Tangu makada kadhaa wa CCM kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Edward Lowassa, Fredrick Sumaye, Msindai, Mgeja, Mungai, Masha, Onesmo Nangole na wengine wengi.
Wakati watu hawa wapo CCM, watanzania na vyama vya upinzani vilikua vinanena maneno yote machafu kwa chama cha mapinduzi.
Na nikupitia maneno hayo mabaya kutoka kwa Watanzania kilichofanya CCM itumue mamlaka yake kuwaengua makada wote wenye kashfa za wizi,ufisadi na ulanguzi kwenye mbio za kusaka kuteuliwa kupeperusha bendera ya ccm kugombea urais.
Baada ya kukatwa watu hao wawili (Lowasa na Sumaye) waliamua kukimbilia upinzani huku wakifuatwa na wanachama wa CCM wachafu kwelikweli, hadi hatua hii wanaccm wachafu wamekimbilia upinzani na hivyo kukiacha CCM kikiwa salama na hivyo kuwafanya upinzani kushindwa kuisemea agenda ya ufisadi kwani mgombea wao ukawa ndio baba na mwalimu wa ufisadi tanzania.
Kwa sasa niwaambie watanzania kuwa chama kilichobaki salama CCM ndicho cha kupewa nafasi wakalete maendeleo na mapinduzi ya kweli.