Chief David Makwaia na Dkt. WBK Mwanjisi katika wasifu wa Julius Nyerere

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,853
30,196
CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA NA DR. WBK MWANJISI KATIKA WASIFU WA JULIUS NYERERE
Siku moja rafiki yangu Edward Makwaia tulikuwa tunasoma darasa moja St. Joseph’s Convent School Dar es Salaam aliniambia nimsindikize kwenda kwa baba yake ambae alikuwa amekuja kutoka Nairobi.

Basi nikamsimdikiza na ndiyo ikawa mara yangu ya kwanza kukutana na Chief David Kidaha Makwaia wa Siha.

Edward Makwaia ndiyo chief hivi sasa.

Toka udogo wangu nimekuwa napenda sana kuvaa vizuri na mama yangu akinisifia akiniambia, ‘’Mwanangu Mohamed Mashaallah una maji ya nguo.’’

Maana ya kuwa na ‘’maji ya nguo,’’ ni kupendeza katika mavazi.

Nilipokuwa sasa mkubwa akinambia, ‘’Nikikuvisha nguo yako uipendayo kutwa nzima uko wima hukai chini unaogopa kuchafua lebasi.’’

Kiswahili hiki hakisikiki siku hizi wazee wameondoka kwenda akhera na Kiswahili chao.

Ninachokikumbuka kwa Chief Kidaha siku ile ni jinsi alivyokuwa amevaa shati na suruali tu lakini zimemkaa vyema.

Siku moja nazungumza na mama yangu Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy mke wa Abdul Sykes.

Kwa sauti ya kawaida tu akaniambia, ‘’Unajua mwanangu Mohamed kuwa Bwana Abdul yeye alimtaka Chief Kidaha awe President wa TAA waunde TANU na Chief Kidaha ndiyo aongoze harakati za kudai uhuru?’’

Kwangu mimi Mama Daisy alikuwa kaniangushia bomu.

Tulikuwa tumekaa nyumbani kwake ‘’sitting room,’’ Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Akili yangu imefunguka kote nasikiliza.

Mama Daisy akaendelea, ‘’Chief Kidaha alikuwa kila akija kuhudhuria vikao vya LEGCO Bwana Abdul atamwalika kuja kula chakula cha jioni nyumbani pale Stanley na mimi nikisikiliza mazungumzo yao.

''Bwana Abdul mara kadhaa akimwambia, ‘’David hebu hebu waache hao Waingereza njoo huku tukuchague kuwa President tuuende TANU tudai nchi yetu.’’

Akisema, ‘’huku,’’ Abdul Sykes alikuwa anakusudia TAA.
Hii ilikuwa kati ya mwaka wa 1951 – 1952.

Lakini aliyotamani Abdul Sykes kwa rafiki yake Cheif Kidaha Allah hakuyajaalia kwa kuwa kiti cha uongozi wa Tanganyika alikuwa kamwandikia Julius Nyerere.

Historia ya uhuru wa Tanganyika ilipokuja kuandikwa si Chief Kidaha wala Abdul Sykes walitajwa au hata kukumbukwa ndani ya historia hiyo.

Lakini zito kwa Chief Kidaha ni kuwa baada ya uhuru alikumbwa na misukosuko mingi sana hadi akahama nchi.

Nimemkuta Chief Kidaha katika Wasifu wa Julius Nyerere.

Hakuna mengi yaliyoelezwa kuhusu yeye.
Nani huyu David Kidaha Makwaia?

David Kidaha Makwaia ni mtoto wa Chief Makwaia Mohamed Mwandwi (1905 – 1945) na babu yake Chief Mohamed Mwandwi ndiye aliyeuingiza Uislam Usukumani kwa kuwaleta walimu kutoka Zanzibar kuja kusomesha dini.

Chief Kidaha alikuwa ‘’chief katika machifu,’’ kwa mfano wa Chief Abdallah Said Fundikira, Thomas Marealle na Adam Sapi Mkwawa.

Nimekutana na Chief Kidaha Makwaia katika Nyaraka za Sykes kupitia kalamu ya Dr. Wilbard Mwanjisi akimsifia Chief Kidaha kwa mchango wake ndani ya LEGCO pale alipowaambia Waingereza wafikirie upya kuwaruhusu wafanyakazi wa serikali Waafrika kujihusisha na siasa.

Hili jambo lilikuwa nyeti sana kwa Waingereza na hapa ndipo alipokamata Dr. Mwanjisi na kulisherehesha kirefu katika makala aliyoandika kama President wa Tanganyika African Governments Servant Association (TAGSA) akikusudia yachapwe katika jarida la TAGSA.

Rashid Kawawa aliyekuwa katika Halmashauri Kuu ya TAGSA alipinga vikali kuchapwa kwa makala haya.

Haya ya siasa madogo katika makala yale aliwaita Waingereza ‘’hawajastaarabika,’’ kwa kudhani akili zinauhusiano na rangi ya ngozi ya mtu.

Hili lilikuwa tusi dhahiri kabisa dhidi ya serikali. Katibu wa TAGSA alikuwa Ally Sykes.

Baadae baada ya kumjua vizuri nilitambua kuwa Dr. Mwanjisi na Ally Sykes walikuwa baba mmoja mama mmoja si watu wa kuwaachia jambo peke yao watakugharisheni nyote, yaani watakuzamisheni wao na nyie pamoja.

Sikupata kujua hisia za Waingereza kwa Chief Kidaha kutokana na maneno yale ndani ya LEGCO.

Hii ilikuwa mwaka wa 1951.

Lakini baada ya makala ile halmashauri karibu yote ya TAGSA ilipigwa uhamisho kupelekwa majimboni mbali na Dar es Salaam.

Ninachotaka kueleza ni kuwa Dk. Mwanjisi katajwa katika Wasifu wa Julius Nyerere kama alivyotajwa Chief Kidaha Makwaia, wamepitiwa juujuu na kitabu kikaendelea na mengine.

Kinachowaunganisha hawa watu wawili, Chief Kidaha na Dr. Mwanjisi ni kuwa wote baada ya uhuru walikimbia nchi kwenda kuishi na kufanyakazi Kenya.

Baada ya kitabu cha Abdul Sykes kuchapwa mdogo wake wake Dr. Mwanjisi Roland alikwenda kwa Ally Sykes na karatasi kama tatu hvi zinazoeleza historia fupi ya msuguano baina ya marehemu kaka yake Dr. Mwanjisi na Mwalimu Nyerere uliomfanya kaka yake akimbie nchi.

Ilikuwa kama vile Roland anamcheka na kumwambia Ally Sykes, ‘’Kiko wapi?’’

Roland bila shaka kafanya haya kwa makusudi akijua kuwa Ally Sykes na kaka yake Abdul walikuwa marafiki-ndugu na Nyerere na siku zile ulikuwa huwezi kumgusa Nyerere wakakuacha.

Sheikh Suleiman Takadir yalimkuta.

Niliwaeleza waandishi wa Wasifu wa Julius Nyerere historia hii ya Dr. Mwanjisi na zile karatasi za Roland walipokuja kufanya mazungmzo na mimi na nilihisi kama walivutiwanayo na kwa hakika ipo katika kitabu.

Historia hii ni nzuri kufahamika ila inataka na Mwalimu na yeye aeleze upande wake jambo ambalo mimi sikuwa na uwezonalo kwa hiyo limebaki katika Maktaba yangu.

Hawa akina Mwanjisi ukisoma historia zao utakuta kuwa walikuwa ‘’left of the left,’’ katika TANU staili ya Zuberi Mtemvu, Steven Mhando na Sheikh Suleiman Takadir wakiona Nyerere anaharibu na kuvuruga mambo.

Zaidi pia hawa akina Mwanjisi juu ya kujaliwa uwezo mkubwa wa akili walikuwa na ‘’hot blood,’’ hasira zao ziko jirani sana hawana simile kiasi ambacho hawakuweza kuwiva na Nyerere kwa lolote.

Hamza Mwapachu Waingereza si tu walikuwa wakimjua ni ‘’leftist,’’ lakini wakiamini ni Mkomunisti hasa lakini juu ya pengine kugongana na Nyerere katika mitizamo hawakupata kugombana kabisa kila mtu alifanya staha kwa mwenzake.

Mwapachu alikuwa na ''Das Kapital,'' Karl Marx toleo la 1924.

Mtemvu toka mwaka wa 1958 baada ya Kura Tatu alimwekea shonde Nyerere hakuzungumzanae hadi anaingia kaburini mwaka wa 1998.

Abdul Sykes kwa ule utu wake na subra aliyokuwanayo hakugombana na Nyerere na siku chache kabla hajafa alimtembelea Nyerere nyumbani kwake Msasani kaongozana na bint yake Aisha, Daisy kama anavyofahamika.

Ally Sykes kwa miaka mingi hakusema na Nyerere.

Kipande hiki kinahitaji makala yenye kujitegemea In Shaa Alla siku ikipatikana fursa nitaeleza historia hii ya hawa wapigania uhuru wawili ambao kadi zao za TANU zinaongozana no. 1 Julius Nyerere na no. 2 Ally Sykes ambao pia mama zao Bi. Mruguru bint Mussa na Bi. Mugaya Nyang’ombe walikuwa mashoga wakubwa wakati watoto wao wanapambana na Mwingereza katika miaka ya 1950.

Wasifu wa Julius Nyerere una mengi na utafaidi kusoma kitabu hiki ikiwa kwa kiasi fulani unaijua historia ya Mwalimu Nyerere na washirika wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika mfano wa Sykes brothers - Abdulwahid na Ally na Mwanjisi brothers - Wilbard na Roland.

Kitu kimoja nihitimishe.

Roland alimwambia Ally Sykes aniambie kuwa kaka yake jina lake ni Wilbard Mwanjisi si William Mwanjisi.

Kwa bahati mbaya katika wasifu Dr. Mwanjisi kaandikwa kwa makosa ‘’William,’’ kwa waandishi kufuata vile mimi nilivyomtaja katika kitabu cha Abdul Sykes lakini nakumbuka kama vile wakati nawaeleza kisa cha Dr. Mwanjisi na Nyerere niliwaeleza kosa hili la jina lakini wakapitiwa.

Tatizo ni kuwa Dr. Mwanjisi maisha yake yote akiandika jina lake WBK Mwanjisi ikanijia baada ya kusoma mtu wa kuniambia jina lake nikahisi kuwa hii ‘’W’’ itakuwa ‘’William,’’ kumbe nimekosea na nimesababisha walimu wangu wakosee.

PICHA:
Chief Makwaia Mohamed Mwandwi, Chief David Kidaha Makwaia, Ally Sykes na Julius Nyerere, Bi. Mruguru bin Mussa na Bi. Mugaya Nyang'ombe.

CHIEF MAKWAIA MOHAMED MWANDU.png

Chief Makwaia Mohamed Mwandwi

CHIEF KIDAHA.jpg

Chief David Kidaha Makwaia

ALLY SYKES NA JULIUS NYERERE.jpeg

Ally Sykes na Julius Nyerere

MRUGURU BINT MUSSA.jpg
MUGAYA NYANG'OMBE.jpg

Bi. Mruguru bin Mussa na Bi, Mugaya Nyang'ombe
 
Ahsante kwa Historia hii tamu ya nchi yetu .
Mzee Mohamed, Una mpango wa kuandika Kitabu kinachokuhusu wewe na vingi ulivuinavyo juu ya historia ya Taifa hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Mohamed Said!

Samahani, Naomba nikuulize maswali mawili matatu.

Ally Sykes na Abdul Sykes ni nani mkubwa na wanaitanaje hao ndugu?

Kati yao "Sykes" ni yupi ana mjukuu au uzao unatokana na msanii Dully Sykes?

Kwenye vitabu vya zamani vya Uraia, Siasa, na Historia kama kile cha, "Tanzania kabla na baada ya uhuru" toleo la 1971 leo hakipo katika mtaala wa elimu lakini hawa mashujaa Abdulwahid, Ally na Abdul Sykes kuna mahali wametajwa katika kitabu hicho.

Nimekuwa nikiyaona majina yao kwenye vitabu vya zamani ila niliibiwa vitabu kadhaa na vingine nilipoteza, ukiazimisha kitabu unadhulumiwa au unaambiwa kile uliniazima kimepotea au kimeibiwa.
 
Je, Huyu Chifu David Kidaha Makwaia ni mwenyeji na mzaliwa wa wapi?

Je, Kuna uhusiano wowote kati ya Chifu David Kidaha Makwaia na Chifu Abdallah Makwaia?
 
..Chifu David Kidaha Makwaia alizaliwa May 7,1922 na kufariki March 31, 2007.

..Baba yake David alikuwa ni Chifu Makwaia Mohamedi Mwandu alizaliwa mwaka 1905 na kufariki mwaka 1945.

..maana yake ni kwamba Makwaia alimzaa David akiwa na miaka 17 tu.
 
View attachment 1447446
Chief Makwaia Mohamed Mwandwi

View attachment 1447447
Chief David Kidaha Makwaia

View attachment 1447448
Ally Sykes na Julius Nyerere

View attachment 1447449View attachment 1447450
Bi. Mruguru bin Mussa na Bi, Mugaya Nyang'ombe
Huu upotoshaji mkubwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu, Mohamed Said!

Samahani, Naomba nikuulize maswali mawili matatu.

Ally Sykes na Abdul Sykes ni nani mkubwa na wanaitanaje hao ndugu?

Kati yao "Sykes" ni yupi ana mjukuu au uzao unatokana na msanii Dully Sykes?

Kwenye vitabu vya zamani vya Uraia, Siasa, na Historia kama kile cha, "Tanzania kabla na baada ya uhuru" toleo la 1971 leo hakipo katika mtaala wa elimu lakini hawa mashujaa Abdulwahid, Ally na Abdul Sykes kuna mahali wametajwa katika kitabu hicho.

Nimekuwa nikiyaona majina yao kwenye vitabu vya zamani ila niliibiwa vitabu kadhaa na vingine nilipoteza, ukiazimisha kitabu unadhulumiwa au unaambiwa kile uliniazima kimepotea au kimeibiwa.
Reg...
Walizaliwa hivi Abdulwahid, Ally na Abbas.
Dully ni mjukuu wa Abdul Sykes.
 
Back
Top Bottom