PostGE2025 Jasiri wa mwisho - JKT dhidi ya mfumo wa vyama

PostGE2025 Jasiri wa mwisho - JKT dhidi ya mfumo wa vyama

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

CHAGOSI GERALD

Senior Member
Joined
Jan 25, 2020
Posts
162
Reaction score
286
Watanzania wanaishi katika maigizo makubwa kuliko “Tausi,” “Siri za Familia,” “Jumba la Dhahabu,” na “Bongo Movie” zote zilizowahi kutengenezwa. Maigizo ambayo kila mtu anajifanya haoni, ilhali moshi wa jiko la taifa unafuka hadharani. Kila mtu anasema “Tatizo ni viongozi” kana kwamba viongozi wametoka kwenye kisiwa cha Wakorea. Wakati ukweli ni mmoja:

Picsart_25-12-02_08-30-46-241.jpg


Tatizo ni mfumo, na mfumo umewekwa ili ushinde Watanzania, sio kuwasaidia.

Vyama vya siasa ni ngazi za kuingia kwenye mfumo, sio silaha za kuubadilisha.
Ndiyo maana watu wanabadili chama, lakini hawabadili tabia ya mfumo.
Ndiyo maana viongozi wanabadilika, lakini maskini hawabadiliki.
Ndiyo maana ahadi zinabadilishwa, lakini mikataba haibadiliki.

Vyama vya siasa viliundwa sio kutatua matatizo, bali kuyalinda.
Vinawapa wananchi uhuru wa kunung’unika, lakini si uwezo wa kubadili.
Ni sawa na mtu aliyefungwa miguuni minyororo, akaambiwa:
“Una uhuru wa kupiga kelele, lakini usisogee hatua tatu.”

Huo ndiyo uhuru wetu wa kisiasa.

Vita halisi si CCM vs CHADEMA,
GEN Z vs CCM
WANANCHI VS MAJESHI YAO
Vita halisi ni:
Vijana vs Mfumo
lakini sijui kama vijana wanatambua hili au wanafuata mkumbo kama inavyodaiwa.

JKT: Ilipotakiwa kuwa Taasisi, Mfumo Ukaigeuza Kambi

Hapo ndipo tunarudi kwenye JKT.
Mahali ambapo Mwalimu alikusudia vijana wajenge uchumi, sio kupigwa push-up na kurudi nyumbani kusubiri ajira ya Sensa au Uchaguzi haramu.

Mwalimu alitaka JKT iwe mahali ambapo:
~ mbegu za viwanda zinapandwa
~ watafiti wanazaliwa
~ wabunifu wanapigwa msasa
~ viwanda vya kutengeneza ndege, magari na mitambo vinajengwa
~ ardhi inageuzwa kuwa gesi ya uchumi
~ kila kijana anakuwa mtengeneza bidhaa, si mtengeneza CV utadhani CV ndio inaeleza ukubwa wa Akili yake.

Lakini nini kilitokea?
Vyama vya siasa vikapewa kipaumbele kuliko taifa.
Wanasiasa wakaigeuza JKT kuwa:
eneo la kutafuta kura, si eneo la kutengeneza taifa. Vijana wanajitoa kujenga vituo vya afya Sifa anapata Mwanasiasa. Hakika vijana wanatumika vibaya.

Vijana wakaambiwa “mjifunze uzalendo,”
lakini hakuna aliyeambiwa “mnaendesha uchumi wa taifa.”

Hapo ndipo mchezo ulipoanzia.

Mwanasiasa akipanda jukwaani kuhubiri uzalendo, swali la kuuliza si “anaongea nini?”,
bali “kuna bendera gani kwenye bahasha aliyopokea jana usiku?”

CCM wanapiga magoti kwa Wamarekani.
CHADEMA wanapiga magoti kwa Ulaya.
Vyama vingine vinapiga magoti kwa yeyote mwenye fedha na mkoba mzito.

Tatizo si kwamba wanapiga magoti -
tatizo ni kwamba wanaficha ukweli kwamba wao ni mawakili wa mataifa yenye malengo yao.
Wanachofanya ni kutekeleza sera zisizotengenezwa katika mtaa wa Buguruni au Mwananyamala,
bali katika ofisi za watu wenye ajenda zao Washington, Brussels, Abu Dhabi au Mumbai.

Ndiyo maana suala la rasilimali halijawahi kuwa kipaumbele chao.
Ukiwaambia taifa liendeshe bandari yake, wanakuuliza:
“Kwani wewe unaweza kuendesha bila mwekezaji?”
Lakini mwekezaji mwenyewe hajawahi kupanda gari la daladala hata siku moja.

Ukweli mchungu ambao unaogopwa kuambiwa

Kama JKT ingesimamia uchumi wa taifa —
vyama vya siasa vingekufa siku hiyo hiyo.

Kwa sababu vyama vinakula kwa mgawanyo wa rasilimali ambao unafanywa na wafadhili.
Lakini JKT ikipewa uchumi:
~ hakuna dili za kupiga commission
~ hakuna mikataba ya kuficha majina ya wabia
~ hakuna chombo cha nje cha kuandika ajenda
~ hakuna kisingizio cha “uwekezaji”

Kwa mara ya kwanza, taifa lingekuwa linaendeshwa na kazi - sio maneno.

Na hapo ndipo mfumo unapoogopa.
Mfumo hauogopi upinzani, mfumo unaogopa uzalishaji.
Mfumo hauogopi vijana, unaogopa vijana wenye uchumi.

Kwa nini Gen Z ndio kizazi hatari zaidi kwa mfumo?

Kwa sababu hawa ni vijana ambao:
  • hawajali vyama
  • hawajali propaganda
  • hawahongwi kwa Tsh 20,000
  • hawaamini simulizi za miaka 60 zisizokuwa na msingi.
  • hawajifungi kwenye makabila wala madhehebu
  • hawatishwi na ofisi yoyote ya dola
  • hawako tayari kuishi kama wanyamapori katika nchi yao wenyewe

Hawa ndio vijana ambao mfumo haujawazoea.
Mfumo umezowea vijana wa aina ile ile toka zamani:
wanaotaka kuwa madiwani, wabunge, au kuajiriwa serikalini.

Lakini Gen Z wanataka mfumo mzima uvunjwe.
Wanataka uchumi unaomilikiwa na vijana, si mabwanyenye.
Wanataka maeneo ambayo zamani yalikuwa ya matajiri sasa yawe viunga vya viwanda vya kizazi chao.

Hapo ndipo serikali na vyama vya siasa vinapata presha.
Kwa sababu kizazi hiki hakina loyalty kwa chama - kina loyalty kwa taifa.

Kama tunataka kutengeneza Tanzania mpya, lazima tubadilishe uwanja mzima.

Hatuwezi kuongeza wachezaji kwenye timu ile ile ya zamani.
Hatuwezi kuongeza maneno kwenye Katiba ya zamani.
Hatuwezi kuweka alama ya penseli kwenye sanduku la kura na kudhani hiyo ndiyo mapinduzi.

Tunataka mfumo unaosema wazi kwamba JKT ndiyo injini ya uchumi.
Na mfumo huo unaweza tu kuwekwa na KATIBA MPYA.

Katiba inayotambua kwamba rasilimali za taifa ni mali ya wananchi,
na mtendaji mkuu ni taasisi ya vijana wenye uzalendo - si watu wanaoitwa wawekezaji.

Katiba inayorudisha nguvu mikononi mwa kizazi kipya,
sio kizazi cha viongozi walioteuliwa kwenye makabrasha ya mabalozi.
 
Sawa, ila Hiyo mifumo inashikiliwa na hao wanasiasa ndio maana kelele wanapigiwa wao. Haitobadilika Hadi wakubali kubadilika.
 
Hii nilichelewa kuisoma, but rest assured, umeandika kila kitu cha maana hapa, great thinker wa kweli mno, kesho nitaisoma tena, na keshokutwa, na mtondogoo, yes, this is it!
 
Back
Top Bottom