Je hapo ulipo mitambo ya analogi imezimwa?

Je hapo ulipo mitambo ya analogi imezimwa?

Sisi watu wa Mbeya bado haijazimwa. Ila kwa wale wanao tumia dish wamesema wataendelea kuangalia kama kawaida wasitupe dish zao.

Chanzo: Startv
 
Mnaandika nyie mnajijibu nyie, Kuna mtu Tz anaweza kusema jamaa wamefanya kweli aiseee tumezoea longo longo hawa hawana? Mangapi mnafanya vizuri mpaka muonekane hamna longo longo? Wenye akili tunajua mna ten percent yenu na watu wa ving'amuzi na sio jingine. Mngekuwa hamna longo longo ving'amuzi si mngehakikisha vipo kila mahali na katika bei ambayo ni affordable kwa wananchi wa vijijini? Hivyo mmefanya kweli mission accomplished ten percent guaranteed.

Kuna harufu ya ukweli hapa, ona issue ya POWER TILLER walivyopigia kelele lakini sasa hivi kiko wapi wakati kilimo ni kila siku mbona nguvu ile ya mwanzo imekwisha na mbaya zaidi mtu wao walivyompa tenda ya kwanza kuleta haya mavitu mbona haleti sasa. (wamehadaa wananchi na wamewafanya wameingia cost ya ziada ya fuel wakati walishajizoelea maksai wao ambao gharama anayotumia ni majani na maji tu ambayo yanapatika)

Ipo siku utasikia wanatoa ving'amuzi bure wewe subiri tu wakishiba
 
Simu yangu ya kichina mbona bado inafanya kazi ni aina y digital au sisi wa vijijini wamesahau kutuzimia?
 
mm tv na king'amuzi chake haviwaki sijui nilikosea nn.

Angalia cable za power ili angalau uone screen ya tv inawaka.
king'amuzi kikiwaka, basi hapo utapata channels. kama channels haziji, check connections za cable ya antena.
 
Vipi jamaa walioko mikoa mingine kama Mwanza, Arusha, MBEYA, n.k. watuambie vipi huko ?

huku mbeya hawajazima mitambo maana wengi tunatumia madishi tofauti na dar mnaotumia antena za chadema, mifupa ya samaki na tubelight
 
kama upo dar tafuta cha ting, ni watu wa atn nadhani wana local chanels nyingi kwa sie wapenda taarifa. Kama upo moro au dodoma tafuta cable tv, wana local chanels na ligi kuu ya uingereza kama kawa

Acha kumshauri vibaya mwenzio. Hao ting wababaishaji. Kama uko dar chukua Easy Tv
 
kama upo dar tafuta cha ting, ni watu wa atn nadhani wana local chanels nyingi kwa sie wapenda taarifa. Kama upo moro au dodoma tafuta cable tv, wana local chanels na ligi kuu ya uingereza kama kawa

Ahsante mkuu.
 
Bonyeeeeeeee mambo ya digitale yakheeeeee kitu laini kama unanawa yalaaaaaa mdebwedoooo!
 
Jamani mi cna king'amuz, hivyo naiombeni mnijuze nyie mnaotumia ving'amuz, ni king'amuz gan kilichoshiba local channels baada ya kuzima huo mtambo wa analojia? HESHIMA KWENU WAKUU.
Tafuta decoder ya Easy Tv, wapo pale Zonghua Garden, Morocco. Wao unapata local channels almost zote, kasoro Ctn. Ni jamaa wazuri sana. Wanauza decoder yao sh. 140,000/- na kila mwezi unalipia sh. 9000/-
 
Mkuu nipo kwa dgital toka mwanzo natumia startime,baada ya kuzima dezo chanel nafungua kingamuzi WAMEKATA clouds,C.TEN na zingine zimebaki Itv,Itv na Dtv na za nje, inakuwaje IMEKULA KWANGU?
 
We FUNGE mbona mimi IMEKATA hata hiyo Tbcm? Yaani niponipo tu kama sijavaa ch...itakuwaje?
 
Msinunue Decoder za Kianalogue ambazo haziwezi hata kurekodi kipindi chochote... Ni Bora kuwasubiri StarTV au Decoder za Mengi tu... Nyanidume Hud Idimi kama Huduma za Cable Tv (ctv ) hazipo karibu mimi nafaidi sana kwa huduma za Ctv Decoder zao ni za kisasa kabisa....
 
Back
Top Bottom