Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Wengi wamekuwa wanajiuliza kuwa Dk. Wilbroad Slaa ni nani? Na anataka au anaweza kuifanyia nini Tanzania. Wanajiuliza kama ni nani na ni nini kinachomsukuma Dk. SLAA kutaka apewe mamlaka ya kuiongoza Tanzania.

Dk. SLAA ni Mtanzania, muumini na Daktari wa Falsafa katika masuala ya dini yake ya Ukristo dhehebu la Katoliki. Alikuwa Kasisi au bado ni Kasisi kwa maana ya Sakramenti isiyofutika, lakini aliasi wakati akiwa Katibu wa Baraza la Maaskofu, nafasi kubwa sana katika kanisa hilo lenye waumini wengi.

Haifahamiki kama alikorofisha nini, ingawa kuna madai kwamba alifanya ufisadi kwenye fedha za kanisa. Inafahamika kwamba alipoondoka kwenye uongozi wa kanisa alioa kama ishara ya kusema sasa ukasisi basi, lakini kanisa lilikataa kubariki ndoa yake kwa maana ile ile kwamba sakramenti hizo hazitolewi mara mbili kwa mtu mmoja.

Asingeweza kupata Sakramenti ya Ndoa baada ya kupata Sakramenti ya Ukasisi. Hakujali akaendelea na shughuli zake na sasa anatarajia kuwa Kasisi wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania kama kura zitatosha ifikapo Octoba 31, mwaka huu.

Katika kitabu anachokitumia Dk. SLAA kwa sala, ambacho ni Biblia, yapo maelezo katika Timotheo sura ya tatu mstari wa kwanza hadi wa tano (Tim.3:1-5) kwamba: “Ni neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya uaskofu; atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole, si mtu wa kujadiliana wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kusimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu, yaani mtu asiyejua kuisimimia nyumba yake mwenyewe, atalisimamiaje kanisa la Mungu”.

Mchanganuo wa aya hiyo hapo juu unatoa picha tofauti za namna ya kumwelewa Dk. SLAA kama mtu anayetafuta nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania. Kwa upande mmoja, hata kama zipo sababu nyingine zilizomwondoa katika nafasi ya Ukatibu wa Baraza la Maaskofu, kuhusishwa kwake na ufisadi wa fedha za misaada kulimwondolea sifa ya kuwa kiongozi kanisa la Mungu, Analaumika.

Naamini hajajitoa kwenye Ukristo bado ni Mkatoliki na zipo taarifa ambazo zimeshaandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba kanisa linamuunga mkono katika harakati zake za kutaka uongozi wa juu wa nchi.

Kanisa limeshakanusha kwamba halimuungi mkono kwa sababu Tanzania haina dini na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakisisitiza kwamba Chama chao kisihusishwe na dini kwa maelezo kwamba uongozi wake ni wa watu wa dini zote na hata pengine wale wasio na dini.

Pamoja na ukweli kwamba viongozi waanzilishi wa CHADEMA ni wakristo, kanisa halingeweza kuonyesha kwamba linamuunga mkono, lakini ni vyema ikakubalika kwamba kwa miaka yote kanisa limekuwa likiamini kwamba dini ya mfalme wako ndio dini yako.

Hata kama Dk. SLAA aliukataa Ukasisi na akaonekana muovu mbele ya macho ya uongozi wa kanisa, lakini kwa sasa anaonekana ni mali kwa kuwa jiwe lililokataliwa na wajenzi wote, sasa limekuwa jiwe la msingi wa nyumba. Ukorofi wa Dk. SLAA kwa kanisa wa kuivuruga Sakramenti ya Ukasisi utavumiliwa na haitashangaza kama hata ndoa yake ikabarikiwa na kanisa endapo atafanikiwa kuupata Urais.

Ushahidi wa hali kama hiyo upo. PASTEUR BIZIMUNGU, hakuwa na ndoa na SERAFIN hadi alipoteuliwa kuwa Rais wa Rwanda wakati RPF inaingia madarakani mwaka 1994. Kanisa ndilo lililomtaka afunge ndoa kabla ya kuapishwa kuwa Rais. Kanisa linachotaka ni Dk. SLAA kuwa Rais wa Tanzania. Waraka wa kanisa uliotolewa na Baraza la Maaskofu tarehe 2 Julai, 2010, ulikuwa ni ishara tosha ya kuwajulisha Wakristo kwa ujumla kwamba wana mtu wao na bila shaka ni Dk. SLAA.

Kasisi/Padre anayejiondoa kwenye huduma zake za Kipadre huchukuliwa na kanisa kama mwana mpotevu (Prodigal Son) au kondoo aliyepotea, ambaye wakati wowote anaweza kurudi kundini. Kwa kuwa kazi mojawapo ya kanisa ni kuwatafuta na kuwarudisha kundini kondoo waliopotea, kanisa halijakata tamaa kuhusu uwezekano wa Dk. SLAA kurudia wito wake wa upadre.

Kwa kuzingatia dhamira yake kama mpakwa mafuta (the anointed) si jambo la ajabu ikiwa Dk. SLAA atarudi kwenye utume wake kama padre na kuiacha nchi “solemba”. Hata asiporudia upadre wake, upo uwezekano wa mchungaji huyo, akisukumwa na sauti ya wito wake wa upadre kuiongoza nchi kwa maslahi ya kanisa ambalo limemlea na kuchora moyoni mwake alama ya upadre isiyofutika (indelible mark) kama Kanisa Katoliki linavyoamini.

Wapo baadhi ya Watanzania watakaokumbuka kwamba mara baada ya uhuru wa Zimbabwe kupatikana mwaka 1980, Waziri Mkuu ROBERT MUGABE hakukubaliana na pendekezo la Rais CANAAN BANANA kwamba nchi hiyo iwe ya kikristo. Hakuna uhakika kama hilo haliwezi kutokea Tanzania ikiwa Dk. SLAA atafanikiwa kuwa Rais.

Taarifa ambazo ni vigumu kuzithibitisha na ambazo si vyema kuzipuuza zinaonyesha kwamba baadhi ya maaskofu wamekuwa wakikutana na uongozi wa Chadema kujadili hoja ya uongozi wa kitaifa na suala la uras mwaka 2015. Maoni ni kwamba hata kama urais hautapatikana mwaka 2010, angalau washinde na kuhakikisha kwamba Chadema kinakuwa chama kikuu cha upinzani bungeni ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa urais mwaka 2015.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba ili kufanikisha dhana ya CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni ni vyema MBOWE arudi jimboni kugombea na DK. SLAA agombee Urais hata kama hatafanikiwa, lakini atakuwa kivutio kikubwa cha kuwashawishi wananchi kuchagua Wabunge wengi wa chama hicho.

Mikakati ya kanisa imekuwa haimshirikishi ZITTO KABWE kwa sababu yeye anahofiwa kwamba ama yupo karibu na CCM au anatumia elimu yake kujijenga ili agombee Urais mwaka 2015.

Dk. SLAA alisita sana kuchukua fomu za chama chake kukubali kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yamkini watu walio wengi walikuwa wanamuuliza ni kwa nini anafanya hivyo, lakini wajuzi wa mambo walitambua kwamba Dk. SLAA alikuwa anasita kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuamini kwamba alishafikishwa mahali pabaya ambapo pande zote mbili na kila upande ukiwa na dhamira yake ulikuwa unataka kumtumia. MBOWE alitaka kumtumia kukijenga Chama na Kanisa kujiimarisha.

Kwa upande mwingine, Dk. SLAA alipokuwa anajiunga na CHADEMA baada ya kuenguliwa CCM alifanya hivyo kwa kuamini kwamba angejijengea wasifu mpya, lakini hakujua kwamba anaingia kwenye Chama cha kifamilia kinachoendeshwa kwa gwanda la kikabila na kuongozwa na MBOWE ambaye naye anatajwa kuwa si msafi sana.

DK. SLAA amekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi hususan ndani ya serikali. Katika vita hivyo, Dk. SLAA amekuwa akisema kwamba serikali ya CCM haiwezi kupiga vita rushwa kwa sababau yenyewe imekuwa ikiendesha ufisadi tangu ilipoingia madarakani enzi za TANU. Kwa hoja hii, Dk. SLAA anaonyesha kwamba sio mkweli labda lengo lake ni kuichafua CCM ili ashinde katika uchaguzi huu.
Lakini hata kama hiyo ndiyo dhamira yake, atakuwa anafanya makosa makubwa akijaribu kupuuza juhudi za serikali ya awamu ya nne chini ya Rais KIKWETE katika kupambana na rushwa na ufisadi. Ni mapema mno Dk. SLAA kusahau juhudi za Muasisi wa Taifa hili Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE na Waziri Mkuu MORINGE SOKOINE katika mapambano yao dhidi ya rushwa na wahujumu uchumi.

Kuna wasiwasi kwamba Dk. SLAA amegombea Urais kupitia kwenye chama ambacho hana madaraka na uwezo wa kukemea maovu ya ndani. Hana maelezo ya wazi kwamba ni kwa nini alikubaliana na ukaidi wa MBOWE alipon’gan’gania kwamba ni yeye pekee asimame kama mgombea wa Uenyekiti wa chama hicho na kumlazimisha ZITTO KABWE aondoe jina lake.

Matumizi ya ovyo ya fedha za CHADEMA ni ugonjwa ambao Dk. SLAA ameshindwa kuupatia dawa ingawa anafahamu kwamba ndio uliosababisha kuleta hali ya kutoelewana kati ya MBOWE na aliyekuwa mbunge wa Tarime CHACHA WANGWE ( sasa marehemu).

Ameshindwa kuyavunja makundi mawili ndani ya CHADEMA; kundi moja likiongozwa na Naibu Katibu Mkuu ZITTO KABWE na kundi lingine likiongozwa na Mwenyekiti FREEMAN MBOWE. Makundi yote haya mawili yanaelezewa kwamba kila moja linataka Urais mwaka 2015. Moja ya athari inayotokana na mivutano ya makundi haya ni kushindikana mara tatu kuteua Wabunge wa viti maalum. Hali hiyo ilitokea baada ya wagombea wanaomuunga mkono FREEMAN MBOWE kushindwa isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtoto wa PHILEMON NDESAMBURO aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini.

Wote wanaoomunga mkono ZITTO walishinda na hali hiyo ilikuwa inaonekana kuwa tishio kwa Mwenyekiti Mbowe, ambaye alitamka kwamba mkutano huo ni batili. Haifahamiki kama wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA watateuliwa lini, lakini swali la msingi na lisilo na jibu ni kwamba kwa nini DK. SLAA amekaa kimya kwenye kadhia hii. DK. SLAA anawashawishi Watanzania waanze kuamini kwamba hata wakimpa mdaraka ya kuiongoza dola ya Tanzania, atakuwa na tabia ya kuuzia masuala ya kitaifa kwa sababu hajiamini. Watanzania wanatakiwa kufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi.

Source: Gazeti la Raia mwema Agosti 25 – Agosti 31, 2010
 
Yawezekana kabisa ni kweli kabisa uyasemayo lakini ukweli unabaki palepale kwamba lengo na nia ya Slaa ni kuleta mabadiliko katika siasa za Tanzania ili mtu wa kawaida na wa chini afaidike na raslimali tulizopewa na Mwenyezi Mungu. Kinachokataliwa na wengi si Ukatoliki wala Uislam wa kiongozi wetu, bali tunataka kiongozi jasiri anayeweza kukemea uporaji wa mali zetu na kutuacha tulio wengi tukiwa watazamaji tu na mashabiki tukiiangalia nchi ikiliwa na wachache.
Kinachoudhi ni kuona viongozi wetu wanaongoza utadhani hawajasoma na kuelimika hata kidogo; hawawezi kupambanua kipi chema kwa watu wetu na kipi hakina faida kabisa.
Slaa ameleta chachu mpya katika mchakato wa urais Tanzania na CCM wanajua hilo. Yupo Lipumba, Mziray na utitiri wao lakini hakuna hata anayewazungumzia kwa sababu hawana chochote kipya; hawana ajenda yoyote ya maana. Lakini Slaa anayo na hilo ndilo linalowatisha watu kama wewe na wenzako msiopenda kuona ukweli kwamba nchi hii inaliwa ovyo na tutabakia omba omba kwa muda mrefu otherwise tufanye mageuzi. Na Slaa anatoa fursa hiyo
 
ahasante raia mwema.......tunaomba wasifu wa mgombea mwenza wa chadema....maana hatumjui.....elimu yake.. Hofu yetu hana elimu kama katiba inavotaka
 
Weka pingamizi dhidi yake ili wewe ndio uonekane kilaza
 
Wengi wamekuwa wanajiuliza kuwa Dk. Wilbroad Slaa ni nani? Na anataka au anaweza kuifanyia nini Tanzania. Wanajiuliza kama ni nani na ni nini kinachomsukuma Dk. SLAA kutaka apewe mamlaka ya kuiongoza Tanzania.

Dk. SLAA ni Mtanzania, muumini na Daktari wa Falsafa katika masuala ya dini yake ya Ukristo dhehebu la Katoliki. Alikuwa Kasisi au bado ni Kasisi kwa maana ya Sakramenti isiyofutika, lakini aliasi wakati akiwa Katibu wa Baraza la Maaskofu, nafasi kubwa sana katika kanisa hilo lenye waumini wengi.

Haifahamiki kama alikorofisha nini, ingawa kuna madai kwamba alifanya ufisadi kwenye fedha za kanisa. Inafahamika kwamba alipoondoka kwenye uongozi wa kanisa alioa kama ishara ya kusema sasa ukasisi basi, lakini kanisa lilikataa kubariki ndoa yake kwa maana ile ile kwamba sakramenti hizo hazitolewi mara mbili kwa mtu mmoja.

Asingeweza kupata Sakramenti ya Ndoa baada ya kupata Sakramenti ya Ukasisi. Hakujali akaendelea na shughuli zake na sasa anatarajia kuwa Kasisi wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania kama kura zitatosha ifikapo Octoba 31, mwaka huu.

Katika kitabu anachokitumia Dk. SLAA kwa sala, ambacho ni Biblia, yapo maelezo katika Timotheo sura ya tatu mstari wa kwanza hadi wa tano (Tim.3:1-5) kwamba: "Ni neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya uaskofu; atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole, si mtu wa kujadiliana wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kusimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu, yaani mtu asiyejua kuisimimia nyumba yake mwenyewe, atalisimamiaje kanisa la Mungu".

Mchanganuo wa aya hiyo hapo juu unatoa picha tofauti za namna ya kumwelewa Dk. SLAA kama mtu anayetafuta nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania. Kwa upande mmoja, hata kama zipo sababu nyingine zilizomwondoa katika nafasi ya Ukatibu wa Baraza la Maaskofu, kuhusishwa kwake na ufisadi wa fedha za misaada kulimwondolea sifa ya kuwa kiongozi kanisa la Mungu, Analaumika.

Naamini hajajitoa kwenye Ukristo bado ni Mkatoliki na zipo taarifa ambazo zimeshaandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba kanisa linamuunga mkono katika harakati zake za kutaka uongozi wa juu wa nchi.

Kanisa limeshakanusha kwamba halimuungi mkono kwa sababu Tanzania haina dini na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakisisitiza kwamba Chama chao kisihusishwe na dini kwa maelezo kwamba uongozi wake ni wa watu wa dini zote na hata pengine wale wasio na dini.

Pamoja na ukweli kwamba viongozi waanzilishi wa CHADEMA ni wakristo, kanisa halingeweza kuonyesha kwamba linamuunga mkono, lakini ni vyema ikakubalika kwamba kwa miaka yote kanisa limekuwa likiamini kwamba dini ya mfalme wako ndio dini yako.

Hata kama Dk. SLAA aliukataa Ukasisi na akaonekana muovu mbele ya macho ya uongozi wa kanisa, lakini kwa sasa anaonekana ni mali kwa kuwa jiwe lililokataliwa na wajenzi wote, sasa limekuwa jiwe la msingi wa nyumba. Ukorofi wa Dk. SLAA kwa kanisa wa kuivuruga Sakramenti ya Ukasisi utavumiliwa na haitashangaza kama hata ndoa yake ikabarikiwa na kanisa endapo atafanikiwa kuupata Urais.

Ushahidi wa hali kama hiyo upo. PASTEUR BIZIMUNGU, hakuwa na ndoa na SERAFIN hadi alipoteuliwa kuwa Rais wa Rwanda wakati RPF inaingia madarakani mwaka 1994. Kanisa ndilo lililomtaka afunge ndoa kabla ya kuapishwa kuwa Rais. Kanisa linachotaka ni Dk. SLAA kuwa Rais wa Tanzania. Waraka wa kanisa uliotolewa na Baraza la Maaskofu tarehe 2 Julai, 2010, ulikuwa ni ishara tosha ya kuwajulisha Wakristo kwa ujumla kwamba wana mtu wao na bila shaka ni Dk. SLAA.

Kasisi/Padre anayejiondoa kwenye huduma zake za Kipadre huchukuliwa na kanisa kama mwana mpotevu (Prodigal Son) au kondoo aliyepotea, ambaye wakati wowote anaweza kurudi kundini. Kwa kuwa kazi mojawapo ya kanisa ni kuwatafuta na kuwarudisha kundini kondoo waliopotea, kanisa halijakata tamaa kuhusu uwezekano wa Dk. SLAA kurudia wito wake wa upadre.

Kwa kuzingatia dhamira yake kama mpakwa mafuta (the anointed) si jambo la ajabu ikiwa Dk. SLAA atarudi kwenye utume wake kama padre na kuiacha nchi "solemba". Hata asiporudia upadre wake, upo uwezekano wa mchungaji huyo, akisukumwa na sauti ya wito wake wa upadre kuiongoza nchi kwa maslahi ya kanisa ambalo limemlea na kuchora moyoni mwake alama ya upadre isiyofutika (indelible mark) kama Kanisa Katoliki linavyoamini.

Wapo baadhi ya Watanzania watakaokumbuka kwamba mara baada ya uhuru wa Zimbabwe kupatikana mwaka 1980, Waziri Mkuu ROBERT MUGABE hakukubaliana na pendekezo la Rais CANAAN BANANA kwamba nchi hiyo iwe ya kikristo. Hakuna uhakika kama hilo haliwezi kutokea Tanzania ikiwa Dk. SLAA atafanikiwa kuwa Rais.

Taarifa ambazo ni vigumu kuzithibitisha na ambazo si vyema kuzipuuza zinaonyesha kwamba baadhi ya maaskofu wamekuwa wakikutana na uongozi wa Chadema kujadili hoja ya uongozi wa kitaifa na suala la uras mwaka 2015. Maoni ni kwamba hata kama urais hautapatikana mwaka 2010, angalau washinde na kuhakikisha kwamba Chadema kinakuwa chama kikuu cha upinzani bungeni ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa urais mwaka 2015.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba ili kufanikisha dhana ya CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni ni vyema MBOWE arudi jimboni kugombea na DK. SLAA agombee Urais hata kama hatafanikiwa, lakini atakuwa kivutio kikubwa cha kuwashawishi wananchi kuchagua Wabunge wengi wa chama hicho.

Mikakati ya kanisa imekuwa haimshirikishi ZITTO KABWE kwa sababu yeye anahofiwa kwamba ama yupo karibu na CCM au anatumia elimu yake kujijenga ili agombee Urais mwaka 2015.

Dk. SLAA alisita sana kuchukua fomu za chama chake kukubali kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yamkini watu walio wengi walikuwa wanamuuliza ni kwa nini anafanya hivyo, lakini wajuzi wa mambo walitambua kwamba Dk. SLAA alikuwa anasita kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuamini kwamba alishafikishwa mahali pabaya ambapo pande zote mbili na kila upande ukiwa na dhamira yake ulikuwa unataka kumtumia. MBOWE alitaka kumtumia kukijenga Chama na Kanisa kujiimarisha.

Kwa upande mwingine, Dk. SLAA alipokuwa anajiunga na CHADEMA baada ya kuenguliwa CCM alifanya hivyo kwa kuamini kwamba angejijengea wasifu mpya, lakini hakujua kwamba anaingia kwenye Chama cha kifamilia kinachoendeshwa kwa gwanda la kikabila na kuongozwa na MBOWE ambaye naye anatajwa kuwa si msafi sana.

DK. SLAA amekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi hususan ndani ya serikali. Katika vita hivyo, Dk. SLAA amekuwa akisema kwamba serikali ya CCM haiwezi kupiga vita rushwa kwa sababau yenyewe imekuwa ikiendesha ufisadi tangu ilipoingia madarakani enzi za TANU. Kwa hoja hii, Dk. SLAA anaonyesha kwamba sio mkweli labda lengo lake ni kuichafua CCM ili ashinde katika uchaguzi huu.
Lakini hata kama hiyo ndiyo dhamira yake, atakuwa anafanya makosa makubwa akijaribu kupuuza juhudi za serikali ya awamu ya nne chini ya Rais KIKWETE katika kupambana na rushwa na ufisadi. Ni mapema mno Dk. SLAA kusahau juhudi za Muasisi wa Taifa hili Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE na Waziri Mkuu MORINGE SOKOINE katika mapambano yao dhidi ya rushwa na wahujumu uchumi.

Kuna wasiwasi kwamba Dk. SLAA amegombea Urais kupitia kwenye chama ambacho hana madaraka na uwezo wa kukemea maovu ya ndani. Hana maelezo ya wazi kwamba ni kwa nini alikubaliana na ukaidi wa MBOWE alipon'gan'gania kwamba ni yeye pekee asimame kama mgombea wa Uenyekiti wa chama hicho na kumlazimisha ZITTO KABWE aondoe jina lake.

Matumizi ya ovyo ya fedha za CHADEMA ni ugonjwa ambao Dk. SLAA ameshindwa kuupatia dawa ingawa anafahamu kwamba ndio uliosababisha kuleta hali ya kutoelewana kati ya MBOWE na aliyekuwa mbunge wa Tarime CHACHA WANGWE ( sasa marehemu).

Ameshindwa kuyavunja makundi mawili ndani ya CHADEMA; kundi moja likiongozwa na Naibu Katibu Mkuu ZITTO KABWE na kundi lingine likiongozwa na Mwenyekiti FREEMAN MBOWE. Makundi yote haya mawili yanaelezewa kwamba kila moja linataka Urais mwaka 2015. Moja ya athari inayotokana na mivutano ya makundi haya ni kushindikana mara tatu kuteua Wabunge wa viti maalum. Hali hiyo ilitokea baada ya wagombea wanaomuunga mkono FREEMAN MBOWE kushindwa isipokuwa mmoja tu ambaye ni mtoto wa PHILEMON NDESAMBURO aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini.

Wote wanaoomunga mkono ZITTO walishinda na hali hiyo ilikuwa inaonekana kuwa tishio kwa Mwenyekiti Mbowe, ambaye alitamka kwamba mkutano huo ni batili. Haifahamiki kama wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA watateuliwa lini, lakini swali la msingi na lisilo na jibu ni kwamba kwa nini DK. SLAA amekaa kimya kwenye kadhia hii. DK. SLAA anawashawishi Watanzania waanze kuamini kwamba hata wakimpa mdaraka ya kuiongoza dola ya Tanzania, atakuwa na tabia ya kuuzia masuala ya kitaifa kwa sababu hajiamini. Watanzania wanatakiwa kufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi.

Source: Gazeti la Raia mwema Agosti 25 – Agosti 31, 2010
Tunaomba utuwekee na makala ya wiki hii "Dr SLAA ASEMA NCHI INALIPUKA"
-MWAKA 2010 HATUDANGANYIKI TENA--
 
..kama makala hii imetoka kwenye gazeti la RAIA MWEMA basi tumekwisha.

..mwandishi wa makala anajikanyaga-kanyaga kiasi hicho na mhariri bado anaruhusu iwe published.

..hii makala imejaa udini, na kitu cha kutisha zaidi ni kwamba imetolewa kwenye gazeti la mtu anayeheshimiwa sana na jamii ya wa-Tanzania, Jenerali Ulimwengu.
 
Slaa ni mtoto wa nyerere hana jipya :huyu ni ccm , akipata madaraka tutarudi zile enzi za nyerere kukaa foleni ya sigara . Hivi karibuni aliutembelea mzimu wa nyerere kule dodoma . Huyu mtu ni hatari sana .
 
Siamini kama mhariri wa raia mwema anaweza kuruhusu upupu huu kuandikwa na gazeti makini kama hilo! Isijekuwa Rostam kesha nunua na raia mwema.
 
Pamoja na yote yaliosemwa lakini mimi bado na imani kubwa na dk slaa, tokea aliposimama bungeni nakuomba mishara ya wabunge ipunguzwe kwani mikubwa mno kulingana na wananchi wa kawawaida. Kitendo kile kimenifanya nione huyu kweli yupo pale kwa ajili ya wananchi na sikitu kingine,kwa hiyo hata akipewa nchi me poa tu!
 
-kama zile hadithi nilizozoea za hapo zamani za kale....
-umwkubali kutumika kisiasa na ccm na umekubali kutumika kidini na kikwete na uislamu..................pole sana
-unazungumzia sokoine na nyerere wakati tunamzungumzia rais dhaifu kabisa kuwahi kutokea yaani kikwete
-mpaka sasa huamini kuwa kikwete aliweka dini ya kiislamu mbele kwa kuweka mambo ya mahakama ya kadhi kwenye ilani ya ccm na kuitetea, hili ni suala la wazi
-kuna swala ambalo halijawahi kujificha na wala kukanushwa na waislamu baada ya ule moto na fukuto waliloonesha juu ya kuondoia mambo yao ya kipuuzi ya oic na mahakama ya kadhi waliposema hawatampiogia kura kikwete na ccm lakini aliwaita wazee ambao wanasambaza habari kwa usiri mkubwa baada ya kuwaahidi kutumia mamlaka atakayokuwa nyo kwa namna yoyote kufanya hiyo mahakama ya kikafiri iwepo kikatiba....
-wanasubiri tu kikwete achaguliwe maana ndivyo walivyoambiwa wasubiri kwani mambo mazuri hayataki haraka kwa mujibu wa kikwete
-mwandishi anajaribu kutumia mgongo wa kuwa alikuwa padre...hiyo ni kitu tofauti ila kwa kikwete ameonesha kwa vitendo...rais wa nchi huwezi kukaa kimya katiba ya nchi inachezewa na wajinga eti kuweka mambo ya dini...ndiyo maana waasisi wa taifa hili baada ya kuwa na mtazamo wa mbali waliamua kuondoa upumbavu huo maana mtu kama mimi siko tayari kodi yangu itumike kumlipa kafiri mshahara eti kwa kuwa mahakama ya kadhi...
-slaa na wakristo kwa ujumla ni watu wa kutafuta amani kwanza hata akichaguliwa kwanza hawezi kuruhusu bunge kuamua kupoteza muda kujadili upuuzi wa kadhi na kuacha mambo ya msingi ya kuwainua watu kiuchumi naamimini hatakaa kimya kwani ni upumbavu kujadili na kupoteza mudfs ikiwemo kuwapa posho wabunge kwa kujadili mambo ya dini
-NAAMINI TUMEELEWANA
 
Wakati huu tutasikia na kuona mengi! Kwa makala hii inanifanya nianze kuwa na mtazamo tofauti na nilivyomdhania Jenerali Ulimwengu! Hofu mojawapo ya mwandishi ni eti nchi itatawaliwa na kanisa kana kwamba hii ni mara ya kwanza kuchagua Rais Mkristo! Cha ajabu zaidi nii pale Rais mwema wanaposhindwa kutofautisha taasisi na mtu binafsi. Urais ni taasisi inayoongozwa na katiba na sheria, Unachokisema wewe ni kama kwamba Dr Slaa atasimama barabarani na rungu kubwa kuwawinda wasitii mamlaka ya kanisa!
Tunacholilia Tanzania ni kujenga demokrasia ya kuwakataa wote wababaishaji, Wala watz sio marobott ya kugeuzwa geuzwa kwa remote Dr Slaa atapimwa kwa mizani ile ile iliyompimia Kikwete na ikiwa haenendi sawa sawa tutamtapika pia!
Mwanzoni wa utawala wa kikwete Cartoon moja ilionekana kwenye magazeti ya Kenya waandishi wa Tz wanamlamba miguu Mhe! Leo hii hakuna kitu kitu kama hicho labda wachache wanaojipendekeza kama Raia mwema na magazeti ya serikali. Why? Kwa sababu mwanaume hasifiwi kwa sura!
 
Nasubiria kuona mods wakifanya kazi yao na kuhamisha hii thread kwenda kwenye jukwaa la dini

count down inaendelea wakati na mimi nikiandaa thread yangu inayofanana na hii
 
Hii makala inashangaza sana! Utadhani Slaa ataongoza nchi kwa misingi ya Kanisa Katoliki. Kwani nchi haina katiba? Haina sheria? Kwa nini tumwogope mtu kwa sababu ya dini yake? Hii mada imejaa: Slaa na ukatoliki wake. Jamani tuache ubaguzi wa kidini. Kama mtu anafaa kutuongoza basi tumkubali bila kuangalia imani yake. Hii makala inapotosha sana ukweli.
 
jenerali ulimwengu wote tunajua yaliyompata huko siku za nyuma kwa hiyo kutafuta hifadhi kwa nguvu zilezile kama za akina mrema...yaani baada ya kufulia wanaanzakutafuta nafasi kama za akina salva mweyemamu....................MTU MWENYEWE SIO RAIA...niambieni jenerali ulimwenguu majina gani hayo hapa kwetu
PAKA SHUME WAMEANZA KAZI ZAO NA WANADANDIA TRENI KWA MBELE...................
ILA NINA WASIWASI NA ROSTAMU AZIZI KUANZKULINUNUA GAZETI HILI KAMA ILIVYOTOKEA KWA GAZETI LA RAI...JAMANI NJAA HIZI ZITATUUA KWANI TUTAANZA KUWAANDAMA WATU WENGINE HASA WAPUUZI KAMA HAWA NA AMBAO SIO RAIA NA KUZAA NAO KWA UJINGA KAMA HUU...............VYEO OMBENI TU KIKWETE AMEAHIDI YALE MAKAPI YOTE AMBAYO HAYAWEZI KUSIMAMA PEKE YAO YATAPEWA UKUU WA WILAYA/MIKOA/UKURUGENZI NA VIVYEO VINGINE VYA KUWAGAWIA MASWAHIBA...................
NYAMBAFUUUUU......
 
Hii makala inaonekana kuandikwa na kada wa CCM. Mambo ya udini na ukampuni wa familia ya Mtei wa CHADEMA ni propaganda ambazo CCM wangependa zipandikizwe kwenye fikra za wapiga kura. No wonder mwandishi hakuthubutu hata kuweka jina lake.
 
jenerali ulimwengu wote tunajua yaliyompata huko siku za nyuma kwa hiyo kutafuta hifadhi kwa nguvu zilezile kama za akina mrema...yaani baada ya kufulia wanaanzakutafuta nafasi kama za akina salva mweyemamu....................MTU MWENYEWE SIO RAIA...niambieni jenerali ulimwenguu majina gani hayo hapa kwetu
PAKA SHUME WAMEANZA KAZI ZAO NA WANADANDIA TRENI KWA MBELE...................
ILA NINA WASIWASI NA ROSTAMU AZIZI KUANZKULINUNUA GAZETI HILI KAMA ILIVYOTOKEA KWA GAZETI LA RAI...JAMANI NJAA HIZI ZITATUUA KWANI TUTAANZA KUWAANDAMA WATU WENGINE HASA WAPUUZI KAMA HAWA NA AMBAO SIO RAIA NA KUZAA NAO KWA UJINGA KAMA HUU...............VYEO OMBENI TU KIKWETE AMEAHIDI YALE MAKAPI YOTE AMBAYO HAYAWEZI KUSIMAMA PEKE YAO YATAPEWA UKUU WA WILAYA/MIKOA/UKURUGENZI NA VIVYEO VINGINE VYA KUWAGAWIA MASWAHIBA...................
NYAMBAFUUUUU......

Mkuu Jile,

Mimi bado sina hakika kama Ulimwengu ameruhusu hii kitu itokee kwenye gazeti lake. Ndio maana watu wengine hapo juu bado wanauliza kama kweli hii kitu imetokea raia mwema (na if so, imekuwaje editor mkuu akaruhusu itokee).
 
Mwafrika,
Inawezekana Jenerali ameacha ichapishwe kwa sababu ni maoni ya mwandishi.(column) Haikuandikwa kama news item. Lakini kosa walilofanya ni kuondoa jina la mwandishi na kutoonyesha kuwa ni op-ed (opinionated editorial which it is) I would have done the same but would have made sure my readers understand this is an op-ed.
 
Slaa ni mtoto wa nyerere hana jipya :huyu ni ccm , akipata madaraka tutarudi zile enzi za nyerere kukaa foleni ya sigara . Hivi karibuni aliutembelea mzimu wa nyerere kule dodoma . Huyu mtu ni hatari sana .
Woga wote wa nini? Lazima utapike ulichoiba weeee dawa yako ikimbie nchi mapema na usijulikane umekwenda wapi maana tutakufuata hata huko.
Mzimu wa Nyerere aufuate wa nini? wakati kila siku yuko Dodoma?
 
Aliyeandika nukuu makala umeacha hii kitu mwishoni "mwandishi wa maoni haya amejitambulisha kama "Chovenge Kipunde" ambaye anasema ni msomaji wa muda mrefu wa raia mwema. Tumeyachapisha maoni haya kwa sababu,pamoja na mambo mengine ndani ya toleo hili kuna mahojiano maalumu ya dk. Wilbroad slaa ambayo mengine yanagusia maoni ya msomaji wetu, kwa mawasiliano naye muandikie katika Kchovenye@yahoo.com

haya maelezo mtoa mada hakupaswa kuyaacha kwani yanatoa pia msimamo wa raia mwema juu ya makala hiyo. All in all majibu yapo kwenye mahojiano yake. Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom