Kujichora tattoo imekuwa chanzo cha kuachwa dada yangu, ni kama ana bahati mbaya

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,823
Naomba uandike hiki kitu kaka kwani mimi kinaniumiza sana, nina miaka 35 sijaolewa nahisi kila mwanaume ananiona Malaya.

Iko hivi, kipindi cha ujana nikiwa chuo kuna mwanaume nilikua naye, kama unavyojua ujana tukachorana tattoo, kiunoni na nyingine kwenye paja juu kabisa.

Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaiangaia mtaani tukaachana, hivyo katika kuifuta ile tattoo nikalazimika kuchora ua kiunoni hivyo ikawa kubwa na hii ya kwenye paja nilichora picha fulani ya ndege hivyo ikawa imepanda juu kabisa karibu na sehemu za siri.

Kaka hiko kitu kimekuwa kikinitesa sana, kila nikiingia kwenye mahusiano nikishakutana na mwanaume kimwili tu unamuona anabadilika. Napata wanaume kweli lakini wanaona kama vile mimi ni Malaya, yaani siwaelewi kabisa.

Kuna wakati niliamua kutokutana kimwili kabisa na mwanaume mpaka ndoa. Kweli kuna kijana mmoja yeye ni mlokole alinikubalia na kila kitu kilikaa vizuri tulikaa mwaka bila kukutana kimwili. Akaja kwetu na kunipeleka kwao.

Ila kuna siku sijui ilikuaje akaona picha yangu moja ya zamani ambayo nilipost Facebook. Kaka ni ya zamani sana kiasi kwamba hata siijui kwani hata Facebook situmii na hiyo akaunti sina hata password yake. Tulikua tunaogelea na marafiki zangu sasa nilivaa nguo za kuogelea hivyo zile Tattoo zikaonekana.

Akaniuliza, "Huyu ni nani?" Nililazimika kumuambia ukweli kwani nilijua nishaharibu. Tangu hapo alibadilika na kusimamisha kila kitu.

Najua ni makosa Kaka niliyofanya na sina namna ya kurekebisha. Lakini naomba uandike kuwa si kila mwanaume anajichora tattoo ni Malaya. Nimechoka Kaka kuachwa kwa vitu vidogo. Waambie wanaume waache ushamba.

Vipi Mdau Una Maoni Gani Kuhusu Jambo Hili....!?
1702387089474.jpg
 
Kinachowakimbiza sio tattoo, Bali wanawaza uliwezaje kujiachia Kwa mchoraji akuchore, tena wachora tattoo wengi ni wanaume....mwanaume mwenye akili timamu hawezi kuoa mwanamke anayeweza kumuachia mwanaume mwingine kiuno achore, huku katulia tuli, anaambiwa geuka anageuka, tulia anatulia....
Atafute mwanaume mwenye tattoo waoane.
 
Kinachowakimbiza sio tattoo, Bali wanawaza uliwezaje kujiachia Kwa mchoraji akuchore, tena wachora tattoo wengi ni wanaume....mwanaume mwenye akili timamu hawezi kuoa mwanamke anayeweza kumuachia mwanaume mwingine kiuno achore, huku katulia tuli, anaambiwa geuka anageuka, tulia anatulia....
Atafute mwanaume mwenye tattoo waoane.
Hasa hapo wakati wa kuichora hiyo tattoo ndipo kuna maswali mengi.
 
Pole sana ila sio lazima uolewa na mwanaume mwenye Pesa unawaza tafuta hata Mwendesha boda bodo akawa baba wa watoto wako na akakustili pia Age ishakutupa mkono na hiyo kasolo kwa sisi waowaji ndio kabsa huwezi tupata
 
Kwa maisha yetu haya inahitaji moyo kweli kuwa na mwanamke mwenye tattoo, unakuta tattoo ya kalio daaah au kiuno daaah nguvu zote zinakuishia unaanza kufikiria mambo mengi sana Bora ule nyama ya mbwa ukiwa huijui ila siyo kabla ya kuila ushaijua.
 
Nilikuwa na ex wangu, nilimpenda sana. Yeye alikuwa na tatoo sema kwa mgongo nilimkuta nayo. Shida yeye alikuwa influenced na movie na utoto. Nilikaa nae and tabia zake hazikuwa hivyo watu wengi wenye tatoo wanavyohisiwa. Kuna kipindi tuliachana alienda ongeza zingine. Aisee nikamwambia utapata sana shida in future to convince wanaume kama uko sawa. Ni vigumu kwa mwanaume mwenye akili timamu kuoa mwanamke mwenye matatoo mwilini.
 
Back
Top Bottom