Je, askari 'wanaotanua' wanalinda sheria za barabarani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, askari 'wanaotanua' wanalinda sheria za barabarani?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Magobe T, Apr 18, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi nimekuwa nikiona kwenye 'traffic jam' madreva wa magari ya jeshi la polisi au JWTZ wakiwasha 'emergency lights' na kutanua na halafu wakishapita magari mengine yanawafuata nyuma na kusababisha msongamano mkubwa sana kwa vile madreva wa magari hayo huwa nao wanapata mwanya wa kutanua.

  Cha ajabu ni kwamba mara zote hukuti gari la askari yeyote likishikiliwa na 'taffic police' kwa kuvunja sheria za barabarani. Hivi hapa huwa ujumbe wake ni upi: kwamba askari hawezi kuvunja sheria isipokuwa raia tu au nini?

  Siku moja nilikuta polisi mmoja kwa sababu ya kutanua kwake na madreva wengine kumfuata akiwa amesababisha 'traffic jam' kubwa sana na akawa yeye mwenyewe anaanza kufokea watanuaji wenzake kwa kuziba njia. Niliona ni ujinga mkubwa wa kujifanya kwa vile yeye ni askari basi anakuwa juu ya sheria.

  Kwa kweli nilimpuuza sana na nikaona askari wa aina yake hawastahili kuwa katika jeshi hilo. Naomba tuchangie kwa hili na wahusika wapelekewe taarifa hizi. Binafsi huwa inanikera sana nikiona haya!

  Pili hili la bajaji; kweli ni sahihi kwa kauli niliyosikia? Mimi naona madreva wa daladala hasa zile zinazomillikiwa na wakubwa ndizo zina madreva na makondakta vichwa maji kwa vile wanajua hata wakivunja sheria hakuna kitakachofanyika dhidi yao.

  Naona kudhani kwamba madreva wa bajaji ndio wanaosababisha ajali barabarani ni kukweta kutatua tatizo la ajali barabarani. Pengine ni mradi wa wakubwa au pengine wamilki wa bajaji wengi si vigogo: mbona kungekuwa na mikakati kama hiyo ambayo imetangazwa kuhusu babajai ajali za magari zingepungua? Naona hapa tunachezewa akili na wakubwa.
   
 2. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli, kila siku njia ya Morogoro Road naona magari ya JWTZ, PT na wakati mwingine hata yale ya Ikulu yenye namba ST(namba)A nayo 'yakitanua'. Naona hiyo ndio staili ya 'kibongo-bongo' mwenye nafasi anaitumia nafasi yake vilivyo. Inasikitisha sana. Anayetakiwa kuwa mfano na kuzilinda sheria, yeye ndio anazivunja kwanza. Sijui, lakini mtazamo wangu ni kwamba, kuna kazi kubwa sana kufika kwenye nchi ya 'utawala bora'.
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Na mbaya zaidi ni pale askari hasa wa JWTZ wanaotanua na gari lao likachubuliwa. Wanasimama mara moja na wakikuta limeharibiwa wanaanza kumpiga buti dreva aliyefanya hivyo. Hapo ndipo huwa naumia sana moyoni kwani huwa naona ni ukatiri usio kifani.

  Hivi siku wananchi nao wakiamua kusimama kidete na kuzichapa si kutatokea mauaji sana (yaani wananchi watauliwa kwa risasi)? Ustaarabu ni mzuri na unaonekana kwa mtu anayefuata sheria lakini siyo ninavyoona kwa askari wetu wanavyofanya. Ndio maana tunasoma lakini hatuelimiki kamwe na tutabaki na ujanjawajanja wa kutumia 'shortcuts' na mabavu kwa vile kichwani hamna sana.
   
Loading...