa siku siku utakuta sina mkaa napikia makaratasi mpaka chai ichemke ninywe au kuchana godoro langu ninalolalia vipisi vidogo vidogo kugeuza mkaa kama raha ya chakula napata mara chache.

Kwa wiki ananitumia 20 napo anaweza akapitisha siku sasa badaye nafsi ikawa imeanza kuangaika niache chuo siku zote za maisha yangu ya shule nikaombewa nimepita kwa waganga naambiwa nimetupiwa jini maisha yangu ya shule yalikuwa ya upweke ya kulala tu siku nzima na kuwaza chakula na nyumba nilokuwa nakaa ilikuwa na kichaa ambaye anaongea siku nzima wakati mimi nipo ndani kila siku.

Nikiwa nimejifungia mlango wangu baada ya kurudi chuo badae nikawa kama nimechanganikiwa naweza shika daftari nikaishia kufungua page tu bila kusoma naingia ndani natoka nje bila sababu natoa daftari kwenye mkoba naingiza tena bila sababu nafsi ya kuacha chuo imechachamaa je hii hali imesababishwa na maisha ya shule au ndo kama waganga wanavyonambia nimetupiwa jini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stress za maisha zinakuchanganya,Umeanza kukata tamaa,
Relax,jichanganye na watu,acha kukaa peke yako na kuwaza sana,maisha yana ups and down.
 
Back
Top Bottom