Je, China imeiwekea Kenya mtego wa madeni?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
VCG111218918157.jpeg
Wakati uchaguzi mkuu wa Kenya unakaribia, baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi vinadai kuwa, China imeiwekea Kenya “mtego wa madeni”.

Nyuma ya madai hayo, madhumuni halisi ya baadhi ya nchi za Magharibi ni kuchafua ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Kenya, na pia kujaribu kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya. Je, China imeiwekea Kenya “mtego wa madeni”? Bila shaka jibu ni hapana!

Kwanza, China si mkopeshaji mkuu wa Kenya. Vyombo vya habari vya Magharibi vinaitaja China kama mkopeshaji mkuu wa Kenya, jambo ambalo ni tofauti na ukweli. Takwimu zinaonesha kuwa madeni ya Kenya kwa China yanachukua asilimia 10 tu ya madeni yote ya umma ya Kenya, na kihalisia, madeni mengi zaidi ya Kenya na nchi nyingine za Afrika yanatoka nchi za Magharibi.

Kwa kulingana na takwimu za mwaka 2022 zilizotolewa na Benki ya Dunia, karibu robo tatu za madeni ya nchi za Afrika zinatoka nchi za Magharibi.

Pili, mikopo na uwekezaji wa China kwa Kenya vimejikita zaidi katika nyanja za maendeleo haswa miundombinu, na kuisaidia Kenya kuongeza uwezo wake wa kujiendeleza, na mikopo na uwekezaji wa China vitaisaidia Kenya kuinua uwezo wa kulipa madeni ya nje kupitia maendeleo. Wakati huohuo, madeni mengi ya nchi za Magharibi kwa Kenya yako katika maeneo yasiyo ya uzalishaji, na yametolewa pamoja na masharti makali ya kisiasa, kama vile haki za binadamu na mageuzi ya mambo ya kisiasa. Lengo kuu la nchi za Magharibi sio kukuza maendeleo ya uchumi wa Kenya, bali ni kuongeza ushawishi katika mambo ya kisiasa nchini Kenya.

Tatu, ushirikiano wa mikopo na uwekezaji kati ya China na Kenya siku zote umefuata kanuni za kibiashara, na uko wazi bila kufanywa kisiri. China haijawahi kuweka masharti yoyote ya kisiri kwenye mkataba wa mkopo, haijawahi kulazimisha Kenya kukopa pesa, na haijawahi kulazimisha Kenya kulipa madeni. Kutokana na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Kenya umeimarishwa siku baada ya siku. Katika miaka ya hivi karibuni, makampuni ya China yamejenga miradi mingi mikubwa ya miundombinu nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na Reli ya SGR, Reli ya Nairobi-Malaba, Bandari ya Lamu, na Barabara ya Nairobi Expressway. Katika bara nzima la Afrika, China imesaidia nchi za Afrika kujenga na kukarabati zaidi ya kilomita 10,000 za reli, karibu kilomita 100,000 za barabara kuu, karibu madaraja 1,000, na bandari 100. Hakuna nchi yoyote ya Afrika imeingia katika matatizo ya madeni kutokana na ushirikiano na China, pia hakuna nchi yoyote imelazimika kuweka rehani rasilimali za kimkakati kama vile bandari na migodi kwa China kutokana na kushindwa kulipa madeni.

Nyuma ya kauli inayodai kuwa China imeiwekea Kenya mtego wa madeni, ni hila ya baadhi ya nchi za magharibi kuipaka matope China, na kuharibu uhusiano wa kunufaishana kati ya China na Kenya. Lakini njama hizo kamwe haitafanikiwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom