Je angefaa kuwa SPIKA wa Bunge Letu - CCM ilimfanyia fitna?

Angefaa sana kuwa Spika...kwa Maana ni Mpinzani ndani ya CCM

siyo mpinzani bali ni majeruhi ndani ya chama baada ya kutishiwa kunywanganywa kadi pale dodoma na adhabu nyingine kunyiwa uspika. huwezi kuwa mpinzani within kwani kufanya hivyo unajimaliza mwenyewe, jamaa lazima waku fix.
 
Hivi Mh. Kikwete asingeteuliwa 2005 kuwa mgombea wa CCM leo angekuwa bado CCM? najaribu kutafakari tuu
 
Swala la either Sitta ana tuhuma au la liko chini ya chama chake. Kama kitendo alichotaka kukifanya wataona ni cha kawaida, basi itakuwa hakuna issue.

Lakini kama watajifanya kama walikuwa hawajui kama alikuwa na mipango ya kukisaliti chama hadi juzi tu Mpendazoe alipotoboa jipu, basi hiyo itakuwa shock kubwa na kuanzia hapo ndo tutajua kama Sitta ana doa ndani ya chama chake au la. Ila najua ccm walikuwa wanajua fika hiyo mipango ya mzee wa Urambo, na ndiyo maana wakamlambisha hako ka u waziri ili apate pa kupumzikia.

Yote kwa yote wanajua kabisa kwamba Sitta siyo wakupelekwa pelekwa. Hivyo hii itawasaidia kukaa naye "vizuri". Vinginevyo kwa mambo tunavyoyaona hakuna mtu ndani ya chama chake anayeweza kumfanya kitu au kumnyooshea kidole.
 
Ninawasiwasi kwa CDM sasa inatumiwa na MAFISADI MAPACHA ili kuwachafua wote wapinzani wao ndani ya chama. Hata kama ni ukweli walitaka kukiasi chama, mbona kuna kundi la G55 lilitotaka kuvurunga muungano lakini bado lipo CCM. Sasa nimekubali usemi wa Mh. Pinda kuwa mafisadi wana nguvu kweli. Ninafikiri wameamua kuwatumia kama siyo wote basi baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani hasa CDM na Mtikila kuwavurunga wale wote waliokuwa wanapamba nao ambao ni Nape, Sita, Mwakyembe, Kilango, na wengine wengi tutawasikia. Lakini kila kitu kina mwisho kwani hata JK alitumia mbinu zake, sasa zinaonekana mzigo kwake.

Mimi nashangaa kumwamini sana Sitta . Kwa kitu gani ambacho kinakufanya udhani kwamba yeye ni mtu msafi ? Chadema haiutumiwi na mafisadi bali anaye ongea na Mpendazoe anasema walikuwa watu 6 toka CCM kamtaja Nape na anasema mwingine ni Sitta sasa unapinga nini . Kwa nini amtaje Sitta kama hakuwepo mbona asimtaje RA na wengineo ? Kama Sitta alikuwa CCJ inasemwa tu na ieleweke na uzuri Mpendazoe kasema ngojea sasa Sitta aje kupinga na kama kuna ushahidi wa maandiko utasemaje ndugu yangu ?
 
Hivi Mh. Kikwete asingeteuliwa 2005 kuwa mgombea wa CCM leo angekuwa bado CCM? najaribu kutafakari tuu

utata mtupu...urais ni mtamu kaka, watu washaanza kampeni za 2015 kimya kimya, wengine wanasema jina tayari lipo kwa mkubwa wetu wakati sisi bado tunahangaikia ka-katiba kapya. duh kazi kweli kweli hii.

mdogo mgogo tu - mwenda pole.
 
Angefaa zaidi ya awamu ya kwanza na ccm ikiona cha moto. Kwa kuona hivyo ndio maana wakamfanyia uchakachuzi wa zamu ya wanawake. Tusubili 2015, itakuwa zamu ya nani urais???????
Sita kifaa mwanangu Humuoni? au huna macho...! Dowans wamelipwa ? kama si michango ya akina sita ingeishalipwa zamani na akina jk.
 
Ninawasiwasi kwa CDM sasa inatumiwa na MAFISADI MAPACHA ili kuwachafua wote wapinzani wao ndani ya chama. Hata kama ni ukweli walitaka kukiasi chama, mbona kuna kundi la G55 lilitotaka kuvurunga muungano lakini bado lipo CCM. Sasa nimekubali usemi wa Mh. Pinda kuwa mafisadi wana nguvu kweli. Ninafikiri wameamua kuwatumia kama siyo wote basi baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani hasa CDM na Mtikila kuwavurunga wale wote waliokuwa wanapamba nao ambao ni Nape, Sita, Mwakyembe, Kilango, na wengine wengi tutawasikia. Lakini kila kitu kina mwisho kwani hata JK alitumia mbinu zake, sasa zinaonekana mzigo kwake.

Ni strategy tuu,hiyo ni political game wanachofanya ni kuionyesha jamii kwamba dhana yao ya kujivua Gamba haina mantiki maana chama kina mafisadi,wavivu,wagomvi,walevi wazinzi,wezi wala rushwa kwa maneno ya Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete,chadema wao wanongezea tu kwamba wapo pia wanafiki akina Sitta,Nape ,Mwakyembe,n.k ni nyongeza ya chumvi tena ili ikolee vizuri baada ya mwenyekiti wa CCM kuikoleza
 
poleni sana na maisha magumu watanganyika wenzangu, tufafika tu mdogo mdogo. Mimi sina mengi ila najaribu kuangalia hizi tuhuma mpya za kisiasa ambazo mpendazoe amezitoa hadharani jana, inaonekana kuna dalili za ukweli kwamba baadhi ya wana ccm (chama tawala) walitaka kukichakachua chama chao mmojawapo akiwa sita samweli kada kwenye uzoefu ndani ya chama hiki kikongwe.

wengi pamoja na mimi tulisikitika sana wakati jina na mpiganaji wa ufisadi huyu ndani ya chama tawala lilivyokatwa wakati wa kuwania uspika wa bunge. Kwa mbali tangu jana naona dalili za uvujifu wa kimaadili ya kichama uliofanywa na kada huyu number moja kutaka kukisaliti chama chake, wana jf changieni

a) je tuhuma hizi zina chembe chembe ya ukweli?

b) je huyu jamaa angefaa kuwa spika wa bunge la jamhuri kwa mara ya pili hasa uliangalia record yake ya kiutendaji wa bunge lililopita?

c) je anafaa kuwa kiongozi wa watanzania na ana uchungu na ubadilifu wa mali za umma? Yaani anaweza kuwa rais kwa nchi hii kama akipendekezwa na chama chake 2015?

d) je ni kipi kilichomfanya ageuke na arudi tena alikotaka kutoka? Ni kweli uchu wa madaraka au kuna jingine limejificha?

e) je nani mwenye makosa, mpendazoe aliyesema tuhuma hizi na kutorudi kwake nyuma au wenzake ambao baadae waliamua kurudi kundini na kuomba msamaha na kupewa madaraka ya kuongoza umma tena?

f) je kisiasa ni makosa kubadilisha msimamo wako hasa unapogundua umefanya makosa ya kukihujumu chama chako? Kosa hili linasameheka?

wengi wetu bado tunaamini kada huyu alionewa kwa kukatwa jina lake kwa kigezo cha jinsia, je ni sahihi na angefaa kabisa kuliongoza bunge regardless hizi tuhuma za mpendazoe ambazo hazina uhakika?

fuso - safarini gairo - dar.
jitihada zake zilikua zimelenga kulinusuru taifa kutoka kwa mafisadi alijitahidi kufanya hivyo ndani ya ccm na nje ya ccm na bado anaendelea kufanya hivyo.kama angelichagulwa kua spika angelifaa taifa kuliko huyu mmama.
 
Back
Top Bottom