Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 189
- 314
Kutokana na makubaliano hayo, kuanzia mwezi Mei, bidhaa muhimu za Kenya ikiwemo chai, kahawa, na parachichi zitaingia katika soko la China bila ya ushuru. Wakati huo huo, China itawekeza mabilioni ya dola kusaidia ujenzi wa miradi muhimu ya miundombinu nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa mtandao wake wa Reli ya SGR.
Makubaliano hayo yana maana muhimu kwa Kenya, kwani kwa muda mrefu, Kenya imekabiliwa na nakisi kubwa ya biashara na China. Kenya inaagiza takriban bidhaa zenye thamani ya dola zaidi ya bilioni 4 kila mwaka kutoka China, huku ikiuza bidhaa zake kwa China takriban dola milioni 200 tu. Utekelezaji wa makubaliano hayo mapya utaongeza kwa kiasi kikubwa mauzo ya bidhaa za Kenya kwa China, na kuifanya Kenya ijiunge zaidi na soko kubwa la China. Kama Rais wa Kenya William Ruto alivyosema, makubaliano hayo ya kibiashara yatatoa nguvu kubwa kwa uchumi wa Kenya.
Zaidi ya hayo, ujenzi wa reli ya SGR itakayounganisha Naivasha, Kisumu na Malaba utaimarisha zaidi mawasiliano ya barabara kati ya Kenya na nchi zisizo na bandari ikiwemo Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda, na hivyo kukuza muunganisho wa kiuchumi wa kikanda. Mradi huu wa reli wenye thamani ya dola bilioni 5.4 za kimarekani unatarajiwa kuwa hatua nyingine muhimu katika ushirikiano wa miundombinu kati ya China na Kenya, ukifuata reli ya SGR kati ya Nairobi na Mombasa.
Ushirikiano kati ya China na Kenya ni mfano mzuri wa ushirikiano unaozidi kuongezeka kati ya China na Afrika. Kuanzia Mei Mosi mwaka huu, China itatekeleza rasmi hatua za ushuru sifuri kwa nchi 53 ya Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo. Wakati wa Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani, Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao alisema wazi kwamba China inakusudia kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na Afrika, kuunga mkono mchakato wa viwanda wa bara hilo, na kutoa michango mikubwa zaidi katika kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya China na Afrika katika enzi mpya. Hatua hizo zinaonesha kwamba China inafuata kanuni za kufungua mlango na kutafuta manufaa ya pamoja, badala ya hesabu za kimaslahi kwa upande mmoja.
Ushirikiano kati ya China na Afrika umejengwa juu ya msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, na utaratibu huu wa ushirikiano unatambuliwa na kukubaliwa na nchi nyingi zaidi za Afrika