Je, ‘’15 minutes of fame’’ za Fatma Karume zimegharimu biashara za IMMMA Advocates na TLS?

Kwenye nchi zetu zinazoendelea huwezi kuepuka ukweli kuwa serikali ndio taasisi pekee ambayo matumizi yake ya pesa ndio kipato kikubwa kwa makampuni makubwa ya huduma na kwa mantiki hii huwezi kufanya kazi za uwakili ambazo zinahusu makampuni makubwa ya ndani na kimataifa ambayo mdawi wake mkubwa ni serikali halafu ukaanza kuishambulia serikali kisiasa ukitegemea mafanikio kibiashara. Ni lazima utapoteza moja au yote. Huu ni ukweli ambao wenye kujua umuhimu wa biashara zao za huduma wanaujua na huufanyia kazi.

IMMMA Advocates ni kampuni kubwa ambayo niya vigogo ndani ya CCM ambao mizizi yao iko pia serikalini na kwenye taasisi ya mahakama. Kwa mantiki hii hawawezi kukubali kampuni yao kugongamishwa kisiasa na serikali waziwazi.

Alichokuwa anafanya Fatma Karume hakina tofauti na kujipiga risasi mguuni bila kujua huku akishangiliwa na watu wanaodhani anachofanya ni kuwaburudisha kwenye mitandao.

Badala ya kutumia Urais wa TLS kama daraja la kuiunganisha IMMMA Advocates badala yake ametumia kama uzio wa kuitenganisha na serikali. Hata Urais wake wa TLS umeifanya TLS kuwa mbali na taasisi ya mahakama badala ya kuwa karibu zaidi.

Washirika wenzake wamemuomba achague moja kati ya mawili kama anataka aendelee kuwa mshirika wa IMMMA Advocates. Kama anataka aendelee na uanaharakati kama Rais wa TLS au aachane na uanaharakati ndani ya TLS.

Kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ilipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la uenyekiti wa Fatma Karume aliposema, ‘’Chama Cha Wanasheria Nchini (TLS) kuacha kujishirikisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati na iwapo watakiuka hilo Mahakama haitowapa ushirikiano’’.

Kauli ya Jaji Mkuu ilihitimishwa pale ambapo kwa mara ya kwanza TLS hawakupewa nafasi ya kutoa hotuba kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kuwafungua macho wanachama wa TLS kuhusu mstakabali wake nchini kama mdau wa sheria. Hii ilipelekea hata jina lake kutopendekezwa na wanachama wa TLS kuwa mgombea Urais.

Yaliyomkuta Fatma Karume yanatoa angalizo kuwa huwezi kuukata mti alioukalia mwenyewe maana ukianguka unaanguka na wewe! Fatma alikuwa anakata mti wa IMMMA Advocates!

Kuna wengine watasema, ''hakuna mkate mgumu mbele ya chai''.
Ni kitu jinga halijawahi kutokea... Tulimuonya Sana akaona sisi washamb na walamba miguu ya serikali ona sasa aibu inamkuta mtu mzima.
 
sikutegemea kama ungekuja na hoja finyu kama hizi.wewe kama watu wachache wa ccm ambao angalau wamebakiwa na akili hata za kuchambua mambo kidogo sana.Lakin leo umezingua.
1.alichokuwa akikifanya Karume hakina uhusiano wowote na kampuni hizo za mawakili.Yeye alifanya hicho kama "binafsi"
2.Unatuaminisha kuwa ili ufanikiwe lazima ujihusishe na ccm moja kwa moja hiyo ni nonsense.wapo kina Manji ,Mo, na wengine kibao washaonja joto la jiwe la unafiki wa ccm.
2.Alichokuwa akikifanya Karume ni kweli tupu hivyo kweli haiwezi kuzidiwa na uongo,unafiki na uzezeta wa ccm kama wanavyofanya akina Mtatiro,kafulila na wengine.

3.TLS kumweka kando urais si sababu ya kisiasa,hizo ni hisia zako.TLS wanafanya uchaguzi after 1 year naye ashatimiza majukumu yake amekamilisha alichoagizwa.katika kipindi cha miaka 3 TLS imekuwa haitishiki na vitisho vya walioolewa na mhimili wa serikali hasa mahakama na bunge.Imejitegemea kama katiba inavyotaka.
4.Seikali ikitaka kila taasisi na chombo na kila mtu awe na mawazo sawa na serikali basi Maendeleo tutasikia kwenye bomba.Mungu aliumba mimea ya aina mbalimbali ipendezeshe dunia.kuna mingine ina rangi nzuri lakini ni sumu hatari.Be careful na lichama lenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulichoandika hapa ni nadharia wakati mimi
Nilichoandika ni practical.

Kumbuka kuukubali ukweli ni njia mojawapo ya kutafuta majawabu sahihi.
 
Lakini huyo anayesema wenzake waache kujishirikisha na mambo ya siasa mbona yeye anashiriki kwenye vikao vya siri vya chama? Hakuthibitishwa kwenye nafasi yake mpaka Mwenyekiti alipojiridhisha kuwa ni kada mwaminifu.

Mpaka leo hii, amekuwa akikutana mara kwa mara na Katibu mkuu wa chama, kabla yya vikao vya chama ili kutoa ushauri wake juu ya wafanye nini ili yeye aweze kuwalinda kisheria
Hoja yako hapa ni nini?

Kwani Fatma Karume alikatazwa na IMMMA Advocates kwenda kwenye vikao vya siri?
 
sikutegemea kama ungekuja na hoja finyu kama hizi.wewe kama watu wachache wa ccm ambao angalau wamebakiwa na akili hata za kuchambua mambo kidogo sana.Lakin leo umezingua.
1.alichokuwa akikifanya Karume hakina uhusiano wowote na kampuni hizo za mawakili.Yeye alifanya hicho kama "binafsi"
2.Unatuaminisha kuwa ili ufanikiwe lazima ujihusishe na ccm moja kwa moja hiyo ni nonsense.wapo kina Manji ,Mo, na wengine kibao washaonja joto la jiwe la unafiki wa ccm.
2.Alichokuwa akikifanya Karume ni kweli tupu hivyo kweli haiwezi kuzidiwa na uongo,unafiki na uzezeta wa ccm kama wanavyofanya akina Mtatiro,kafulila na wengine.

3.TLS kumweka kando urais si sababu ya kisiasa,hizo ni hisia zako.TLS wanafanya uchaguzi after 1 year naye ashatimiza majukumu yake amekamilisha alichoagizwa.katika kipindi cha miaka 3 TLS imekuwa haitishiki na vitisho vya walioolewa na mhimili wa serikali hasa mahakama na bunge.Imejitegemea kama katiba inavyotaka.
4.Seikali ikitaka kila taasisi na chombo na kila mtu awe na mawazo sawa na serikali basi Maendeleo tutasikia kwenye bomba.Mungu aliumba mimea ya aina mbalimbali ipendezeshe dunia.kuna mingine ina rangi nzuri lakini ni sumu hatari.Be careful na lichama lenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo maana hata kufanya biashara nje ya nchi kwa watanzania ni ngumu Kwa sababu washaaminishwa lazima utegemee ccm ndo ufanikiwe
 
Kwa Africa,
Ukiamua kuwa Mfanyabiasha achana na siasa za Upinzani....

Ukiaamua kuwa Mpinzani au mwanaharakati, achana na Biashara.....

Wengi hawaelewi haya,.

Nikiwa hapa JF, namsakama sana Jiwe na CCM....

Lkn huku Nje ni Kada Ndakindaki......

Kwenye Pesa Mangi nitakuwa mnafki mpaka kufa kwanguuuu....

Sitaki masihara bwasheee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Heri umekiri kuwa wewe ni mnafiki
 
Kabla ya Lissu na Fatma Karume nani aliizungumzia TLS? ukweli ni kuwa imekuwa threat kwenye mfumo uliozoea kusifiwa tu kwa kila jambo.
Sio kweli.
TLS imefanya mengi sana katika kubadili sheria na sera mbali mbali kandamizi.
Mabadiliko ya sheria ya ardhi, sheria ya ndoa, sheria ya haki za mtoto ni sehemu ya mafanikio ya TLS.
Kwa taarifa yako rais wa TLS ni mjumbe wa bodi kubwa sana hapa nchini zinazoshughulikia mambo ya sheria na utoaji wa haki.
Na Rais wa TLS ilikuwa haimchukui muda kupata hata appointment ya Ikulu au kwa Spika.
TLS ni chombo kimeundwa kwa sheria. Kina majukumu na wajibu wake.
Ukihama usitegemee wadau wakupe ushirikiano.
Na sio kupinga tu, kama sikosei, hakuna chombo kimepinga sheria na sera za nchi hii na kuleta mabadiliko makubwa ya Katiba, sheria na sera kama TLS
 
wewe ni kati ya watanzania wajinga kabisa kupata kutokea hivi mtu akitetea uhiru wa faragha anatetea ushoga? kwa hiyo na madaktar wanaohifadhi siri za wagonjwa wa HIV nao wanasambaza ukimwi!
haki ya usiri /privace ipo kikatiba kwakuwa mmezoea kukenua meno katiba inapovunjwa ndo mana mnaona kawaida tu
Nina wasi wasi na wewe.........!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom