Je, ajira za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinapatikana vipi na vigezo vyake ni vipi?

Tunaajiri kwa kuwachukua chuoni moja kwa moja vijana walifaulu vizuri kuanzia O'Level, A' Level na Chuo.
Yaani wale ma genius.
Walio na Bachelor, Masters au PHD.
Ukiondoa Wapishi, Walinzi na watunza mazingira.
 
Tunaajiri kwa kuwachukua chuoni moja kwa moja vijana walifaulu vizuri kuanzia O'Level, A' Level na Chuo.
Yaani wale ma genius.
Walio na Bachelor, Masters au PHD.
Ukiondoa Wapishi, Walinzi na watunza mazingira.
Mkuu...ni wakati wote wanafanya hivyo?wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda gani sasa?
 
Si yuko Ud km 'pesa zao zinarudi'kama kawa!
Sawa na kutoa pesa mfuko wa kushoto na kuiweka wa kulia.

Hakuombwa kusomeshwa na b.o.t bali b.ot wao ndo huwa wanawasomesha wenye gpa kali na yeye ndo aliongoza,hakuna sehem inayombana lazima afanye b.o.t
Wacha apige uchumi soon anakuwa mshauri wa magu bado anazunguka palepale.
Mkuu lakini hizi taasisi zinapokusomesha hazikusomeshi bila makubaliano, pesa zao anarudishaje?

Sent from my SM-G900P using JamiiForums mobile app
 
Habari za asubuhi watanzania wenzangu.

Ninaomba kuuliza, hivi ajira za kazi kwa Benki ya Tanzania huwa zinatangazwa vipi. Na km ukitaka ku apply inabidi uwe navigezo vipi?

Ninandoto zakufanya kazi B.O.T kwa mkoa wowote wa Tz na masomo niliyosomea niya biashara. Naomba msaada wenu.

Ndoto zangu zilianzia hapa...nikiwa kidato cha tatu,
Sikumoja nilikua napita ktk mabenki ktk mkoa mmoja kusini Kwa lengo lakubadili hela yangu (10,000Tzs) iliyokuwa imechanika. Hovyo kwamatumizi yakawaida ilikua ikishindikanika.

Nakumbuka nilipita km bank tatu tofauti na zote zilinipa majibu..."sisi hatubadili pesa chakavu hapa labda nenda banki nyingine unaweza pata huduma hiyo"
Sikuchoka na nilipoenda banki ya nne wao walinijibu kuwa niende B.O.T.

Nilielekea huko lakini baada yakufika nilipatwa na mshangao kwa jinsi nilivohudumiwa. Wale wafanyakazi walionesha dhahiri wanamaadili ya kazi zao. Hawakunidharau na elf 10 yangu bali walikua straight kunielekeza kuwa ukitoka hapa. Utaenda pale. Baada ya pale nenda dirisha lile.

Kwakweli nilifarijika sana sana ,kwani kuanzia walinzi hadi wafanyakazi wengine walinionesha kunijali. Tofauti na wale wa awali niliokuwa nipita kuuliza ktk banki kubadili fedha yangu.

Hapo ndipo ari yakusoma kwa bidii ilishika kasi kwa lengo moja tu. KUFANYA KAZI B.O.T
Na namshukuru Mungu mwaka jana nime graduate salama.

Utata unapoanzia nihapa.
Nikuwa, nimetafta sana njia zakufanya maombi yakazi huko lakini sijaona.
Nimejaribu kununua magazeti yale international wide kuwa whuenda nikaona matangazo huko lakini wapi...
Nimetumia njia nyingi sana kufanikisha hili kwakifupi bado sijafanikiwa.

Hivyo basi kwa yeyote mwenye uelewa na haya mambo naomba anipe namna ili niweze kukamilisha ndoto yangu.
MPAKA UWE KADA WA CHAMA TAWALA UNLESS UKOO WAKO UNATAMBULIKA NA TANU...............................
 
Note this, office assistant au dereva TPDC first appointment anaanza na basic ya 1.3m, anapata housing allowance 350k, transport allowance 300k, Risk allowance 300k ..
BOT kwa kada hizohizo unakopeshwa 60m bila riba kwa ajili ya kujenga nyumba
Not true
 
Wewe njaa kali ndo unawaza sana mtonyo,kakataa ofa za wazungu baada ya phd kasema anataka kurud ud kufundisha ndo kazi anayopenda lazima arudi alipotokea na arudishe alichokipata kwa jamii.
Itakuwa tu alitaka kwenda kuwatambia totoz za ud,na kuwala kwenye cw
 
Exactly kabisa hata mwaka huu kuna watu wameitwa kufanyiwa interview pasipo kuomba wamechukuliwa majina ya ma best kutoka bcom udsm na chuo cha kodi kwa miaka tofauti majina yamechukuliwa vyuoni watu wakapigiwa simu mchakato umesimamiwa na wizara ya fedha wameombwa tu cv ni watu km 30 wameambiwa wataajiliwa either BOT na Wizara ya fedha
kikawaida BOT huwa wanatangaza kwenye vyombo vya habari kama wana nafasi iliyo wazi.
Ila mara nyingine BOT wanakwenda chuoni na kuajiri moja kwa moja wale waliofaulu vizuri sana darasani ambao vipanga kuna ndugu yangu alimaliza BCOM alipata first class yaani mwaka wao wote waliopata First class BCOM waliajiriwa BOT.
Otherwise pia wanaoffer scholership yao inaitwa mwalimu nyerere scholership kusomesha masters degree, mara nyingi watu wanaomaliza hizo scholership na kufanya vizuri pia wanapewa ajira BOT kiufupi BOT wanaangalia sana grade zako za darasani degree yako ili kupata ajira kwa sasa. zamani wakati wa akina liumba kulikuwa na kamtelezo flani hivi hadi watu wasiokuwa na vyeti waliajiriwa ila kwa sasa hakuna huo ubabaishaji. Kama hauna first class ndugu achana na mawazo ya kufanya kazi BOT
 
Usibishe kitu usichokijua mkuu.. hapa ujue unabishana na watu wenye first hand information.. kwani umsoma chuo gani? Story za huyo Chegere ulishawahi kuziskia?
nadhani hajazisikia stori za chegere.... jamaa alikuwa sio TANZANIA ONE tu Alevel EGM pugu ... Bali alikuwa THE BEST STUDENT UDSM Undergraduate
 
Kama sio siri,basi hebu attach hapa salary slip zako za miezi mitatu nyuma
Mzee unachanganya mambo Kuna salary slip ya mwajiriwa, na rank za mishahara za taasisi ..., Kwa serikali kuu mbna zinatolewa ziko wazi..

Kwa mashirika ya umma wanaogopa kuweka wazi kwa sababu mishahara ni mikubwa na kuna tofauti kubwa ya gap ya mishahara kwa kada zinazofanana Kati ya walio serikali kuu na mashirika ya umma, wanaogopa watu kuhoji zaidi na SI vinginevyo
 
Back
Top Bottom