Je enyi wadada wa kibongo mwaweza hii!!

Je enyi wadada wa kibongo mwaweza hii!!

Ningaliwapa ufafanuzi bahati mbaya hapa sio jukwaa husika...
Ila kama Imani yenu ndio hiyo basi na muendelee kuamini hivyo...

MKUU hiyo sio mpya hicho ni kipimo tosha
wanawake wanashida sana ya kutaka kuolewa
ila basi tu

Wala sio mpya kama unavyodhani ni kawaida tu..ndoa ya mke mmoja ni matunda ya kutekwa kwa imani ya kikristo na utamaduni wa wazungu kubana matumizi..unakumbuka ya Taurati na Zaburi si bible pia? Lakini mitume kama Suleiman, Daudi, Ayubu walikuwa na wake zaidi ya mmoja lakini hakukua na sheria za sasa za uzunguni katika agano jipya..nampa pongezi huyo bwana kwa kutukuza AGANO...
 
Wengi huwa wanaandika vile wanavyojisikia kwa kuwa kiuhalisia hatuwafahamu...wala usikate tamaa ukaamini haya watu waandikayo

Namuombea sana binti angu Beata yani wanaume jamani, comment zenu zinanivunja mifupa. Namuombea ampate mwenye unafuu!
 
1 Wakorintho 7:2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Wala sio mpya kama unavyodhani ni kawaida tu..ndoa ya mke mmoja ni matunda ya kutekwa kwa imani ya kikristo na utamaduni wa wazungu kubana matumizi..unakumbuka ya Taurati na Zaburi si bible pia? Lakini mitume kama Suleiman, Daudi, Ayubu walikuwa na wake zaidi ya mmoja lakini hakukua na sheria za sasa za uzunguni katika agano jipya..nampa pongezi huyo bwana kwa kutukuza AGANO...
 
JAMAA AFUNGISHWA NDOA YA WAKE WATATU

Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.

FELA Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti, amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba wanaweza kuoa wanawake wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.

mmmmh!wanawake wana shida na kiu ya kuolewa lakini hiyo mpya kwangu.
 
Last edited by a moderator:
Sio neno la Mungu bhana Everlenk bali la Wazungu wa Agano jipya!! Mambo wameyafanya mitume wa zamani hayo..wanaendeleza utamaduni wa kweli wa Kiimani!!
Si wazungu kwani hata wazungu wana mila zao na tamaduni zao za kuoa wake wengi,mpango wa Mungu ni kila mtu anywe maji ya birika lake mwenyewe na wala ashirikiane na mgeni hiyo nI ktk Agano la kale soma hii Mithali 5:15-18.
 
1 Wakorintho 7:2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
Je hilo ni agano jipya au lili la Kale yakasemwa hayo na Wakorintho??? Kama ni jipya bado hoja yangu ipo pale pale pamoja mimi ni mkristo lakini agano jipya limechakachuliwa mno na tamaduni za kizungu...
 
kajitahidi kubalansisha.... mwembamba, size ya kati, bonge....
hapo nje watamsikia kwa jirani tu

Kweli nakubaliana na wewe jamaa akitaka nene anapata, akitaka nyembamba anapata na akitaka ya kati vile vile ipo!!
 
JF pazuri lol!
wapo watu wa kila aina!! nashukuru kwa ujumbe eeeh!!
ungeniwekea na vifunngu vyake ningeenda kukesha leo kusoma biblia

Si mpango wa Mungu bali ni tamaa za mwanadamu tu ndo maana Mungu akawaacha waende kwa kufuata tamaa zao za mwili,ukitaka kujua si mpango wa Mungu ndio maana Mungu alimuumba mwanamme mmoja na mwanamke mmoja akawabariki wakazae waijaze dunia na kuthibitisha hilo wakati wa Nuhu alimwambia kwmb aingie yy na familia yake na aingize kila kiumbe cha kiume na kike tu yaan viwili viwili tu,Na Yesu akaja akathibitisha hilo ktk agano jipya kmwb kila mtu mme na awe na mke wake mwenyewe na alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe mpka kifo,na waweza achana kwasababu ya uzinzi tu ndo waweza oa au olewa lkn si vinginevyo.
 
mbona wote kama aina moja tu! hakuna cheupe hyakuna extra fat, hakuna black ya ukweli, hakuna twembamba twakutosha, sura za kawaida zote umri wote sawa, ndo maana wenzie tunachukua kwa awamu ukiwa umesha soma mapungufu! huyu bado haja solve tatizo tutagongana nae mtaa tu!

Hahahaaa.... Semaga weyee..!!
 
kasoro rangi tu ndio kachemsha kwani wote hao ni ma black angechanganya na ka white kidogo ingekuwa poa zaidi
Mbona una usemea moyo, kama ana allergy na ka white.
 
katimiza ahadi ya kiduni na wala si ya mbinguni kaongeza matatizo kabla ya kupunguza
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni wapi vile walipoonesha mtu aoe mke mmoja?

Soma hapa;
1 Wakorintho 7:2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
 
Basi endelea kuamini uaminivyo...ikiwezekana nawe uandike bible yako.
Ngoja tuheshimu jukwaa husika kuwa si sehemu ya kujadili haya tunayojadili.

Back
Top Bottom