Je africa sattelite inahusu chanel za bure kwene ving’amuzi?

Friedrich Nietzsche

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
1,145
1,911
Wakuu naomba tujuzane kitu

Kuna uzi unatrend sana humu jf wa kuhusu kuset chanel unaitwa Africa satellite sat gear

African Satellite World and Sat Gear

Je unahusu namna ya kuset channel za bure au??
Wengine kingereza hatujui
 
Huo ni uzi ambao wadau wanajadili namna ya kutazama FTA ambazo zipo free kwa wakati huo...

FTA maana yake ni free to air, hizi ni stesheni za TV ambazo mtu akiwa na dish na receiver anaweza akazitazama pasipo malipo...

Huko angani kuna utitiri wa satelaiti ambazo zinarusha matangazo ya televisheni sehemu mbalimbali duniani, na satelaiti hizo zipo uelekeo tofauti ambao mara zote ni nyuzi kadhaa magharibi au mashariki...

Ili kupata mawimbi ya satelaiti fulani huku duniani, unapaswa uwe ndani ya kivuli cha satelaiti hiyo (wanaita footprint) na uelekeze dish lako kwenye uelekeo ilipo satelaiti hiyo...

Ukiachana na hizo FTA, pia kuna mawimbi mengine ambayo yamewekewa ulinzi(keys) unaohitaji uwe na receiver inayoweza kuzisoma ili kuweza kufungua channels. Katika uzi huo pia kuna majadiliano yanayohusiana hili nililolieleza hapa...
 
Mkuu unaonekana una uelewa wa haya mambo!!

Je mfano ukiwa na dist la azam au dstv unawez kuzipata hizi chanell

Na je unaset vip

kama hutojali tuelezew hilo! maana wengi wanaonekana hawana uelewa
 
Ni maelezo marefu kidogo mkuu...

Kwa kutumia dish la Azam au DSTV na receiver za kawaida za FTA sio hizi za DSTV au Azam, unaweza kupata channels za masafa ya kU...

Dish la Azam, DSTV au kampuni yeyote huwa limelekezewa kwenye satelaiti inayobeba masafa ambayo Azam, DSTV wamepewa kibali kuyatumia kurusha matangazo yao...

Mfano ukiwa na receiver ya FTA zile za kariakoo, pasipo kugeuza wala kugusa dish la Azam, ukichomeka waya kwa receiver ule unaotoka kwa dish, ukascan kuingiza channeli utapa za bure kadhaa kama TV ya Zimbabwe, baadhi ya channels za Iran n.k fungua hii link na tazama majina yaliyoandikwa kwa rangi ya njano ndio TV za bure....

Elimu zaidi pitia huu uzi umeandikwa kwa kiswahili na huyu member...

Thread 'Wale wa madish ya ku-band na C- band pamoja na receiver pitia hapa' Wale wa madish ya ku-band na C- band pamoja na receiver pitia hapa
 
mkuu mungu akuweke
 
nunua universal DVB ambayo inaweza kuwa na support nyingi za satelite mfano etisalati 7A hii unaweza kupata DSTV na etisalat 7B unaweza kupata AZAM.
kila setelite ina uwelekeo wa dishi na angle.
na mpaka sasa hivo DVB ZIPO AMBAZO UNAWEZA KULIPA CHANELI KWA SARAFU YA KIDIGITALI NA ZENGINE FREE
 
hizi ukiwa nazo kifurushi kikiisha unaendelea free kwa baadhi ya chanel
 
Ni hivi chanzo Cha channel nyingi Huwa ni Bure mfano channel nyingi za Tanzania,Asia,Africa au za habari za kimataifa Huwa ni za Bure hivyo ukiwa na dish sifa ya kukamata channel husika basi utaipata
Cha kwanza Ili ufaidi free tv lazima uwe na aidia hata kidogo juu ya masuala ya satellite hasa ukamataji na vifaa vyake
Mfano lazima ujue uelekeo wa dish, setting(frequency, symborate&polarization,) vifaa utofauti kati ya receiver na decoder, Nini maana ya ku na c band, longitudinal angle nakadharika.
Ukishavijua hivyo hapo jua kamwe hautokuja kulipia tv, shida huwa inaleta addiction yaani unaweza jikuta Kila mara unataka kugeuzageuza dishi kupata channel tofauti tofauti.
 
Receiver zipo aina mbalimbali na bei tofauti,mfano juzi kati nimenunua mediastar 4030 pro kwa 300k,ni bonge la decoder.ingia Google utapata sifa zake hapa nitajaza ukurasa kuielezea.ninachokipata kwa dekoda hii hata hawa akina azam naona kama uchaf tu.

hii decoder inakua na chanel zote za nje na ndani au inakua na chanel za ndan tu
 
Ni hivi chanzo Cha channel nyingi Huwa ni Bure mfano channel nyingi za Tanzania,Asia,Africa au za habari za kimataifa Huwa ni za Bure hivyo ukiwa na dish sifa ya kukamata channel husika basi utaipata
Cha kwanza Ili ufaidi free tv lazima uwe na aidia hata kidogo juu ya masuala ya satellite hasa ukamataji na vifaa vyake
Mfano lazima ujue uelekeo wa dish, setting(frequency, symborate&polarization,) vifaa utofauti kati ya receiver na decoder, Nini maana ya ku na c band, longitudinal angle nakadharika.
Ukishavijua hivyo hapo jua kamwe hautokuja kulipia tv, shida huwa inaleta addiction yaani unaweza jikuta Kila mara unataka kugeuzageuza dishi kupata channel tofauti tofauti.

we unaweza unisaidie
 
Back
Top Bottom