Je familia ya Mwangosi wanaweza kuishitaki serikali kama ilivyofanya familia ya Lt.Gen.Kombe?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je familia ya Mwangosi wanaweza kuishitaki serikali kama ilivyofanya familia ya Lt.Gen.Kombe??

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by JokaKuu, Sep 8, 2012.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..naomba msaada wa wanasheria hapa wenye uelewa wa kesi ya madai ya familia ya Lt.Gen.Imran Kombe.

  ..hivi Daudi Mwangosi hakuuwawa katika mazingira yanayofanana-fanana na mauaji ya Imran Kombe??

  ..Mwangosi amekufa kutokana na uzembe na ukatili wa askari polisi, sioni kwanini familia yake wasifungue shauri dhidi ya Polisi na Jamhuri.

  ..nawasilisha.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,195
  Trophy Points: 280
  ...Mie si mwanasheria lakini kwa maoni yangu Serikali ina kesi ya kujibu hapa. Familia ya Mwangosi inastahili kulipwa fidia kubwa tu kutoka Serikalini. Tatizo ni kwamba mahakama zetu nazo haziko huru kabisa kwenye kesi kama hizi zinazoihusu Serikali.
   
 3. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  I second the motion. mkuu

  Pia mimi ni layman hasa wa penal codes. Lakini ni vema na haki kama wanasheria wetu watashiriki na kuwezesha familia ya marehemu Mwangosi kufungua kesi dhidi ya Polisi na JMT.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..napendekeza zaidi ya rambirambi, lipatikane JOPO LA WANASHERIA litakalowasaidia familia ya Mwangosi na yule kijana aliyeuwawa Morogoro.
   
 5. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  si mweledi wa sheria lakini kwa hili la mwangosi inawezekana kudai na kufidiwa ,tena hii hiko tofauti sana .na ya kombe .watalipwa haraka .kwani ushaidi wote hupo .vidio na wawatu ,
   
 6. M

  Mzee wa fund JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napendekeza familia ya mwangosi na yule kijana wa morogoro waishitaki serikali.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa waishitaki serikali ili watakachopata wasomeshe watoto na kuendeleza miradi yao ....ya kula kila siku!!uonevu dhahiri kabisa!huyo Kamuhanda ingekuwa mtoto wa dada yake angekubali kweli kumuua bila hatia?
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..tena inawezekana kuwashitaki askari wote waliokuwa wakipiga kwa MAUAJI.

  ..inawezekana Mwangosi alishakata roho kabla hata ya kulipuliwa na bomu.

  ..halafu kwasababu alikufa kwa kipigo, kamanda aliyetoa amri ya kumpa kipigo naye aunganishwe ktk kesi ya mauaji.
   
 9. n

  ngonani JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 1,371
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hii sio kesi ya penal code,ni kesi ya madai,na ni kweli familia watafute mawakili wazuri wanaoweza kusaidia pro bono.Wafungue kesi
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  haiwezekani kuishitaki serikali kudai fidia kutokana na kifo cha mwangosi, kwasababu hapo hakuna sababu ya kuifanya mahakama iilazimishe serikali kutoa fidia. kwanza kabisa, elewa kwamba, mwangosi hakuuawa na serikali, aliuawa na individual persons ambao kwa haki kabisa wanatakiwa wakamatwe na kufunguliwa shitaka la mauaji. nashangaa hadi sasa hajakamatwa mtu, labda wanasubiri hiyo tume. naamini wale polisi waliohusika kuua watakamatwa, kwasababu waliua sio kwasababu wametumwa na serikali wauwe, waliua kwasababu wameamua wao wenyewe tu kuua.

  sasa, kama wauaji watakamatwa na kufikisha mahakamani kwa murder au manslaughter(badae baada ya kusoma jalada kwa state attorney kama wataona ni manslaughter), anayetakiwa kutoa fidia hapo ni wale wauaji au serikali? serikali hapo inahusikaje? kwani pale walikuwa wanafanya kazi ya mauaji au ilikuwa ordinary duties za mapolisi?...ordinary duty ya polisi sio kuua,...kama polisi atafanya kinyume na vile terms za ajira yake zilivyo atabeba individual responsibility kwa aliyoyatenda. kitakachoendelea sasaivi ni kesi ya criminal dhidi ya wauaji...baadae sasa ndo labda kesi ya madai itafunguliwa kwa wauaji, lakini si serikali kwasababu serikali haikuhusika kwa namna yeyote ile na haiwezi kubeba makosa ya mwajiriwa wake katika mazingira kama haya...labda yangekuwepo mengine.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hakuna kesi za penal code, kuna kesi za jinai na kesi za madai. mnataka kufungua kesi ya madai kumdai nani? muuaji wa mwangosi au mwajiri wa muuaji wa mwangosi? kwa namna gani sasa.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  Ubungoubungo,

  ..kuna sheria fulani inaitwa VICARIOUS LIABILITY nadhani inaweza kutumika hapa.

  ..uko sahihi kwamba polisi wale hawakutumwa na serikali kuua. kwa msingi huo wanapaswa kushitakiwa kwa MAUAJI.

  ..halafu kuna kesi nyingine ya MADAI, ambapo jeshi la polisi na serikali wanaweza kishitakiwa kutokana na uzembe wa watumishi wao, yaani wale askari waliomuua Mwangosi.

  ..katika suala la Lt.Gen.Imran Kombe, askari waliotenda kosa walishtakiwa na kuhukumiwa kwa kosa la mauaji. serikali nayo ilifunguliwa kesi ya madai na mjane wa Lt.Gen.Kombe alilipiwa milioni mia kadhaa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kuna nadharia na vitendo.

  Kinadharia mtu yeyote anaweza kufungua kesi kudai haki. Kivitendo katika dunia ya leo haki inanunuliwa. Nikisema kunuuliwa simaanishi rushwa ila ni kwamba kote duniani utafuta haki ni swala linalohitaji fedha za kuajiri wanasheria na kudhibiti vitimbi mbalimbali vya unayemshtaki.

  Kwa jinsi familia ya Mwangosi ilivyo dhaifu kiuchumi, kuwashauri wafungue kesi dhidi ya serikali ni kuwatafutia matatizo zaidi.
   
 14. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mkuu wewe ni Mwanasheria? Hata General Kombe aliuawa na Individual person, serikali haikumtuma.
  Yes! Familia ya Mwangosi wanayo haki ku SUE Serikali kwa Maauaji ya Mwangosi. Yule Individual aliyeua alikuwa anatekeleza wajibu wake kwa amri aliyopewa na wakuu wake kikazi. Serikali inahusika moja kwa moja, sababu yule individual ni mwajiriwa wa serikali na alikuwa kazini wakati wa tukio. Serikali ilimwajiri, kumpa mafunzo na kumwamini amefauli minimum knowledge to handle the weapon. Haiwezekani kupewa siraha kama hakuwa amefikia vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Jeshi la Police.
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wewe ndio unaongea sense, sitakubishia kabisa hadi nikaperuz, kwasababu unaongea kwa kutumia case law, sio kwa maneno ya mdomo..ila naomba iyo kesi kama unayo niisome. ni kweli vicarious liability inaweza kumfanya mwajiri au superior kuwa na responsibility za subordinate/mwajiriwa kama huyo subordinate/mwajiriwa alisababisha matatizo bishaniwa katika mazingira ya utendaji kazi...akiwa ana deliver duties zake. siwezi kupinga hili kwasababu umekuja na case law, cha muhimu tungepata iyo case (mimi sina) na ningependa niisome..pia ni vigumu kwetu kufikia conlusion kwasababu ushahidi woote uliopo ni ule tu tunaouona jf, kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari, ambavyo kila mtu ana testify kulingana na feelings zake. ...ajabu yake, kama kweli hao watu watakamatwa na kufunguliwa murder, ....utakuja ushangae sana kuona maelezo ya folio C (mashahidi, kwa wale ma prosecutor wataelewa nini folio c) yameeleza tofauti kabisa na vile tulivyoona na kusikia kwenye vyombo vya habari. Polisi wanaweza kupindisha kabisa..kwani anayeandika maelezo ya ushahidi ni nani? si polisi? nani asiyewajua polisi kwa kupindisha? wanakuwa wawili tu kwenye chumba cha upelelezi pale polisi kutoa maelezo anaweza kumwambia "sema hivi"au aka mu induce kwa namna yeyote, ndio maana ni vigumu kufikia conclusion hiyo...kwasababu you never know what the police are planning about it....

  uchunguzi ukikamilika wale jamaa wakakamatwa, itabidi wake ma folio D (accused), na itabidi polisi watafute mashahidi na waandike maelezo, yale maelezo watakayoandika mashahidi ndio pekee yatakayotumika kum lead witness kwenye prosecution. kwahiyo, tusubiri kushangaa kile kitakachotokea wakati wa uendeshaji wa kesi,....ila Mungu pekee ndiye hakimu wa kweli katika maisha ya duniani.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
 17. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nigeshauri mabero marando hamtetee huyu mama
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hapana, Mwangosi ameuwawa na polisi waliokuwa ndani ya uniform wakifanya kazi yao kipolisi kwa mujibu wa sheria, kwa hiyo walikuwa wakifanya kazi kwa niaba ya serikali, na hivyo serikali inahusika moja kwa moja. Angeuwawa na polisi mitaani kwa sababu zao binafsi ndipo hoja yako ingekuwa sahihi.
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Hivi vile vitisho vyako vya kumfungulia mashitaka spika wa zamani wa bunge bw. Pius Msekwa viliishia wapi?

  Wengine tulijua ni mikwara ya kwenye mitandao tu.....au unasemaje?
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nilishafungua kesi hiyo na jambo hilo sasa hivi linashughulikiwa na Nebraska District Court. Kwa kwa sasa hivi siwezi kuongelea zaidi jambo ambalo bado liko mahakamani.
   
Loading...