Je familia ya Mwangosi wanaweza kuishitaki serikali kama ilivyofanya familia ya Lt.Gen.Kombe??

Nilishafungua kesi hiyo na jambo hilo sasa hivi linashughulikiwa na Nebraska District Court. Kwa kwa sasa hivi siwezi kuongelea zaidi jambo ambalo bado liko mahakamani.

Teh teh teh....I just don't believe you but it's ok.
 
Hapana, Mwangosi ameuwawa na polisi waliokuwa ndani ya uniform wakifanya kazi yao kipolisi kwa mujibu wa sheria, kwa hiyo walikuwa wakifanya kazi kwa niaba ya serikali, na hivyo serikali inahusika moja kwa moja. Angeuwawa na polisi mitaani kwa sababu zao binafsi ndipo hoja yako ingekuwa sahihi.
itabidi hata polisi akila rushwa akiwa kwenye uniform, selikali ndio iwajibike kwasababu alikuwa anafanya kazi akiwa kwenye uniform za serikali? ndio tuseme hivyo?, ....inawezekana kabisa selikali ikawa responsible for the wrongs of its servants...lakini wale servants wanatakiwa wawe walikuwa wanafanya shughuli walizotumwa na mkubwa wao. superior anaweza kuwa responsible for the wrongs of the subordinate only where he commanded it be done, au labda tuseme yale mambo aliyoyafanya polisi yalikuwa part of his day to day duties. tuseme polisi kazi yao ni kuua wananchi? ....nawezasema kwamba, inawezekana na pia inaweza kuwa haiwezekani, ngoja kwanza nikaperuzi kwenye madesa na case law, ndio nitatoa jibu la maana. nawaachia wenzangu muendelee kuchangia.
 
Ubungoubungo,

..kama unaweza tafuta kesi aliyofungua mjane/familia ya Imran Kombe dhidi ya serikali.

..sidhani kama kuna ugumu hapa. hii inapaswa kuwa kesi ya madai kama zilivyo kesi nyingine za namna hiyo.

..mfano mwingine: serikali ilibeba mzigo wa fidia baada ya waziri Magufuli kutoa amri ya kuvunja kituo cha polisi Mwanza. U would think aliyepaswa kushitakiwa ni Magufuli binafsi, lakini ilishtakiwa serikali kwasababu Magufuli alikuwa anatekeleza majukumu yake kama mtumishi wa serikali.

..Polisi wameua wakiwa kazini, wakiwa na uniform, wakitumia silaha walizopewa na serikali ya Jamhuri wa Tanzania. kwa msingi huo hapa kesi ya MADAI itakuwa ni dhidi ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

..kwa upande mwingine Jamhuri nayo itawashitaki Polisi wake kwa kufanya mauaji. tena kwa kufanya hivyo Jamhuri inajichongea yenyewe kwenye kesi itakayofuatia ya madai.
 
Last edited by a moderator:
..napendekeza zaidi ya rambirambi, lipatikane JOPO LA WANASHERIA litakalowasaidia familia ya Mwangosi na yule kijana aliyeuwawa Morogoro.

Kwa Lulu mbona wamejitokeza faster kwa mwandishi hakuna mtu alieonyesha interest ya kusaidia haki ipatikane
 
itabidi hata polisi akila rushwa akiwa kwenye uniform, selikali ndio iwajibike kwasababu alikuwa anafanya kazi akiwa kwenye uniform za serikali? ndio tuseme hivyo?, ....inawezekana kabisa selikali ikawa responsible for the wrongs of its servants...lakini wale servants wanatakiwa wawe walikuwa wanafanya shughuli walizotumwa na mkubwa wao. superior anaweza kuwa responsible for the wrongs of the subordinate only where he commanded it be done, au labda tuseme yale mambo aliyoyafanya polisi yalikuwa part of his day to day duties. tuseme polisi kazi yao ni kuua wananchi? ....nawezasema kwamba, inawezekana na pia inaweza kuwa haiwezekani, ngoja kwanza nikaperuzi kwenye madesa na case law, ndio nitatoa jibu la maana. nawaachia wenzangu muendelee kuchangia.

Mfano uliotumia una walakini mkubwa sana; ni kama vile unalinganisha machungwa na maembe. Unasahau kuwa rushwa ni kosa la jinai linalohusisha watu wawili: mtoaji na mpokeaji rushwa unless liwe limefanyika kwa mtego wa kumnasa mmoja wao kukiwa na ushahidi wa awali kuwa mtu huyo ana tabia ama ya kutoa au kupokea rushwa. Kwa apokeaji rushwa, mtego huo hutumia pesa zenye alama maalum.

Kosa lililoko mbele yetu linahusisha mtumishi wa serikali ambaye alifanya kosa hilo akiwa anatekeleza amri halali za serikali alizopokea kutoka kwa wawakilishi wa serikali hiyo na akiwa amepewa zana za kutekeleza amri hizo, na akawa ametumia zana hizo hizo alizopewa na serikali hiyo.

This government cannot run away out of this mess.
 
kisheria fmilia inaweza kuishitaki serikali kama ilivyofanya familia ya kombe.wanaweza kudai fidia katika sheria ya athari/madhara yaani tort law.
 
Hebu wanasheria maarufu wenye mapenzi mema na nchi hii mtusaidie kuliangalia hili suala kwa mapana kama inawezekana ili serikali ibanwe kisheria. Kwa mtizamo wangu naona inawezekana. Wenye taaluma zao washauri zaidi.
 
Back
Top Bottom