Je, haiwezekani kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wanao kiuka viapo vyao?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
Jana nilimsikia Mhe. Rais alipo kuwa ana waapisha Mawaziri walio teuliwa kuwa viongozi wote wanao wajibu wa kuzingatia viapo vyao na kuzingatia katiba Ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kuchunga mipaka yao lakini pia kuzingatia kiapo cha maadali kwa kutunza siri.

Mara kwa mara inaonekana baadhi ya viongozi walio teuliwa na Rais wamekuwa wakikiuka viapo vyao, sasa je? hakuna namna ya kuwachukulia hatua za kisheria kama vile kufikishwa mahakamani zaidi ya kuwatumbua?

kama kuna sheria inayo weza kuwafikisha mahakamani nashauri itumike sasa ili kuondoa tatizo hili au kama hakuna basi Bunge letu liangalie namna ya kutunga sheria ili kuwathibiti viongozi watukutu.

maana sisi wananchi tumechoka kuona Rais wetu anashughulishwa na baadhi ya viongozi wasio taka kuheshimu viapo vyao.

Kama kiapo ni ahadi ya kisheria, sasa hao wanao apa kiapo cha kutunza siri halafu baadae wanakiuka kiapo ndio iishie tu kuwatumbua? hakuna namna ya kuwachukulia sheria.
 
Na hili lingekuwa ni suluhisho la viongozi kutekeleza majukumu yao vyema kwa mujibu wa viapo vyao,mara nyng viapo ni geresha tu,wanayoyafanya ni tofauti na wayoyanena kweye hivyo viapo

Ngoja tuone manguli wa Sheria watasemaje ktk hili
 
Watu. Wa kuchukuliwa hatua kwa kuvunja katiba ni Raisi,spika,makamu,waziri mkuu,Hawa wamekuwa wakivunja katiba kwa kipindi kirefu.
Raisi wako ni dhaifu sana,anaogopa wenye elimu na waliomzidi kiwango Cha exposure,Mulamula katumbuliwa kwa sababu ya hizi picha,Wakati Raisi yupo Msumbiji anazindua halmashauri,Akili kubwa kutoka Bukoba.

20221003_085318.jpg
20221003_085307.jpg
20221003_085312.jpg
 
Watu. Wa kuchukuliwa hatua kwa kuvunja katiba ni Raisi,spika,makamu,waziri mkuu,Hawa wamekuwa wakivunja katiba kwa kipindi kirefu...
mada yangu haikumlenga mulamula bali nimeongelea kwa ujumla, viongozi wanao teuliwa na kisha kuapa kuzingatia katiba na kutunza siri halafu wakavunja au kukiuka viapo vyao, je hakuna uwezekanao wa kushitakiwa zaidi ya kutumbuliwa?

akili kubwa kazi yake ni kutafakari kabla ya kutenda, kinyume chake hiyo ni akili ndogo.

Hapa natafuta jinsi ya kukomesha tabia hii kwa baadhi ya viongozi watukutu wasio ambilika.
 
Kwa nchi masikini kama tanzania,sheria huwa ziko kwa ajili masikini na siyo viongozi
hakika nasema endapo kama kiongozi yeyote akikiuka kiapo chake kisha pakawepo utaratibu wa kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo la kuvunja kiapo chake na akahukumiwa jela miaka 5, naamini hakuna atakaye rudia ujinga, wote watanyooka barabara.
 
Mara kwa mara inaonekana baadhi ya viongozi walio teuliwa na Rais wamekuwa wakikiuka viapo vyao, sasa je? hakuna namna ya kuwachukulia hatua za kisheria kama vile kufikishwa mahakamani zaidi ya kuwatumbua?

kama kuna sheria inayo weza kuwafikisha mahakamani nashauri itumike sasa ili kuondoa tatizo hili au kama hakuna basi Bunge letu liangalie namna ya kutunga sheria ili kuwathibiti viongozi watukutu.
Mtu afikishwe mahakamani kwa kupiga picha!
 
Mtu afikishwe mahakamani kwa kupiga picha!
kuna mambo ya Msingi sana yametamkwa na Mhe. Rais.
1. Kutunza/kufuata Viapo
2. Kutunza Siri.
3. Kuheshimu mipaka ya majukumu kwenda juu na kushuka chini
Hayo mambo makubwa 3 ni muhimu sana kuyapigia mstari.
 
Back
Top Bottom