Je Hadi Sasa Mungu hajamtumia mtumishi wake yeyote kuongea na Rais au anakubaliana na Ushwari wa kitaifa?

Je Hadi Sasa Mungu hajamtumia mtumishi wake yeyote kuongea na Rais au anakubaliana na Ushwari wa kitaifa?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,461
Reaction score
23,241
Rais ni mtumishi wa Mungu anayetumika katika kitengo cha kutawala watu kiserikali. Kwa mujibu wa ISAYA 49, watumishi wa Mungu wa KIROHO ni walezi wa wafalme na mamalikia na marais.

Kama Kuna chochote kisichofaa, ili kuepusha MADHARA ya baadae atatumwa mtumishi hata kutoka nje ya nchi ili kumpa Rais au wasaidizi wake nini cha kufanya.

Zoezi hilo halikufanyika KWA public broadcasting ( kupayuka hovyo Barabara au mitandaoni) bali moja KWA moja KWA muhusika na system yake. Wote waliotii walikula mema ya nchi.

Hii haikujalisha kama huyo Rais anamuamini au hamuamini Mungu maana wote huwa wanawekwa na Mungu hata kama kajiweka kibabe.

Mfano
Mtu wa Mungu alitumwa huko Dani na Betheli kumuonya Rais wa Israel kusini Yeroboamu.

Nathan aliingia Ikulu kumuonya Daudi.

YOHANA mbatizaji Aliingia Ikulu kumuonya Rais Herode mtoto wa herode mkuu.

Senakeribu kutoka Syria alipotaka kuivamia Israel Elisha alijulishwa akaingia Ikulu moja KWA moja na kutoa USHAURI ulioliokoa taifa.

Paulo aliingia Ikulu ya Cyplus kumpa maneno ya neema Rais Sergio Paulus aliyekuwa amezunguwa na Chawa mchawi.

Yona alihubiri Hadi Ikulu huko Ninawi na Rais akafanya maamuzi ambayo yaliokoa taifa

Kama kwetu ni kimya?

1: Je Mungu ameridhia utumishi wa Mama na anaunga mitano Tena?

2: Je nchi haina changamoto ya haraka ambayo halihitaji Mungu ahangaishe Bure watumishi wake?

3: Wanatumia kisirisiri na Kila malalamiko yako kwenye pipeline ya kushughulikiwa?

4: Watanzania hawana haja ya Mungu kuingilia kwenye mambo yao. Hivyo na yeye anasikilizia.

5: Malalamiko yetu ni kawaida kiasi cha kutohitaji uingiliaji wa Mungu. Na waombaji wote wameacha kuomba au wanaomba vibaya.

Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi.
 
Kama Kuna chochote kisichofaa, ili kuepusha MADHARA ya baadae atatumwa mtumishi hata kutoka nje ya nchi ili kumpa Rais au wasaidizi wake nini cha kufanya.


Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi.
Mtumishi Ndlovu wa Zimbabwe alitumwa na Mungu, ujumbe wake wa Agosti 2021 huo hapo chini.

Pray for the lady president.
 
Mtumishi Ndlovu wa Zimbabwe alitumwa na Mungu, ujumbe wake wa Agosti 2021 huo hapo chini.

Pray for the lady president.
View attachment 3444206
Huu ni unafiki. Mtu akitumwa KWA mtu anamface muhusika KWA mujibu wa pattern ya mifano niliyoitoa. Wote wanaoongea mitandaoni na makanisani jambo linalomuhusu mtu aliyeikulu KWA mtazamo wangu wanajituma na wengine ni wabashri tu kama wale jamaa wa nyota
 
Huu ni unafiki. Mtu akitumwa KWA mtu anamface muhusika KWA mujibu wa pattern ya mifano niliyoitoa. Wote wanaoongea mitandaoni na makanisani jambo linalomuhusu mtu aliyeikulu KWA mtazamo wangu wanajituma na wengine ni wabashri tu kama wale jamaa wa nyota
Mtazamo wako, hakuna anayebisha. Hata kwa Jiwe wapo waliosema kama usemavyo wewe.

Dunia ya kidijitali tuendelee kutumia njia zilizotumika miaka zaidi ya 2000 iliyopita. This is weird.
 
WANA CCM TENA WANEC ,Mungu anakupa washauri wa kukuonya wa ndani na nje
VIONGOZI
1)askofu GWAJIMA
2)Hamphfrey Polepole


WAZEE
1)Warioba;
2)BUTIKU

VIONGOZI WA DINI
1)sheikh Ponda na wengine
2)mapadre ,maa askofu,wachungaji,manabii n.k

WANACHI WA KAWAIDA/RAIA

soma comments za mitandao ya kijamii hata hapa jf watu wanashauri vizuri,sio kusikiliza machawa tu wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa walamba viatu.

ANGALIZO :Lakini kusikiliza ushauri inategemea na mshauriwa amejiambatanisha na madhabahu gani/ana imani gani.IMANI YA MSHAURIWA.

MFANO Nabii Musa alitumwa na Mungu akamfuata mfalme PHARAO wa nchi ya Misri,akwambie MUNGU AMEMTUMA AMESEMA ,WAFUNGULIE HURU (waachie huru hawa wafungwa,uliowafunga utumwani wana wa israeli..

( UJUMBE kwa wakati HUU wa leo NI SERIKALE IMWACHIE HURU TINDU LISU),UHURU WA KUABUDU iruhusu watu wa dini zote waabudu bila kufungia baadhi ya makanisa,..HAKI YA KUISHI..ikomeshe MAUAJI watu kutekwa na watu wasiokulikana na kuuwawa,watu kitekwa na hawajulikani walipo...UHURU wa kisiasa ,watu waruhusiwe kushiriki siasa za vyama vingi,wafuasi wq chadema waruhusiwe kushiriki siasa,..
Wakosoaji warhihusiwe KUKOSOA NA KUSHAURI...
watu tuko zaidi ya milioni 60 tuna maoni tofauti HATUWEZI WOTE TUKAWA NA AKILI MOJA ya UCHAWA na kujipendekeze kulamba lamba viatu na KUSIFIA SIFIA...kubali kukosolewa ...HAKUNA MTU ASIYEKOSOLEWA...

Musa wakati anapewa ujumbe na na Mungu akaomba Mungu ampe uwezo wa kufanya ishara za kumuonyesha mfalme Pharao wa Misri ili akiziona hizo aamini kuwa ni Mungu ndiye aliyemtuma.


LAKINI MFALME PHARAO ALIFANYA MASIKIO YAKE KUWA KIZIWI,na Macho yake kuwa kipofu...bado alikataa hizo ishara nyingi zaidi ya 9

AKASEMA HIZO ISHARA HATA MAJINI YAKE ANAYOFUGA,na waganga wake wa kienyeji anaowategemea na kumpigia ramli , kumtabiria mambo yajayo mbeleni, WANAWEZA KUFANYA miujiza kama hizo za Musa alizopewa na Mungu,huku akicheka kwa dharau na kejeli.


mpaka ishara ya 10 ya PIGO LA KUFIWA NA mwanawe,akakubali nusu akawaruhusu kwa muda japo walipotoka nje akawafuata tena kuwakimbiza awakamate ,Mungu akapasua bahari ya SHAM mateka wakapita katikati ya bahari...yani hata ISHARA KUU kama hii bado mfalme Pharao alojitia ukiziwi na upofu hakuona uwezo wa Mungu,..
.ni sawa na ISHARA YA WAKATI HUU WA KEO NI LISU KUPONA risasi 16 ,sina uhakika kama kuna mtu duniani aliyewahi kupigwa risasi 16 akapona ..huu ni muujiza mkubwa wa Mungu,Huyu Mtu TINDU LISU,amebeba kusudi la Mungu.

Kilichowapata Pharao na jeshi lao walipoendelea na ku prosecute /kuwafuatilia wana israeli hata katikati ya bahari Mungu aliyowatengenezea njia katikati ya bahari ili waisraeli wapite kurudi kwao kutoka Misri utumwani......wote tunakijua WOTE WANAOSHINDANA na HAKI YA MUNGU HUISHIA KUANGUKIA PUA...

HITIMISHO
Kusikiliza ushauri unaotokewa kuna tegemea na imani ya anayeshauriwa ,kama anayeshauriwa ana amini waganga wa kienyeji na majini sio rahisi KISIKILIZA ,atakuwa KIZIWI kama Pharao wa Misri mpaka apate PIGI KUU ,hata baada ya pigo kuu anaweza akawndelea kuwa na moyo mgumu mpaka MAUTI.
 
Back
Top Bottom