Je angefaa kuwa SPIKA wa Bunge Letu - CCM ilimfanyia fitna? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je angefaa kuwa SPIKA wa Bunge Letu - CCM ilimfanyia fitna?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FUSO, May 17, 2011.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Poleni sana na maisha magumu Watanganyika wenzangu, tufafika tu mdogo mdogo. Mimi sina mengi ila najaribu kuangalia hizi tuhuma mpya za kisiasa ambazo Mpendazoe amezitoa hadharani jana, inaonekana kuna dalili za ukweli kwamba baadhi ya wana CCM (Chama Tawala) walitaka kukichakachua chama chao mmojawapo akiwa Sita Samweli kada kwenye uzoefu ndani ya chama hiki kikongwe.

  Wengi pamoja na mimi tulisikitika sana wakati jina na mpiganaji wa ufisadi huyu ndani ya chama tawala lilivyokatwa wakati wa kuwania uspika wa Bunge. Kwa mbali tangu jana naona dalili za uvujifu wa kimaadili ya kichama uliofanywa na kada huyu number moja kutaka kukisaliti chama chake, Wana JF changieni

  a) Je tuhuma hizi zina chembe chembe ya ukweli?

  b) Je huyu Jamaa angefaa kuwa spika wa bunge la Jamhuri kwa mara ya pili hasa uliangalia record yake ya kiutendaji wa bunge lililopita?

  c) Je anafaa kuwa kiongozi wa watanzania na ana uchungu na ubadilifu wa mali za umma? yaani anaweza kuwa Rais kwa nchi hii kama akipendekezwa na chama chake 2015?

  d) Je ni kipi kilichomfanya ageuke na arudi tena alikotaka kutoka? ni kweli uchu wa madaraka au kuna jingine limejificha?

  e) Je nani mwenye makosa, Mpendazoe aliyesema tuhuma hizi na kutorudi kwake nyuma au wenzake ambao baadae waliamua kurudi kundini na kuomba msamaha na kupewa madaraka ya kuongoza umma tena?

  f) Je kisiasa ni makosa kubadilisha msimamo wako hasa unapogundua umefanya makosa ya kukihujumu chama chako? kosa hili linasameheka?

  Wengi wetu bado tunaamini kada huyu alionewa kwa kukatwa jina lake kwa kigezo cha jinsia, je ni sahihi na angefaa kabisa kuliongoza bunge regardless hizi tuhuma za mpendazoe ambazo hazina uhakika?

  FUSO - safarini Gairo - Dar.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  very simple hakuna tuhuma juu ya sitta

  Think big
   
 3. F

  FUSO JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  safi sana mkuu, lakini ninavyojua mimi lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani - ndiyo maana nikasema suala likisemwa lazima lina chembe chembe za ukweli ndani yake, hebu tusikie wana JF wengine na mitizamo yao.

  Wewe umesahau makamba alivyofunga safari toka dar hadi urambo kwao sitta? alienda kufanya nini?

  Tatizo si kufichaficha jambo ili tujue halipo, turuhusu tuongee na kuona kwamba mzee wetu yupo safi na alionewa na wana ccm wenzake na anabakia kuwa mpiganaji ndani ya chama na angefaa kabisa kuishikiria hii post ya juu ya uongozi wa bunge.
   
 4. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sita yuko vizuri CCM ndio iko hovyo wanataka kumuua kisiasa tu maana aliwabana sana wakati akiwa spika.
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Je yupo sahihi kuendelea kubaki ndani ya chama chenye watu wanaotaka kumuua kisiasa? je atajinasua vipi mbele na masikio ya watanzania wajue kwamba yote hayo ni njama tu juu yake? atajitetea vipi ki-uwazi akiwa ndani ya chama ili wananchi wamuelewe?
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kijana unapenda pumba vichochoroni.....:dance::dance::dance::dance::A S 103::A S 103::A S 103:
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  King of Kings ndugu yangu ziite Pumba lakini ndani yake kuna mchele tena wa Mbeya. - ha ha ha

  Mficha maradhi...... mficha moto.......yasemwayo.........

  kuna hoja ya msingi inayotaka majibu.
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mimi naona bhal bhal hakunam hoja ya msingi

  Sitta ndo mtu pekee ccm hizo tuhuma zako ni legelege, kapate chai kwanza ndo ulete zingine
   
 9. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ninawasiwasi kwa CDM sasa inatumiwa na MAFISADI MAPACHA ili kuwachafua wote wapinzani wao ndani ya chama. Hata kama ni ukweli walitaka kukiasi chama, mbona kuna kundi la G55 lilitotaka kuvurunga muungano lakini bado lipo CCM. Sasa nimekubali usemi wa Mh. Pinda kuwa mafisadi wana nguvu kweli. Ninafikiri wameamua kuwatumia kama siyo wote basi baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani hasa CDM na Mtikila kuwavurunga wale wote waliokuwa wanapamba nao ambao ni Nape, Sita, Mwakyembe, Kilango, na wengine wengi tutawasikia. Lakini kila kitu kina mwisho kwani hata JK alitumia mbinu zake, sasa zinaonekana mzigo kwake.
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sisi webgine sidhani kama tunaweza kuziita tuhuma isipokuwa ccm maana ndo waliotaka kuondokewa na Sitta. Hii imekuwa wazi kuwa ccm walimgundua Six kabla ndo maana walimtema kwenye usipika.

  Lakini pia inaonyesha CCM wanamwogopa six ndo maana ****** amemtuliza kwa huo uwaziri. Nadhani CCM walimwita six pengine na Mwakyembe wakawasihi warudi na kuwaahidi hivyo vyeo. Issue inayowasumbua CCM hapa ni mgawanyiko ambao ungeweza kutokea ikiwa wangeruhusu six na kundi lake waondoke ccm. Nadhani usipika ni critical kwao ndo maana hawakuweza kurisk kumpa six maana alishawaliza kipindi kilichopita.

  Kimsingi hakuna tuhuma na wala ccm sidhani kama watasema chochote kwa hili maana walikuwa wanalijua ila ilikuwa haijawa wazi to public.
  Impact ya hii issue ni kwa wahusika wenyewe(six,nape na mwakyembe) ambao wataonekana ni watu ambao ni rahisi kununuliwa na kubadilisha msimamo wao. Kama CDM wataiuza hii issue kwa mtindo wa kuwaua hawa jamaa basi watamalizika kisiasa ila sioni direct impact kwa chama cha magamba.

  Hii pia inaweza kuimply kuwa Nape naye alihongwa kile cheo cha udc kwa sababu ya hii issue hivyo ni mchumia tumbo tu hana uzalendo wowote kama anavyodai majukwaani.
   
 11. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani alichokifanya Sitta kinazidi kuonyesha ya kuwa ni mtu makini. Ikumbukwe baada ya kuhenguliwa EL kuliibuliwa mkakati wa kuwahengua Sitta na Mwakyembe ndani ya CCM. Katika hali hiyo, ilikuwa ni jambo la busara kujiweka tayari tayari ili wasije kukosa mahali pakukimbilia endapo hilo lingelitokea. Kwakuwa halikutokea hapakuwepo sababu yeyote ya kukihama chama chao.
   
 12. r

  repaka New Member

  #12
  May 17, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitta ni mchezaji imara kwenye timu mbovu. Ni vigumu kutambua mchango wake katika timu hiyo. Hata hivyo alitumia vizuri nafasi aliyoipata kwa kuanika maovu ya yanoyofanywa na chama chake cha ccm. Hivyo bado ni shujaa na tusimtathmini kwa tuvijimambo tudogo tudogo kama hutu!!!!!!
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Mtu makini ni yule anafikia hatua ya kukisaliti chama chake? Yeye na lowassa nani ni makini kwa mtazamo wako? ni sawa na General Manager kuanza kula dili za barabarani kuinyika kampuni anayoiongoza tender za kazi. a senior person like him aamue kuingia vichakani kukisaliti chama then mnasema hana hoja ya kujibu - this is strange.

  Hili jambo ni kubwa unless Mpendazoe awe muongo, mimi nafikiri kosa la mpendazoe ni kuanza kutoa siri walizokula kiapo hawatazisema milele if it was like that.
   
 14. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  I beg to differ. Chadema ikiwachafua akina Sitta si kwa msukumo wa mafisadi. It's rather a political tactic!

  Hata kama wewe ungekuwa Chadema unayetaka kuipokonya madaraka CCM some day (na si kuendelea kubaki mpinzani milele), nina uhakika ungependa kuiona CCM ikiwa weak all the time.

  Sitta & co wakiendelea kubaki CCM na kuifanya CCM ionekane iko unified, hiyo si habari njema kabisa kwa Chadema....so lazima mbinu ya kuwagombanisha CCM itumike!

  Adui mwombee njaa ati!
   
 15. F

  FUSO JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  kwa nini uendelee kukaa kwenye timu ambayo ni mbovu, haina kocha wala benchi zuri la ufundi? then bado ujiite mchezaji bora wa viwango?
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  suala la G55 senario yake si kama hii ya kina NAPE na uasisi wao wa CCJ ndugu yangu usichanganye mambo. G55 walikuwa ni wabunge na walijulikana kwa majina na msimamo wao wa kudai Tanganyika ndani ya bunge, huo haukuwa uasi.

  Hawa kina NAPE walikuwa Msituni.
   
 17. V

  Vonix JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Upandacho ,ndicho utakachovuna Sitta na wale waliojulikana kama wapambanaji dhidi ya ufisadi hawakuwa wakweli wale wanaojifanya kusukuma gari wakiwa ndani haliendi,wa Tz tuache ushabiki mtazunguka weeee..........mtarudi mimi ningewaelewa kama wasingekubali hizo nyazifa zao vinginevyo njaa inawasumbuwa.
   
 18. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  majibu anayo yeye mwenyewe...CCM haina mwelekeo leo Magufuri atasema hivi kesho pinda vile wanauana tu kisiasa na sasa hivi tunajipanga tu sisi 2015 mtatukoma na MAGAMBA yenu
   
 19. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii imekaa ki-shabiki zaidi
   
 20. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #20
  May 17, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Angefaa sana kuwa Spika...kwa Maana ni Mpinzani ndani ya CCM
   
Loading...