SoC02 Je, Elimu inaendana na dira ya taifa?

Stories of Change - 2022 Competition

Changer 22

Member
Jul 29, 2022
11
5
Utangulizi.

images.jpeg

Zaidi ya miaka 50 Tanzania imekuwa ikipiga hatua katika kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu iliyo Bora.Baada ya Tanganyika kupata Uhuru mwaka 1961 serikali ilianza kutengeneza mazingira ya kuwasaidia wananchi kutokomeza changamoto kuu tatu zilizokuwa zinalikabili TAIFA ambazo ni maradhi, Ujinga na Umasikini. Katika kutokomeza Ujinga serikali iliamua kuwapelekea vijana katika shule zilizokuwa chini ya madhehebu ya kidini kiwepo kanisa katoliki. Huku vijana wengine wakipelekwa kwenye shule za mwanzo ikiwepo Tanga technical, Lyamungo, Tosaganga, Minaki, Mzumbe na Iyunga zilizopo katika mikoa mbali mbali ya Tanganyika na Tanzania baada ya kuungana na Zanzibar na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Je! Elimu inayotolewa inaendana na DIRA ya TAIFA..?

download.jpeg

Mabadiliko makubwa yamekuwa yakifanyika katika uboreshaji wa utoaji wa elimu kuanzia mitaala ya elimu, mfumo wa utoaji wa elimu pamoja na uboreshaji wa mazingira ya elimu hiyo. Hii inaambatana na Ujenzi wa madarasa, vyuo vya kati na vyuo vikuu pamoja na mikopo kwa wanachuo ambayo inawawezesha kujikimu katika masomo Yao.

Lakini Bado swali linabaki kuwa Je elimu inayotolewa inaendana na DIRA ya TAIFA.
Bado Kuna changamoto hasa katika uandaaji wa mitaala ya elimu hasa Lugha inayotumika, vitendea kazi pamoja na kuhimiza matumia ya elimu ya vitendo zaidi ya kuendelea kutumia elimu ya nadharia ambayo hupoteza uhalisia wa ndoto za mwanafunzi Moja kwa moja.

Bado serikali inahitajika kuangalia ufanisi wa utoaji wa elimu lakini pia kuingiza DIRA ya TAIFA katika mfumo wa elimu ambapo hii itawezesha uandaaji wa wakufunzi na wahitimu ambao watapata nafasi ya kazi zitakazolisaidia TAIFA kufikia malengo yaliyopo kwenye DIRA ya TAIFA.

Umuhimu wa elimu inayoendana na DIRA ya TAIFA..
Kuna umuhimu mkubwa wa Serikali kutengeneza mazingira ya elimu ambayo yanaenda na DIRA ya TAIFA kwani hili litachangia kuongezeka kwa wataalamu ambao watawezesha kufikia DIRA ya TAIFA,kila mwaka Wanafunzi wengi wanamaliza vyuo huku wengine wanadahili katika vyuo mbalimbali bila kujua DIRA ya TAIFA inaelekea wapi.

Pengine hii ndio sababu kubwa kwa kuwa na wahitimu wengi wasio na kazi kwani wengi wanaenda kusoma vitu ambavyo kipaumbele chake kimeshapitwa na wakati. Ni Bora sasa TAIFA likae na wataalamu wabobezi katika nyanja ambazo serikali imejikita kama DIRA ya taifa na kuanza kutengeneza mazingira ya uandaaji wa mitaala na kuweka kipaumbele kwenye utoaji wa elimu itakayo wezesha serikali kufikia malengo na DIRA iliyojiwekea.
 
Back
Top Bottom