Je, CCM imebaki safi baada ya kuondoka Lowassa?

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,626
870
wakuu saalaamu

naomba wale wana ccm wanijuze je ccm imebaki safi baada ya kuondoka lowassa?? Yaani huko ccm mchafu alikuwa lowassa tu. Kama kweli alikuwa mchafu huyu tu mbona hawamfikishi mahakamani hadi leo kama kweli alilitia taifa hasara??/

katika ile list of shame ya dr. Slaa, aliwataja mafisadi papa 11 akiwemo jk na lowasa
sasa je lowasa kuondoka kwakwe ccm imebaki safi, hao 10 waliobaki wako wapi??

Hawa watu wako chama gani, wameshindwa kuchukua hatua stahili kuthibiti mambo mbalimbali,

1. Jk........ Richmond, epa, madawa ya kulevya, escrow..mikataba feki ya kichina, ya gesi na mafuta

2. Mkapa....... Uuzwaji holela wa viwanda zaidi ya 70 nchi nzima (ubinafsishaji), na kujimilikisha kiwira

3. Karamagi..... Kuusika na mikataba feki ya madini

4. Msabaha.....mikataba feki ya mafuta, gesi na wanyama pori

6. Chenge (nyoka wa makengeza)..... Mikataba lukuki feki inayolitafuna taifa

7, tibaijuka..... Vibari feki vya ardhi, ishu ya escrow, na ramani feki za kigamboni.

8. Madabida.......ishu ya arv feki

9. Magufuli...kudanganya bunge kwa bajeti feki ambayo haikutumika kujenga barabara (cag-ripoti), kuuza nyumba za serikali kwa vimada, na kufanya maamuzi ya sifa yaliyoligharimu taifa

10.ngereja... Mikataba ya feki ya madini

11.filemoni luhanjo......

12.wakurugenzi wengi wanaokula pesa za halmashauri.....................

Je ccm ni safi???
 
Wananchi tumechambua kilichobaki ni maamuzi sahihi. Mimi binafsi nitampigia LOWASA kwa sera mzuri ya elimu (elimu bure hadi chuo kikuu).

Pia kwa uamuzi wake wa kutoka chooni
 
Cc; Faiza Foxy, Big Show, Jingalao, Simiyu yetu, Eliza Boni (Lizaboni), Mr. Chini, Juliana wa Kufyonzwa, Mtela Mwampamba, Lumumba team (5000tsh FC) et al...
 
Mabadiliko ya kwanza ni kuiondoa sisiem kambi la wapiga deal,then miswada hovyo yote ivunjwe,bodi zinazosimamia maliasili zivunjwe,wanaosimamia viwanja vya ndege wastaafishwe wote,bandarini kusafishwe,nishati na madini kusafishwe,bunge lisimamiwe na majembe,walolipa taifa hasara wafilisiwe,na haya na mengoneyo yanayofanana na haya yatawezekana endapo tu sisiem itaondolewa
 
Shina na mizizi ya ufisadi imekomaa ndani ya ccm na imetambaa kila ofisi za umma na za binafsi.Dawa nikung'oa shina

na kulichoma moto kabisa
 
Yan alipokuwa ccm choo kilikuwa sebuleni lkn ukawa kimeamia bedroom tafakari

Think critically!!! Slaa kutoa mfano wa choo na mavi alimaanisha kuwa,choo ni chama,mavi ni mtu.so sisiem ndo choo mavi ni mafisadi walioko sisiem,sasa jiulize na kujijibu kimoyomoyo,hv yale mavi ya escrow,mabehewa feki,dawa za kulevya,kagoda,meremeta,kivuko kibovu,epa,utoroshwaji twiga,majangiri,ofisi ya spika urambo,dah na mengine mengi yameondoka humo chooni????'!!!
 
Ni kweli Lowasa ndiye chanzo cha ufisadi woote, mkuu naskia hata Escrow chanzo ni Lowasa, hata madawa ya kulevya chanzo ni Lowasa, licha ya kwamba JK anawajua wauza madawa ya kulevya woote, ila hawezi wachukulia hatua jiulize huyu kweli ni Raisi huyu?Hata mikataba feki 17 ya gesi na mafuta iliyo SIRI mpaka leo chanzo ni Lowasa....??
Ufisadi chanzo lowasa hakuna mjadala sindano imewaingia mtajibeba mwaka huu
 
Cc; Faiza Foxy, Big Show, Jingalao, Simiyu yetu, Eliza Boni (Lizaboni), Mr. Chini, Juliana wa Kufyonzwa, Mtela Mwampamba, Lumumba team (5000tsh FC) et al...

Hawawezi kujitokeza kujibu hizi hoja zaidi ya kupiga porojo tu, walidhani kumchafua Lowasa ni kujisafisha na ufisadi Lizaboni
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom