University of Dar es salaam, Je mmeitelekeza SMJC?

N'yadikwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
4,829
2,000
SJMC kwa wasiokijua ni Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Shule hii zamani ilijulikana kama TSJ - Tanzania School of Journalism na baadae ilipopewa kwa UDSM ikaitwa IJMC yaani Institute of Journalism and Mass Communication na kisha UDSM ktk utaratibu wao wa kubadilisha majina ya Faculties IJMC ikawa moja miongoni mwa Schools za UDSM yenyewe ikijikita kufundisha, kushauri na kutafiti masuala ya Uandishi wa Habari, Mawasiliano kwa Umma na Public Relations hapa nchini. Miongoni mwa watu mashuhuri waliosoma katika Shule hii ni Hayati Reginald Mengi, Harrison Mwakyembe, japo kuwataja kwa uchache.

Wakati SJMC ikijulikana kama IJMC ilikuwa chini ya Uongozi wa Profesa Mwajabu Possi ambae ni mama yake na akina Dkt Abdallah Possi huyu balozi wetu wa Ujerumani na yule wakili Possi alietusaidia kuikomboa ndege yetu Afrika Kusini hivi majuzi. Huyu mama ni nguli, guru na gwiji katika kuboresha hii shule. Baada yake akaja wakati huo DKT Benadetha Killian ambae sasa ni Profesa na Mkuu wa DUCE(kama sijakosea). Hawa viongozi wawili walikuwa na mipango madhubuti ya kuushauri utawala wa UDSM kukiboresha SJMC kuwa miongoni mwa taasisi muhimu sana na yenye miundombinu mizuri ya kujifunzia waandishi wa habari.

KINACHOSIKITISHA SASA KUHUSU SMJC

  1. SJMC kina miundombinu chakavu kutajwa, majengo ni makukuu sana na hata ukifika hapo chuoni hautapata picha ya haraka kwamba hapa wanafunzwa waandishi wa habari ambao Taifa linawategemea!!. Ajabu ni kwamba UDSM kwa miaka zaidi ya 8 sasa tangu chuo kibadilishe mifumo yake miundombinu ya SJMC bado hairidhishi. Wakati huo wa 2010-11 kulikuwa na mpango wa kujenga jengo jipya pale ili lisaidie madarasa, studio za kujifunzia na ofisi za magazeti lakini hadi leo hakuna lililofanyika.
  2. Miundombinu ya kujifunzia kwa vitendo ni hoi. Ikumbukwe kwamba uandishi wa habari unataka mazoezi kwa vitendo kila wakati, lakini vyombo vya habari vya SJMC/UDSM kwa sasa ni chokest, redio Mlimani hata ukiwa Magomeni Mapipa tu hapo kuipata ni shida studio zake ni choka. Vivyohivyo Mlimani TV hoi bin taaban hadi wafanyakazi wake wa muda wameamua kutimkia tbc 1 imebaki hoi kabisa. Picha hazitazamiki, sidhani kwenye mazingira kama haya wanafunzi watapata maarifa stahiki ya uandishi wa habari.
  3. Staff: Kwa sasa taasisi hii ina uhaba wa walimu hasa wa mafunzo kwa vitendo. Wanafunzi wanaweza kutestfy
  4. Chuo hakina hata Canteen ya maana wala ukumbi wa mikutano, kweli? Photo lab ni almost haipo maana inayotumika ni ya mwaka 70 huko ya kuloweka films!
  5. Ofisi za Gazeti la mafunzo ya vitendo hakuna, na gazeti lenyewe ni kama limeshajifia hivi Hill Observer.
  6. Maktaba haina resource za kutosha.
NB: VC tuma timu yako ikafanye ukaguzi pale wakuletee ripoti utagundua SJMC kimechoka na kinahitaji structural, administrative and institutional intevention!!

Sasa wito wangu kwako Profesa Anangisye, ni wakati sasa kupeleka nguvu kwenye chuo hiki ili waandishi wa habari wanaozalishwa na UDSM wawe na sifa na viwango vile vinavostahiki. Kwa mazingira yale ya SJMC ndugu Profesa hatuwezi kujenga waandishi competent, nguvu iliyotumika kuimarisha na kuboresha Ukuta unaoendelea kujengwa surrounding the main Campus upande wa Ubungo, nguvu inayoboresha UDBS, nguvu inayoboresha Maktaba Mpya, nguvu inayoboresha COICT,n guvu inayoboresha Constituencies MUCE/DUCE basi ielekezwe pia kwenye Shule ya Uandishi wa Habari SJMC.

SJMC ina historia ndefu lakini siku za karibuni kimekuwa kama chuo kilichotelekezwa! UDSM Utawala elekezeni nguvu sasa kukiboresha SJMC mmekitelekeza inatosha.Taifa linahitaji waandishi wa Habari competent lakini hawawezi kuwa nurtured kwenye mazingira kama yale ya SJMC.

#udsmutawalarevampsjmc#

by mdau!
 
No retreat no surrender

No retreat no surrender

JF-Expert Member
1,898
2,000
SJMC/IJMC ndo ile iliyopo karibu na Bamaga?
 
N'yadikwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
4,829
2,000
Dah...kweli wafanye renovation ya majengo na intervention zingine. Enzi za chuo tulikuwa tunaenda kule kufokafoka na kuimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitaleta picha...zaidi vifaa vya kujifunzia kwa vitendo hakuna pale hata ukipita tu unakutana na taasisi iliyokunja sura kwa uchakavu wa majengo na miundombinu mingine
 

Forum statistics


Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom