Je, Dkt. Abdallah Possi na Dkt. Ally Possi ni ndugu? Nimevutiwa nao...

Kwa wenye akili tumeshaenda mbali zaidi na kujua hasa ' Kiini ' cha huu ' Uzi ' wako ambapo unachotaka kusema hapa japo unazunguka zunguka tu ni kwamba Watu wawili ambao pia ni Ndugu wa damu kabisa wamepewa ' Wadhifa ' Serikalini hivyo unaonekana hujapenda na ' Wivu ' umekujaa.

Kwa kukusaidia tu ni kwamba hao wote ni Ndugu na huyo Ally Kwao ndiyo ' the last born '. Kitu cha kufurahisha tu ni kwamba katika Familia yao hakuna ambaye hana ' Doctorate Degree / PhD ' kwani hata Wazazi wao nao ni ' PhD ' Holders halafu pia Familia yao ni ya mambo safi tupu.
Ushaambiwa kwamba baba yao hana PhD mama yao ndio anayo pamoja na hao wengine sidhani kama huo ndo ulikua mtazamo wa mleta mada bali yeye ameona kushahibiana majina sasa mtu apate wivu kivipi maana hao watu kama ni elimu kweli wanayo na imeshiba vizuri
 
Professor Mwajabu alinifundisha course ya special needs education, sijui PE ngapi nishasahau, alikuwa akiwatolea sana mifano wanawe hawa ktk lecture zake. Alinuia kusoma course za special needs kwa sababu ya wanae hawa walokuwa na mahitaji maalum
 
Habari wakuu,​
View attachment 746281
Dr. Abdallah Possi(Kushoto) na Dr. Ally Possi(Kulia)
Jana Rais Magufuli alifanya teuzi mbalimbali, moja ya teuzi ilikuwa ya Dr. Ally Possi ambaye ni Albino. Katika akili za haraka haraka bila kutuliwa nikajua ndo yule Possi ambaye ni Balozi huko Ujerumani. Kwanini nilijua hivyo! Ni kwamba, Kwanza Albinism, Jina la Possi na Elimu isiyoacha shaka ya uzamivu(PhD).​

Leo katika pitapita nikiendelea kudadisi nikagundua kwamba ni watu wawili tofauti. Huyu akiitwa Ally na yule akiitwa Abdallah na wote wakitumia ubin wa Possi. Mmoja ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na mwingine ni Balozi wa Tanzania nchini ujerumani.

Basi hapo shaka yangu ikawa imeisha. Nilichovutiwa kuanzisha hapa uzi ni kutaka kujua kama hawa wasomi wenye wasifu usioacha shaka ni ndugu.

Pia wamechapisha > Abdallah Possi & Ally Possi ‘The identity question versus appropriateness of legal anti - discrimination measures: Endorsing the disability rights approach to albinism ’ (2017) 5 African Disability Rights Yearbook 118 - 140

Ingia hapa kusoma wasifu wa Dr. Ally Possi > Ally Possi

Ingia hapa kusoma wasifu wa Dr. Abdalla Possi > Abdallah Possi

UPDATE: Baada ya kusoma maoni ya wanaJF nimekutana na bandiko kuhusu mama yao. Soma >Prof. Mwajabu Possi wa UDSM aula TBC

Asanteni.
ni ndugu baba mmoja na mama mmoha ni watoto wa prof mwajabu pissi
 
Professor Mwajabu alinifundisha course ya special needs education, sijui PE ngapi nishasahau, alikuwa akiwatolea sana mifano wanawe hawa ktk lecture zake. Alinuia kusoma course za special needs kwa sababu ya wanae hawa walokuwa na mahitaji maalum
EP siyo PE
 
Sio mapacha ila ni mtu na kaka yake. Yule balozi ndio Mkubwa.
Mama yao na baba yao ni Maprofesa wapo UDSM japo ni wazee. Wamekuwa exposed tangu kale.
Walipelekww kusoma nje na wote ni PHD holder
Baba si Profesa ila mama ni Profesa UDSM. Vijana walitambua umuhimu wa shule mapema. Dkt. Ally alisomeshwa na pesa ya wazazi LLM (UCT) baadae akapata scholarships UP kusoma LLD. Tupeleke watoto shule
 
Huyo mdogo wake anaitwa nan na yuko mwaka wa ngap? Maana cna hakika na unachokisema!!

Wewe kiazi kweli.....


Soma nilichoandika.

Nimesema yuo Udom ni Mwl... Alisoma Law unauliza yuko mwaka wa ngapi.
 
Wakat Prof. Possi anapeleka wanae university za maana, wengine wanaishia kunywa bia, kuhonga na kuchangia harusi. Na kushinda instagram
 
Sio mapacha ila ni mtu na kaka yake. Yule balozi ndio Mkubwa.
Mama yao na baba yao ni Maprofesa wapo UDSM japo ni wazee. Wamekuwa exposed tangu kale.
Walipelekww kusoma nje na wote ni PHD holder
Nikusahihishe kidogo, uko sahihi kwa baadhi ya mambo isipokuwa ambaye ni profesa Udsm ni mama yao tu. Baba yao ni mtu wa kawaida, mfanyakazi wa reli zamani.
 
Hawa ni ndugu mkuu
Ally Possi ni class mate wangu Makongo High school way back 2000 tukiwa o-level
Abdala alitangulia nadhan ni advance inteck ya kwanza makongo
 
Mama ndio prof Udsm kitivo cha uhandishi wa habari na Yupo bodi YA TBC... Baba Yao Ana elimu YA kawaida degree labda na master..... Wamesoma elimu YA awali hapa TZ hadi dree YA kwanza wote wawili hapa TZ UDSm. Kaka yake master na PhD alichukulia German na ndipo Yupo balozi.... Mdogo wake wakili Ali master na PhD amechukulia south Africa.... baba, mama na dada Yao ni weusi kwa ngozi Ila wenyewe ndio wana albinism kiumri Bado ni vijana wadogo nilipoamia tabata abdala alikuwa high school Ila mdogo wake Ali ndio nilikuwa nimemzidi darasa moja kijana wa makongo enzi za kipingu huyu..... Wapo vizuri Sana wanaishi maisha YA kawaida Sana.....
Kumbe tupo wengi mkuu vijana wa kipingu
Shift one au 2
Nilikiluwa 4A4 2000
 
Hii mada inampa chachu mtu mwenye wivu kwa watoto wake.
....
Ninachokiona.
Njia uli/unayopitia inatoa taswira kwa wanaokufuata kama vile wanao.
 
Wakat Prof. Possi anapeleka wanae university za maana, wengine wanaishia kunywa bia, kuhonga na kuchangia harusi. Na kushinda instagram
Ally Possi alipelekwa University of Cape Town kwa ufadhili wa wazazi wake. Tofauti na mwenzangu na mie unachangia kwa sifa harusi za ndugu na majiran mamilioni ila wajao hawapati hata milo mitatu
 
Back
Top Bottom