Je, Biblia inasema nini kuhusu chakula?

Je, Biblia inasema nini kuhusu chakula?

maforce

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2017
Posts
669
Reaction score
641
HAKUNA CHAKULA NAJISI.

Warumi 14:2,14,20

2 Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.

14 Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.

20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza.

Marko 7:18-19

18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;

19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.

Wakolosai 2:16

16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Waebrania 13:9

9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; Masharti hayo kamwe hayakumsaidia mtu yeyote aliyeyafuata.
 
ACHA KUTAFSIRI BIBLIA KIHOLELA HIVO, TABIA HII IMEPELEKEA MADHEHEBU MENGI NA UTITIRI WA MANABII NA MITUME WASIOHESABIKA HAPA DAR ,ACHANA NA WALE WA MIKOANI,

Biblia haikurupukiwi hivo, HASA MAANDIKO YA MTUME PAULO

Ikumbukwe kuwa vitabu vya Paulo viliandikwa kama barua na wakati mwingine ilikuwa ni katika kujibu hoja ambazo zilileta mkanganyiko kwa waumini maana Paulo alikuwa akihubiri na kisha kuondoka mahali hapo asirudi tena. Hivyo kama kulikuwa na jambo lolote lililohitaji ufafanuzi basi walimwandikia Paulo naye aliwaandikia kuwajibu ambapo nyaraka zake zilikusanywa na kuwekwa pamoja na leo tunazisoma kama maandiko yaliyovuviwa. Kwa bahati mbaya nyaraka zile ambazo waumini walimtumia Paulo hatunazo hivyo wakati mwingine inakuwa vigumu kujua ni kitu gani kilipelekea mitume kujibu hivyo walivyojibu.

Wengi kati ya wakristo wa awali ambao Paulo alikuwa akiwaandikia barua walikuwa ni wapagani waongofu na hivyo waliishi katika jamii ya kipagani, na sehemu kubwa ya jamii iliyowazunguka walikuwa ni wapagani.

Katika kipindi hicho kulikuwa na utaratibu kwamba nyama yoyote kabla ya kuuzwa ilikuwa sharti itolewe sadaka kwa sanamu. Jambo hili liliwapa shida kidogo baadhi ya wakristo kwamba huenda Mungu akawahesabia dhambi kwa kula nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu.

Ndipo Paulo sasa anawajibu na kuwaambia kuwa sanamu haineni na wala siyo kitu na mwenye imani anajua kuwa sanamu si kitu chochote na hivyo hula nyama pasipo kujali kwamba imetolewa sadaka kwa sanamu au la. Lakini yule mwenye imani haba huwa na mashaka kwamba huenda ikawa ni dhambi na hivyo anaacha kula nyama na kuamua kula mboga.

Mahali pengine anaandika kwamba mkienda sokoni msiulize ulize na wala ndugu yenu akiwakaribisha kuleni bila kuuliza. Hakusema kwamba wasiulize ile nyama ni ya mnyama gani hasha! Alisema wasiulize kama hiyo nyama imetolewa sadaka kwa sanamu au la. Mwishoni anasema endapo kwa yeye kula nyama ( iliyotolewa sadaka kwa sanamu ) kutamkwaza nduguye basi hatakula nyama ili asije akamkwaza ndugu yake ambaye Yesu Kristo alimwaga damu pale mslabani kwa ajiliya wokvu wake.

Bado tunaona kwamba tatizo hapo halikuwa juu ya wanyama najisi bali lilikuwa juu ya nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu.

Jambo hili la vyakula safi na najisi lilikuwa linaeleweka vizuri miongoni mwa wakristo wa kipindi hicho, ndiyo maana huoni Biblia ikiliongelea. Katika mafungu yote hapo juu tumeona kuwa hakukuwa na shida yoyote juu ya wanyama najisi na wasio najisi.
 
IMG-20171219-WA0042.jpeg
 
Katika hiyo hiyo biblia tuwekee hapa walawi 11 kwenda mbele alafu utueleweshe tuielewe vp biblia huku ni ndio na kule ni hapana katika jambo hilohilo
 
naona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.
 
Mbona hiyo ipo wazi, soma had mwisho, hakuzungumzia vyakula,bali matendo ya mwili

KWANINI USIJIULIZE, TUNAJUA MUNGU HAJIPINGI WALA SIO KIGEUGEU, MIAKA 700 NYUMA KABLA YA HILO ANDIKO LA marko 7 ,kupitia nabii ISAYA, huyo huyo Yesu akiwa mbinguni alinena haya

ISAYA 66

15 Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

16 Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.

17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.

18 Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.

HAPO ANAZUNGUMZIA SIKU YA KIAMA ATAKAVYOWACHALAZA VILIVYO WALA NGURUWE ,PANYA NA MACHUKIZO(najisi nyingine kama punda, kunguru n.k)
 
naona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.
Anachoelekeza Yesu hapa ni kukanusha imani iliyokuwa imeenea kuwa endapo Myahudi mtauwa (mcha-Mungu kwelikweli) angefuata tu sheria za usafi na taratibu za kidini angekuwa safi kimaadili/kiroho. Kwa upande mwingine, hakuna chakula ambacho kwa chenyewe kinaweza kuinajisi tabia ya mtu. Kinachonajisi ni mawazo maovu (ambayo hujitokeza kwa ndani na kujidhihirisha katika matendo ya nje). Ndiyo maana Biblia inatuambia, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mithali 4:23

Tunapaswa kuwa makini hapa kwa sababu Yesu hasemi kuwa vitu vyote vinaruhusiwa au vinafaa kuliwa. Hapa Yesu hazungumzii wanyama najisi na safi. Mada yake ni juu ya chanzo cha unajisi wa kimaadili/kiroho. Yesu anatumia kielelezo cha vitendo vya nje kama kuosha mikono na kula ili kuweza kutofautisha na hali ya moyoni. Yesu hugeuza mtazamo wa walimu wa sheria: walikuwa wamejikita katika mambo ya nje, wakati Yesu alisisitiza matendo ya ndani ya roho, hali ya kimaadili/kiroho. Kwa wengi, ni rahisi kudumisha hali ya nje ya kuwa Mkristo kwa kile tunachofanya au tusichofanya. Hata hivyo, wakati ambapo wanadamu huangalia nje, Mungu huangalia hadi ndani ya moyo—hupima nia na makusudi yanayosukuma matendo yetu. (Rejea Mwanzo 1:29-30; Matendo 10; 1 Wakorintho 10:31; Mathayo 5 :28, 29).
 
Amin
 
Madhara ya kakaririshwa badala ya kuelewa maandiko ndo haya

Na kwa umelo huu watu mtajikuta mnakula hadi nyama za watu hakyanani...!!!
Watakula hadi ya kenge, ukiwauliza Baba askofu gwajima amesema tule kila kitu,

HII TABIA YA KUKURUPUKIA MAANDIKO ,HASA NYARAKA ZA PAULO ,NDIO IMESABABISHA MADHEHEBU KAMA UTITIRI YA KILOKOLE KILA KICHOCHORO NA YOTE NA MANABII NA MITUME WANAONGEA LUGHA ZA KIPUUZI
 
2 PET. :3:15
Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;

2 PET. :3:16
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Mtoa mada ni mmoja wa watu wasio na elimu anayejaribu kupotosha ukweli
 
Kwenye agano la kale unajisi uko kwenye vitu vingi sio nguluwe tu, mfano mwanamke akiwa kwenye siku zake je hili nalo linafuatwa? Anyway sishabikii ulaji wa kitimoto kwanza hata kiafya tu anatatizo, ila nataka kujenga a big picture tusiwe tunaangalia angle moja kwenye kujenga hoja.
 
Swali. Maneno ya barua za Paulo ambazo si sahihi kuyaita injili yanapo pingana na injili takatifu utashika lipi for exp msidhani yakwamba nimekuja kuitangua torati
 
naona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.
Tofauti yako wewe na wakristo wa zamani.waliowekewa mipaka ya vyakula ni nini??
KATI YA MUNGU ALIYEWEKA KATAZO LA KULA VYAKULA FULANI.NA PAULO ALIYEHALALISHA KULIWA KWA KILA CHAKULA.

NANI AFATWE KATI YA MUNGU AU PAULO?
 
Kwa hiyo Mungu akisema kuwa kuna vyakula najisi anaweza kusema tena kuwa hakuna Vyakula najisi mungu huyo wa hivyo anajichanganya sana.

Mwenzako ametoa na maandiko ya bibilia wewe unaleta story zako za Facebook
 
Back
Top Bottom