Je, asali haipandishi kiwango cha sukari mwilini?

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
6,032
3,944
Salamu Waungwana na Wataalamu wa Baraza letu hili la Afya. ninaomba kujuzwa suala hili ambalo limekuwa likinitatiza sana.
Baada ya kupata matatizo ya Kisukari, miongoni mwa Ushauri niliopewa in ule wa kutumia Asali kwenye Chai na Maziwa ninayokunywa badala ya kutumia Sukari.

Ninaomba utaalamu na Ushauri wenu. Je Ninapokunywa Maziwa ama Chai, Kijiko kimoja cha Asali ninachoweka kwenye chai ama maziwa hayo, kinafanya Maziwa ama Chai hiyo kuwa na Utamu kuzidi ule wa Sukari!.

Ni kweli kwamba Utamu huo huwa unaishia mdomoni tu na unakuwa hausababishi Sukari kupanda mwilini?

Ninaomba Ushauri wenu.

Asali kweli haipandishi kiwango cha Sukari mwilini?
 
Asali na sukari vyote ni sukari tofauti ni kuwa asali ni monosaccharides sugar maana yake inaingia kwenye mfumo wa damu moja kwa moja.
Asante mpendwa Sky Eclat. Kwa maana hiyo hata ninapokunywa kijiko kimoja cha Asali asubuhi ninapoamka na usiku ninapokwenda kulala kama tunavyoshauriwi haipandishi kiwango chochote cha Sukari mwilini mwangu??
 
Asali na sukari vyote ni sukari tofauti ni kuwa asali ni monosaccharides sugar maana yake inaingia kwenye mfumo wa damu moja kwa moja.
Mono sacharide ni nini mkuu kwa lugha rahisi ?
Na nitatambua vipi kwamba chakula hiki ni mono,hiki ni poly na hiki ni disaccharide ?
 
Asali ina madhara kama sukari
Eeh!...kumbe sio kila Ushauri was Wataalamu wetu no was kufuata!!!
Siku zote nikilamba kijiko kikubwa cha Asali asubuhi kabla sijakula kitu na usiku kabla ya kulala, kumbe ndio ninazidi kujiangamiza!! Asante sana Eclat.

Nikuulize mpendwa, wewe binafsi unaweza ukashauri nini mbadala wa Sukari na Ssali kuongeza Utamu kwenye kinywaji cjochote unachokunywa katika Hall hii...?
 
Mono sacharide ni nini mkuu kwa lugha rahisi ?
Na nitatambua vipi kwamba chakula hiki ni mono,hiki ni poly na hiki ni disaccharide ?
Sukari ya matunda kama ndizi mbivu, matango nk ni mono hii ikifika tumboni inaingia kwenye mfuomo damu moja kwa moja. Sukari ya viwandani inapitia mfumo wa usagaji na kubadilishwa kuwa mono ili iweze kutumika mweilini.
 
Eeh!...kumbe sio kila Ushauri was Wataalamu wetu no was kufuata!!!
Siku zote nikilamba kijiko kikubwa cha Asali asubuhi kabla sijakula kitu na usiku kabla ya kulala, kumbe ndio ninazidi kujiangamiza!! Asante sana Eclat.

Nikuulize mpendwa, wewe binafsi unaweza ukashauri nini mbadala wa Sukari na Ssali kuongeza Utamu kwenye kinywaji cjochote unachokunywa katika Hall hii...?
Asali ni nzuri ukiwa na sukari ndogo inakurudisha haraka katika kiwango chako cha kawaida.
 
.. Nafahamu Sukari ya kawaida mwilini kabla hujakula chochote in kati ya 4 hadi 6 ama 7...unaposema 'Sukari Ndogo: kwa kipimo kama hicho, inakuwa kati ya ngapi hadi ngapi ndio inawe ikawa 'Sukari ndogo' mpendwa Eclat ambayo ninaweza kuendelea kulamba kijiko kimoja cha Sukari asubuhi na usiku, pengine hats na mchana?
 
Kwa wenye kisukari wanaelewa unapokua hypoglycaemia.
 
Salamu Waungwana na Wataalamu wa Baraza letu hili la Afya. ninaomba kujuzwa suala hili ambalo limekuwa likinitatiza sana.
Baada ya kupata matatizo ya Kisukari, miongoni mwa Ushauri niliopewa in ule wa kutumia Asali kwenye Chai na Maziwa ninayokunywa badala ya kutumia Sukari.

Ninaomba utaalamu na Ushauri wenu. Je Ninapokunywa Maziwa ama Chai, Kijiko kimoja cha Asali ninachoweka kwenye chai ama maziwa hayo, kinafanya Maziwa ama Chai hiyo kuwa na Utamu kuzidi ule wa Sukari!.

Ni kweli kwamba Utamu huo huwa unaishia mdomoni tu na unakuwa hausababishi Sukari kupanda mwilini?

Ninaomba Ushauri wenu.

Asali kweli haipandishi kiwango cha Sukari mwilini?
Asali Ni sukari Kama sukari nyingine .
Tofauti asali ni natural na hi nyingine Ni artificial.
Lakini pia ASALI huongeza kiwango Cha sukari kwenye damu .
Kama una kisukari acha kutumia ASALI,TENDE na VINAVYOFANANA NA HIVYO Mkuu.
ASALI HUPANDISHA SUKARI KWA KIWANGO KIKUBWA TU! USITUMIE KWENYE CHAI WAKA UJI WALA MAZIWA!
 
.. Nafahamu Sukari ya kawaida mwilini kabla hujakula chochote in kati ya 4 hadi 6 ama 7...unaposema 'Sukari Ndogo: kwa kipimo kama hicho, inakuwa kati ya ngapi hadi ngapi ndio inawe ikawa 'Sukari ndogo' mpendwa Eclat ambayo ninaweza kuendelea kulamba kijiko kimoja cha Sukari asubuhi na usiku, pengine hats na mchana?
Sukari ndogo, nafikiri(na ndio hivyo) kipimo kikisoma chini ya hiyo 4 mfano 2, 2.5molimol/ lita.
 
Asali na sukari ya kawaida inayotokana na miwa (sucrose) ni disaccharides zinazoundwa na sukari rahisi ( monosaccharide) za Aina mbili glucose na fructose. Tofauti ya asali na sukari ya miwa Ni uwiano wa sukari rahisi ambapo asali ina asilimia 40 fructose na asilimia 30 Ni glucose. Sukari ya viwandani inayotokana na miwa ina uwiano wa 50% glucose na 50% fructose. Kwa minajili hii sukari ya miwa ina kiwango kikubwa Cha sukari ukilinganisha na asali. Mathalani uwezo wa sukari ya kawaida kupandisha kiwango Cha sukari kwenye damu ( glycemic index) Ni 60 wakati glycemic index ya asali ni 58. Kwa hiyo asali na sukari ya kawaida vinaweza kupandisha sukari kwenye damu kwa haraka kwa sababu zote Ni disaccharides na zinafyonzwa (absorbed) kwa haraka baada ya kutumia. Pia mfanano wa monosaccharides na utofauti mdogo wa glycemic index unafanya sukari ya miwa na asali kupandisha kiwango Cha sukari kwenye damu kwa wingi zaidi ukilinganisha na vyakula visivyokobolewa. Kwa minajili hiyo haishauriwi mtu mwenye kisukari kutumia asali. Kula asali hata kijiko kimoja kunaweza kupandisha sukari kwa haraka na kumsababishia matatizo mhanga wa kisukari. Pia ni hatari zaidi kuitumia kabla ya kulala. Ukitaka kuthibitisha hili tumia asali kabla ya kulala halafu ukiamka asubuhi pima sukari yako uone itakavyokuwa kubwa ukilinganisha na siku ambazo umelala bila kuitumia.
Nakushauri unywe chai yenye viungo kama tangawizi, mdalasini, limao, pilipili mtama na karafuu bila kuweka sukari ya aina yeyote.
 
Safii ujumbe mzuri Sana Mkuu kuhusiana sukari halisi na artificial katika kuongea / kupandisha sukari katika damu
 
Salamu Waungwana na Wataalamu wa Baraza letu hili la Afya. ninaomba kujuzwa suala hili ambalo limekuwa likinitatiza sana.
Baada ya kupata matatizo ya Kisukari, miongoni mwa Ushauri niliopewa in ule wa kutumia Asali kwenye Chai na Maziwa ninayokunywa badala ya kutumia Sukari.

Ninaomba utaalamu na Ushauri wenu. Je Ninapokunywa Maziwa ama Chai, Kijiko kimoja cha Asali ninachoweka kwenye chai ama maziwa hayo, kinafanya Maziwa ama Chai hiyo kuwa na Utamu kuzidi ule wa Sukari!.

Ni kweli kwamba Utamu huo huwa unaishia mdomoni tu na unakuwa hausababishi Sukari kupanda mwilini?

Ninaomba Ushauri wenu.
16346318992585266185438617818529.jpg

Asali kweli haipandishi kiwango cha Sukari mwilini?
Watu wenye Sukari wana sukari yao maalumu ya kutumia. Inapatikanika sehemu nyingi. Inakuwa ya kidonge au drops. Kidonge kimoja ni sawa na kijiko kimoja cha sukari. Nimeattach picha hapa
16346318992585266185438617818529.jpg
 
Back
Top Bottom