Habari wakuu
Nina kama miezi miwili tangu nilipo rejea kutokea nchi jirani ambako nilipokuwa nikiishi, niliondoka nikiwa mtoto mdogo sana na baada ya miaka ipatayo 8 hatimaye nimerejea.
Jirani na kwetu kuna binti ambaye nilimuacha mdogo lakini nilishangazwa kumkuta amekua binti mkubwa. Kwakuwa tumejuana kitambo tangu enzi za utoto, yalianza mazoea akawa anapenda sana utani na mimi.
Sasa kilicho nifanya niandike huu uzi ni kwamba siku za hivi karibuni yule binti ameninunia bila sababu yeyote kwani sijawahi kugombana nae wala kupishana kauli, hili limeniacha na maswali mengi inakuaje ghafla tu mtu akununie bila sababu.
Wakuu najua humu kuna wataalam wa saikolojia ya wanawake, naombeni mnisaidie nimeshindwa kumuelewa.
Nguvu moja