Je, G55 ndio Wale Nyoka ndani ya CHADEMA?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,171
Reaction score
79,626
Habari za Jumapili!

Kila chama kina watu ndumilakuwili,snitch, Wasaliti na Nyoka.

Kijasusi Tofauti kubwa ya Nyoka na Panya ipo kwenye kujificha na kujihami.
Nyoka anaweza kuingia katika Nyumba yako akakaa hata Miaka mitano Mpaka akawa chatu au Nyoka Mkubwa na wewe usijue kuwa ndani ya nyumba yako kuna kiumbe Hatari upo nacho Muda mrefu lakini wewe hujui.
Udhaifu wa Nyoka mara baada ya kutambua uwepo wake NI katika kujihami usimuue. Nyoka ukimuona Leo ndani ya nyumba yako uhakika wa kumuua ni siku hiyohiyo. Nyoka Hana ujanja wa kukimbia Kifo. Tofauti na Panya

Panya,
Kwa upande wa Panya yeye, hana uwezo wa kujificha, Panya akiingia Leo Basi NI siku hiyohiyo utajua kuwa nyumba yako inaugeni wa Panya. Akijitahidi Sana kujificha Panya Basi atachukua siku mbili tuu lakini kamwe haiwezi kuzidi siku Tatu usitambue nyuma yako ina Panya.

Panya unaweza kumuona Leo ndani ya nyumba yako lakini kumuua ikakuchukua wiki nzima ukihangaika naye.
Panya ni mzuri kwenye kujihami kuuawa.

Kiintelejensia, Nyoka kwa kujua kuwa siku atakayokamatwa hawezi kukimbia Kifo ndio maana hutumia Akili nyingi Sana kujificha..

Kumgundua Rafiki Nyoka,
Au kwenye siasa kumjua mtu Nyoka ni Kazi ngumu zaidi kwa Sababu wengi wao ni wajanja katika kujificha na sio kwamba wanaakili nyingi za mambo ya maana.

Kiintelejensia, kwenye Jeshi au Usalama wa Taifa Nyoka wakati wa kujihami akihisi unaanza kumshtukia na kumfutilia. Nyoka huweza kukuuma na kukuua ili usitoe Siri kuwa ndani ya Jeshi kuna msaliti anayetoa Siri kwa adui.

Kwenye vyama vya siasa nyoka wapo, Kanuni Zao ni zilezile. Kujificha sana lakini akiaanza kuhisi usalama wake umeanza kuwa mdogo au watu wameanza kumshtukia. Huweza kuua. Au kumfanyia Mhusika Blackmail ili kujihakishia Usalama.

Kila chama cha siasa kina nyoka
Ubaya unakuja pale ambacho chama cha siasa kuwa na Nyoka wengi tena kwenye Nafasi za maana au Nyoka hao kupewa Fursa ya kuwafikia wananchi na kuwa na nguvu ya ushawishi kupitia mitandao.

Nyoka ukilala uchi chumbani kwako anakuona wewe humuoni.
Ukibadilisha nguo zako anakuona.
Ukilala na Mkeo au Mumeo anakuona,
Ukiingoza hawara au Malaya anakuona.
Ukiwasiliana na watu anakuona.
Alafu wewe hujui kama unaonwa. Huyo ni Nyoka.

Mtaani unapita kwa kujiamini kumbe watu wanakuchora. Nyoka kafanya yake.
Mipango yako unayoiona ya Siri kumbe watu wanaijua. Nyoka kafanya yake.

Nyoka ni adui na ndio maana lazima ashirikiane na adui zako. Hiyo ni Kanuni

Kuna kitu wengi hawakijui kuhusu Nyoka.
Moja ya dalili za Awali kumtambua Nyoka ni uwezo wake wa kujua baadhi ya taarifa kutoka kwa adui yako.

Upo na mtu lakini kila mara anakuwa wa Kwanza Kupata taarifa na kujua kinachoendelea upande wa Pili.
Anakuwa WAKWANZA kukuhabarisha. Na unashangaa baada ya muda mchache habari aliyokupa inajitokeza mbele za Umma na ni habari ya Kweli.

Kijasusi, kama una mtu wa aina hii kwa Sisi Watibeli lazima uanze kumtilia mashaka.
Ni lazima taarifa hizo anazitoa kimkakati. Ni taarifa ambazo zipo planned na hazina athari yoyote kwa adui yako.
Nyoka akikupa taarifa lazima ujue taarifa hiyo haina madhara kwa adui yako Mkubwa.
Kwa sababu kikawaida Nyoka hawezi kuwa kinyume na adui yako Mkubwa.

Lengo la yeye kukupa taarifa au kutoa taarifa ni aidha kujenga Uaminifu wake kwako. Lakini la Pili ni kujua mipango yako.
Na atahakikisha anakuseti utoe mipango na mikakati yako. Kisha ataonyesha kuguswa na kukusaidia kwa namna ya kufanikisha mipango na mikakati yako ili kukuweka karibu zaidi.

Swali Linakuja je G55 ndio Nyoka wa CHADEMA?

Nakabidhi Maiki

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Inafikirisha mkuu
 
Wakati wa Nyoka kukuuma au kuangusha Ngome Yako!

1. Nyoka atakuuma pale ukimkanyaga.
2. Nyoka atakutemea mate pale utakapomuona.
3. Nyoka atakukabili vilivyo ukiyasogelea mayai yake au watoto wake.

4. Nyoka ataungana na adui zako waziwazi pale atakapoona Hana Muda mwingine WA maana zaidi ya huo.

4. Nyoka atajitokeza waziwazi pale atakapoona upo kwenye target yake. Yaani umeingia kwenye mfumo
 
Habari za Jumapili!

Kila chama kina watu ndumilakuwili,snitch, Wasaliti na Nyoka.

Kijasusi Tofauti kubwa ya Nyoka na Panya ipo kwenye kujificha na kujihami.
Nyoka anaweza kuingia katika Nyumba yako akakaa hata Miaka mitano Mpaka akawa chatu au Nyoka Mkubwa na wewe usijue kuwa ndani ya nyumba yako kuna kiumbe Hatari upo nacho Muda mrefu lakini wewe hujui.
Udhaifu wa Nyoka mara baada ya kutambua uwepo wake NI katika kujihami usimuue. Nyoka ukimuona Leo ndani ya nyumba yako uhakika wa kumuua ni siku hiyohiyo. Nyoka Hana ujanja wa kukimbia Kifo. Tofauti na Panya

Panya,
Kwa upande wa Panya yeye, hana uwezo wa kujificha, Panya akiingia Leo Basi NI siku hiyohiyo utajua kuwa nyumba yako inaugeni wa Panya. Akijitahidi Sana kujificha Panya Basi atachukua siku mbili tuu lakini kamwe haiwezi kuzidi siku Tatu usitambue nyuma yako ina Panya.

Panya unaweza kumuona Leo ndani ya nyumba yako lakini kumuua ikakuchukua wiki nzima ukihangaika naye.
Panya ni mzuri kwenye kujihami kuuawa.

Kiintelejensia, Nyoka kwa kujua kuwa siku atakayokamatwa hawezi kukimbia Kifo ndio maana hutumia Akili nyingi Sana kujificha..

Kumgundua Rafiki Nyoka,
Au kwenye siasa kumjua mtu Nyoka ni Kazi ngumu zaidi kwa Sababu wengi wao ni wajanja katika kujificha na sio kwamba wanaakili nyingi za mambo ya maana.

Kiintelejensia, kwenye Jeshi au Usalama wa Taifa Nyoka wakati wa kujihami akihisi unaanza kumshtukia na kumfutilia. Nyoka huweza kukuuma na kukuua ili usitoe Siri kuwa ndani ya Jeshi kuna msaliti anayetoa Siri kwa adui.

Kwenye vyama vya siasa nyoka wapo, Kanuni Zao ni zilezile. Kujificha sana lakini akiaanza kuhisi usalama wake umeanza kuwa mdogo au watu wameanza kumshtukia. Huweza kuua. Au kumfanyia Mhusika Blackmail ili kujihakishia Usalama.

Kila chama cha siasa kina nyoka
Ubaya unakuja pale ambacho chama cha siasa kuwa na Nyoka wengi tena kwenye Nafasi za maana au Nyoka hao kupewa Fursa ya kuwafikia wananchi na kuwa na nguvu ya ushawishi kupitia mitandao.

Nyoka ukilala uchi chumbani kwako anakuona wewe humuoni.
Ukibadilisha nguo zako anakuona.
Ukilala na Mkeo au Mumeo anakuona,
Ukiingoza hawara au Malaya anakuona.
Ukiwasiliana na watu anakuona.
Alafu wewe hujui kama unaonwa. Huyo ni Nyoka.

Mtaani unapita kwa kujiamini kumbe watu wanakuchora. Nyoka kafanya yake.
Mipango yako unayoiona ya Siri kumbe watu wanaijua. Nyoka kafanya yake.

Nyoka ni adui na ndio maana lazima ashirikiane na adui zako. Hiyo ni Kanuni

Kuna kitu wengi hawakijui kuhusu Nyoka.
Moja ya dalili za Awali kumtambua Nyoka ni uwezo wake wa kujua baadhi ya taarifa kutoka kwa adui yako.

Upo na mtu lakini kila mara anakuwa wa Kwanza Kupata taarifa na kujua kinachoendelea upande wa Pili.
Anakuwa WAKWANZA kukuhabarisha. Na unashangaa baada ya muda mchache habari aliyokupa inajitokeza mbele za Umma na ni habari ya Kweli.

Kijasusi, kama una mtu wa aina hii kwa Sisi Watibeli lazima uanze kumtilia mashaka.
Ni lazima taarifa hizo anazitoa kimkakati. Ni taarifa ambazo zipo planned na hazina athari yoyote kwa adui yako.
Nyoka akikupa taarifa lazima ujue taarifa hiyo haina madhara kwa adui yako Mkubwa.
Kwa sababu kikawaida Nyoka hawezi kuwa kinyume na adui yako Mkubwa.

Lengo la yeye kukupa taarifa au kutoa taarifa ni aidha kujenga Uaminifu wake kwako. Lakini la Pili ni kujua mipango yako.
Na atahakikisha anakuseti utoe mipango na mikakati yako. Kisha ataonyesha kuguswa na kukusaidia kwa namna ya kufanikisha mipango na mikakati yako ili kukuweka karibu zaidi.

Swali Linakuja je G55 ndio Nyoka wa CHADEMA?

Nakabidhi Maiki

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Hatari, nani angeweza kufikiri kuw Mbowe anaweza luwacadui wa CDM?
 
Nimeandika mahali...njaa mbaya...wanaojiita G55 ni njaa inawasumbua hadi kuamini labda mwaka huu 2025 dola na chama cha kijani watabadilika na kuwaachia majimbo...jambo ambalo ni gumu
 
Ingawa siwaungi mkono hao G55, ila naona kuna shida kubwa sana (hasa kwa upinzani) kukubaliana na mtazamo tofauti kutoka kwa watu wengine.

Ukiwa na mawazo tofauti na upinzani unaonekana we ndo msaliti namba moja nchini, sijui hii imetoka wapi!!
 
Hii ni moja ya kampeni ya kuua G55??

Nyoka anawatemea mate?😌 kabla ya kuua

Safari hii mbona hamsemi mitafaruku hii ni Demokrasia?
 
Demokrasia inakanuni zake na mahali pake.
CCM Wana demokrasia Yao, CHADEMA Wana demokrasia Yao.
Taifa Lina demokrasia yake.
Wazungu Wana demokrasia Yao.

Inategemea
 
Ingawa siwaungi mkono hao G55, ila naona kuna shida kubwa sana (hasa kwa upinzani) kukubaliana na mtazamo tofauti kutoka kwa watu wengine.

Ukiwa na mawazo tofauti na upinzani unaonekana we ndo msaliti namba moja nchini, sijui hii imetoka wapi!!

Watu hawapingi Mawazo tofauti ila wanapinga Hatua zinazochukuliwa na kufuatwa na hayo Mawazo tofauti yanayovunja Sheria za chama husika au sheria za nchi husika
 
Uko sahihi mkuu na ndo maana nimesema siwaungi mkono.

Ila ukisoma coments za watu wengi humu mitandaoni, utaona kuna shida kubwa sana, hasa kwenye kuelewa watu wenye mitazamo tofauti.
 
Hii nchi kupata ukombozi ni ngumu sana, wenye akili na uwezo ni wachache sana.....tuliobaki Mungu ndo anajua.
 
Back
Top Bottom