Je, baba Daimond anaweza kumshtaki Daimond?

B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,279
2,733
Kuna tetesi kwamba baba Daimond, Mzee Abdul kaenda kustaki Daimond Mahakamani akidai fidia na kuzalilishwa. Hivi anaweza kulipwa? Na kama ikitokea akilipwa, inatakiwa alipwee mahela ya kutoshaa asee na hapo ndio hapo naamini usikate tamaa mpaka kaburini hakuna maskini.
 
Hio familia imejaa drama jamani duhhh. Washtakiane wasishtakiane nobody cares kwakweli. Hapa mjin kila mtu ana mambo yake
 
Hamna kesi hapo istoshe anajua kitambo nasib sio mwanae, yeye ndio kamdhalilisha kwa kusema yule mama alitoa mimba yake
 
Hiyo kesi itatupiliwa mbali, Diamond ana pesa, anavalishwa kofia na rais, anajulukana. Atapendelewa tu
TANZANIA HAMNA HAKI
 
Huyu Mzee Abdul anajidhalilisha tu; kwanini asitulie tu na kuendelea kwenda kusali msikitini? Diamond kisha tamka kuwa baba yake ni marehemu sasa huyu baba mwingine anatoka wapi?
 
Ili alipwe ni lazima aoneshe ni kwa namna gani amedhalilishwa,pia ni lazima aoneshe thamani yake,na hadhi yake ili mahakama,ipange fidia
 
Ngoja wajuzi wa sheria waje...

hivi defamation inaingia hapa?
Defamation ili uweze kushinda lazima uthibitishe kuwa;

Kuna habari au taarifa iliyotolewa na mtu mmoja kwenda kwa mtu au watu wengine na taarifa hiyo ni ya uongo ila huyo aliyetoa amewaaminisha watu kuwa ni ukweli na taarifa hiyo imekuletea madhara aidha kijamii au kiuchumi.

Sasa baba Diamond hapo hawezi kuthibitisha lolote kati ya hilo. Labda aje atuambie kuwa aliaminishwa kuwa mtoto ni wa kwake na akamlea hivyo anahitaji kufidiwa garama zake za malezi na matunzo ya mtoto huyo.
 
Mzee apambane ale jasho la ulezi sababu hata huyo Sandra mwenyewe ukute Diamond sio mwanae vilevile ..kamuokota tu kariakoo soko dogo na kumpeleka tandale.. huyo mtoto hana mwenyewe bana sandra asijifanye ye ndo wake saaaana!
 
Hamna kesi hapo istoshe anajua kitambo nasib sio mwanae,yeye ndio kamdhalilisha kwa kusema yule mama alitoa mimba yake
Diamond ni mstaarabu sana. Sanaaa.. Licha ya mapungufu yake.

Huyu mzee ilibidi yeye ndo awe ndani saiz..
Kwamba Diamond alitokana na Condom kupasuka. WTF.

Aisee.... Mi ningemweka ndani hata mwezi mamaee.
 
Kumshitaki anaweza lakini hawezi kushinda kwa sababu kuna Sheria inaitwa law of interectual property ambayo inazungumzia kuhusu patent right, copy right hivyo basi jina nasib au Abdul huyo mzee hana copy right yake hivyo kwa base hiyo hawezi toboa.

Mfano diamond platinum Hilo jina Lina copy right ukilitumia jipange
 
Back
Top Bottom