Je, ‘’15 minutes of fame’’ za Fatma Karume zimegharimu biashara za IMMMA Advocates na TLS?

Kwenye nchi zetu zinazoendelea huwezi kuepuka ukweli kuwa serikali ndio taasisi pekee ambayo matumizi yake ya pesa ndio kipato kikubwa kwa makampuni makubwa ya huduma na kwa mantiki hii huwezi kufanya kazi za uwakili ambazo zinahusu makampuni makubwa ya ndani na kimataifa ambayo mdawi wake mkubwa ni serikali halafu ukaanza kuishambulia serikali kisiasa ukitegemea mafanikio kibiashara. Ni lazima utapoteza moja au yote. Huu ni ukweli ambao wenye kujua umuhimu wa biashara zao za huduma wanaujua na huufanyia kazi.

IMMMA Advocates ni kampuni kubwa ambayo niya vigogo ndani ya CCM ambao mizizi yao iko pia serikalini na kwenye taasisi ya mahakama. Kwa mantiki hii hawawezi kukubali kampuni yao kugonganishwa kisiasa na serikali waziwazi.

Alichokuwa anafanya Fatma Karume hakina tofauti na kujipiga risasi mguuni bila kujua huku akishangiliwa na watu wanaodhani anachofanya ni kuwaburudisha kwenye mitandao huku kampuni ya IMMMA Advocates ikipata matatizo kibiashara.

Badala ya kutumia Urais wa TLS kama daraja la kuiunganisha IMMMA Advocates kibiashara badala yake ametumia kama uzio wa kuitenganisha na serikali. Hata Urais wake wa TLS umeifanya TLS kuwa mbali na taasisi ya mahakama badala ya kuwa karibu zaidi.

Washirika wenzake wamemuomba achague moja kati ya mawili kama anataka aendelee kuwa mshirika wa IMMMA Advocates. Kama anataka aendelee na uanaharakati kama Rais wa TLS au aachane na uanaharakati ndani ya TLS.

Kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ilipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Urais wa Fatma Karume aliposema, ‘’Chama Cha Wanasheria Nchini (TLS) kuacha kujishirikisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati na iwapo watakiuka hilo Mahakama haitowapa ushirikiano’’.

Kauli ya Jaji Mkuu ilihitimishwa pale ambapo kwa mara ya kwanza TLS hawakupewa nafasi ya kutoa hotuba kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kuwafungua macho wanachama wa TLS kuhusu mstakabali wake nchini kama mdau wa sheria. Hii ilipelekea hata jina lake kutopendekezwa na wanachama wa TLS kuwa mgombea Urais.

Yaliyomkuta Fatma Karume yanatoa angalizo kuwa huwezi kuukata mti alioukalia mwenyewe maana ukianguka unaanguka na wewe! Fatma alikuwa anakata mti wa IMMMA Advocates na TLS kwa kujua au bila kujua!

Kuna wengine watasema, ''hakuna mkate mgumu mbele ya chai'' hasa kama kuna mlaji!
mmmmmmhhhhhhh
 
Kwa Africa,
Ukiamua kuwa Mfanyabiasha achana na siasa za Upinzani....

Ukiaamua kuwa Mpinzani au mwanaharakati, achana na Biashara.....

Wengi hawaelewi haya,.

Nikiwa hapa JF, namsakama sana Jiwe na CCM....

Lkn huku Nje ni Kada Ndakindaki......

Kwenye Pesa Mangi nitakuwa mnafki mpaka kufa kwanguuuu....

Sitaki masihara bwasheee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengine wanaouza kwenye magenge sababu hawajui hilo watabisha. Dawa yao kitambulisho cha JPM
 
All this is because we are fighting the dictator, violation of human rights, etc. Fatuma yuko sahihi! Had it not been for the dictatorial regime current undeminig Tanzania freedom , all this would not have happened! TUNAPIGANA NA IDD AMIN, MUUAJI!
kweli wewe ni retired umechoka hata kimawazo😂😂😂😂
 
Udhalimu kwenye serikali za Africa is the order of the day. Huu ndio ukweli. You can accept and live by or perish!

Ndivyo ilivyo Africa kwa sababu serikali ndio mlaji mkuu lakini pia ndiye mtumiaji mkuu wa huduma and goods.

Hata wapinzani wakiingia madarakani watafanya udhalimu vivyo hivyo kama CCM wanavyofanya lakini inawezekana wapinzani wakafanya zaidi ya CCM.

Wanaojua ukweli huu hawahangaiki kupigana vita ya waziwazi ambavyo wanajua hawawezi kushinda.

Fatma Karume amerudi square one wakati huo huo amepoteza vingi zaidi. Waliokuwa wanamshangilia wamehamia kwa mwingine kuendeleza burudani zao. Hii inaitwa 15 minutes of fame.
Mwenzako ana property za kutosha uk hta asipofanya uwakili hawezi kufa njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameona atetee walio wengi kuliko kuangalia maslahi yake na kampuni yake!

Halafu wewe bwana selfish unajifanya kuandika hapa kumuelekeza jinsi ya kua selfish kama wewe atetee tumbo lake na kampuni yake!

Halafu tangu lini ushauri kutoka kwa mwanaCCM yeyote unakua na manufaa kwa mwanaharaki au mpinzani?

Hii dunia hakuna majitu manafiki kama mawanaCCM!
Ulichokiandika ndicho ambacho kwa sasa amechagua kutokifanya baada ya wenye kampuni kumwambia achague kusuka au kunyoa.

Wewe unampa umaarufu wa dakika 15 wakati kampuni ya IMMMA Advocates inapata matatizo kibiashara wakati huo huo hata TLS ikipoteza uaminifu wa taasisi ya Mahakama.

Uselfish anza kuondoa wewe mwenyewe kwa kuondoa fake ID ili upambane kindaki ndaki kama yeye!
 
Unampangia cha kufanya?

IMMMA yeye ana share!Ukimtoa asifanye kazi haimaanishi share zake ndio zinakufa!

Yaani kama hajavunja sheria popote huna cha kumuambia wewe!

Na huo ushahidi kua kaambiwa aondoke IMMMA unao au unajiandikia tu?

Fame unayosemea maana yake ni nini?Kutoa ukweli?Kama kutoa ukweli ni fame then so be it,mwache awe maarufu,wewe inakuumia nini?

Inakosa uaminifu na mahakama kasema nani?Wewe?

TLS ni ya kutetea wanyonge pia kisheria,kama kutetea wanyonge ni branded activism au vyovyote vile utakavyo,then so be it!

Sioni greater good on this planet on whatever reason kama mtu anatumia alichonacho kutetea wasio na sauti,hata kama ni kuongea against authority kandamizi!

Fatuma just did that,ndio maana group kubwa tumempenda and she will always be in us,ataacha TLS ila tutampata kwenye tweeter,interviews,mahakamani,etc!

Sijui kwanini watu kama akina Tundu Lissu au Fatuma etc wanawalaza macho wazi namna hii?Kwanini?
 
Hawa ndiyo walishambulia ofisi za IMMMA Advocates kwa mlipuko,

Unaona Mada zao,zimejaa uzandiki na chuki dhidi ya Shangazi wa Taifa.
 
Kwenye nchi zetu zinazoendelea huwezi kuepuka ukweli kuwa serikali ndio taasisi pekee ambayo matumizi yake ya pesa ndio kipato kikubwa kwa makampuni makubwa ya huduma na kwa mantiki hii huwezi kufanya kazi za uwakili ambazo zinahusu makampuni makubwa ya ndani na kimataifa ambayo mdawi wake mkubwa ni serikali halafu ukaanza kuishambulia serikali kisiasa ukitegemea mafanikio kibiashara. Ni lazima utapoteza moja au yote. Huu ni ukweli ambao wenye kujua umuhimu wa biashara zao za huduma wanaujua na huufanyia kazi.

IMMMA Advocates ni kampuni kubwa ambayo niya vigogo ndani ya CCM ambao mizizi yao iko pia serikalini na kwenye taasisi ya mahakama. Kwa mantiki hii hawawezi kukubali kampuni yao kugonganishwa kisiasa na serikali waziwazi.

Alichokuwa anafanya Fatma Karume hakina tofauti na kujipiga risasi mguuni bila kujua huku akishangiliwa na watu wanaodhani anachofanya ni kuwaburudisha kwenye mitandao huku kampuni ya IMMMA Advocates ikipata matatizo kibiashara.

Badala ya kutumia Urais wa TLS kama daraja la kuiunganisha IMMMA Advocates kibiashara badala yake ametumia kama uzio wa kuitenganisha na serikali. Hata Urais wake wa TLS umeifanya TLS kuwa mbali na taasisi ya mahakama badala ya kuwa karibu zaidi.

Washirika wenzake wamemuomba achague moja kati ya mawili kama anataka aendelee kuwa mshirika wa IMMMA Advocates. Kama anataka aendelee na uanaharakati kama Rais wa TLS au aachane na uanaharakati ndani ya TLS.

Kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ilipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Urais wa Fatma Karume aliposema, ‘’Chama Cha Wanasheria Nchini (TLS) kuacha kujishirikisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati na iwapo watakiuka hilo Mahakama haitowapa ushirikiano’’.

Kauli ya Jaji Mkuu ilihitimishwa pale ambapo kwa mara ya kwanza TLS hawakupewa nafasi ya kutoa hotuba kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kuwafungua macho wanachama wa TLS kuhusu mstakabali wake nchini kama mdau wa sheria. Hii ilipelekea hata jina lake kutopendekezwa na wanachama wa TLS kuwa mgombea Urais.

Yaliyomkuta Fatma Karume yanatoa angalizo kuwa huwezi kuukata mti alioukalia mwenyewe maana ukianguka unaanguka na wewe! Fatma alikuwa anakata mti wa IMMMA Advocates na TLS kwa kujua au bila kujua!

Kuna wengine watasema, ''hakuna mkate mgumu mbele ya chai'' hasa kama kuna mlaji!
Acha PROG bro:confused::confused:
 
Tatizo watu hawamuambii ukweli huyo Fatma sababu harakati zake zinawafaidisha. TLS iligeuka kuwa taasisi ya kiharakati badala ya kusimamia misingi ya kuanzishwa kwake.

Nchi hii siku hizi ukishabikia siasa za upinzani unaonekana ndio unafanya kazi kwa usahihi lakini wanasahau tunapaswa kuwapinga watawala na CCM kwa sisi kuwa mfano. Niliwahi kusema huko nyuma, si sahihi mwenyekiti wa TLS kushinda twita akivizia statement za makada wa CCM na kuzipinga hadi inaonekana dhahiri kama ana upande kinyume na nafasi yake.

Hata kama ukweli lazima usemwe lakini inapitiliza na kugeuka ushabiki wa kisiasa dhahiri.

Kwa mara nyingine wapinzani wamepewa fursa ya kutoa mfano lakini platform hiyo imetumika vibaya. Tulitegemea walau hata vuguvugu la katiba mpya kupitia TLS hii ya Lissu na Fatma lakini wanaiacha kama walivyoikuta labda wameisaidia CCM kuonesha dunia kuwa hata wapinzani wanapata fursa kama hizi bila serikali kuingilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Mkuu, ufafanuzi murua kabisa. Nimejifunza jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom