Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi

Wakisusa itabaki na tutauza kipindi Dunia mambo yakibadilika ,lakini wanazihitaji ndio maana walikubaliana na mabadiliko yetu ya kisheria na kisera
Dunia inabadilika kwenda kwenye kutumia magari ya solar energy and thus shunning away with petrol! the same applies to all those gold, diamond etc!
 
Angalieni ukweli ulioandikwa na si vinginevyo

Businesses are shutting,
1.CBA wamefunga matawi ya mtwara, tunduma, moshi na mbeya.
2.Biashara ndogo ndogo za maduka nazo pia zinafungwa.
3.Dangote cement inalegalega bado kuondoka tuu kama terms alizopewa wakati anakuja hazitotimizwa.
4.Mabenki mengine yamefungwa kabisa Twiga
Na yaliyobaki yamezidiwa na non performing loans hadi yamepewa warning na BOT.

exports are slumping,
kwenye hili kwa mtu yeyote anaefuatilia report za BOT anajua ukweli (mnaweza hata kurejea tuu mada aliyoweka zito kabwe humu jamvini akiuliza kinachosababisha kushuka kwa uuzaji wa mazao yaliyokuwa yanauzwa India).

investors are fleeing and economic growth is forecast to slow.
Kwenye economic growth kwanza data zimekuwa review kutokana na kuwepo kwa "UPISHI"

KUNA MSEMO "UKITAKA KUMUUWA MBWA MPE JINA BAYA"

WAWEKEZAJI WA NJE WAKILALAMIKA HALI MBAYA WANAITWA "WEZI WA RASILIMALI ZETU"

WAWEKEZAJI WA NDANI WAKILALAMIKA WANAITWA "WAPIGA DILI" "WAKWEPA KODI"
Ndicho kinachofanyika sasa hivi kila anaeonyesha mapungufu ya sera za kiuchumi za utawala wa awamu ya 5 anapewa jina baya
HATUTOENDELEA KWA MWENDO HUU
 
Pascal Mayalla Haya Mataifa hayawezi kuunga mkono juhudi za Mh. Rais, hasa pale ambapo tunaanza kufanikiwa katika kuwabana wanyonyaji wa maliasili zetu. Watakuja na kila aina ya propaganda, na watatumia vyombo na taasisi zao kutuchafua. Mambo ya aina hii yamekua yakitokea sio tu kwa Tanzania, tumeona propaganda za namna hii zikienezwa kwa nchi nyingine zilizokataa unyonyaji wa mataifa ya maghalibi na zilizoamua kusimamia usawa katika kusimamia maliasili za nchi.


Sisi watanzania hatupaswi kurudishwa nyuma na propaganda dhaifu kama hizi, inafaa tusimame kwa pamoja, tumuunge mkono Mh. Rais wetu, na tuendelee mbele. Tanzania ki uhalisia tulihitaji kiongozi wa kaliba ya Mh. Magufuli, sasa tumempata tumtumie katika kipindi hiki cha miaka 10 na tutafikia pazuri.

Kuna mabandiko ambayo watu wa mahaba hamtakiwi kuchangia, sababu si ya kimahaba. Sio yale ya kusoma heading halafu unachangia. Moja ya mabandiko ni kama haya ya Pascal Mayalla. They are way too much above your heads. Pole sana.
 
swali la msingi... je,wanachokizungumza hao economic kina ukweli??au wametungatunga tu???
 
GDP na GNP ni vipimo vya pato la taifa ambavyo havina uharisia tupime kukua kwa uchumi wetu kwa kutumia Growth National Happiness (GNH) na Genuine Progressive Indicator(GPI)
 
Wanaweweseka hao. Walizoea kujisombea madini na resources zetu huku wakitusifia kua uchumi wetu unapanda?

Nchi imepata Rais mwenye akili na anayewajua janja yao, sasa wameanza propaganda za kishenzi.

Kama uchumi unadorora si watuache kama wanaweza?


Ebu nikuulize kuwa hivi kusonga mbele kuna mahusiano gani na kuuliwa kwa watu, kupotea kwa watu, kamatakamata ya Watu, kufungia magazeti
 
Mkuu.
Unaporekebisha nchi ambayo ilikuwa na uhovyo mwingi kwa kiasi tulichokuwa tumefikia, ni lazima maumivu yatatokea. Ndio maana Rais anasema tuvumilie lakini ni lazima tupitie kipindi hiki kama kweli tupo serious tunataka kupona kama nchi.
Kweli kabisa, mkuu, tumefikia kipindi cha baadhi ya ndugu zetu kudhani wale wageni wavimizi wa mababu zetu tuliowaondoa madarakani miaka ya sitini, wanacho cha kutushauri ili tupate kusonga mbele. Kana kwamba simba mwenye njaa anaweza kumshauri swala namna nzuri ya kujificha ili asimtie makuchani mwake, aendelee kuishi kwa kula nyasi huku simba mwenyewe akifa njaa!
 
Paskali tunakusamehe bure
Angali thred zako zote unaleta thred kimzaa mzaa lkn ukisoma unakuta unataka kutuaminisha ujinga
Magazeti ya wanyonyaji hayawezi hata siku moja kumsifu mtu anayewanyanganya manyangau ulaji, ni watanzania wangapi wanasoma hilo gazeti lako
Kwa nini huleti thred za Magufuri anapofanya mambo makubwa na yenye kuleta maendeleo makubwa ya nchi.
Ww kila siku kumsakama Rais
Unataka Magufuri afanye nini hili muone nchi hii anaipeleka kwenye neema
Wacha awe dikteta kama unavyotaka kutuaminisha lakini ajenge Reli , Ajenge Viwanda , alete nidhamu kazini, akamate mafisadi , akamate wala Rushwa, Madawa ya kulevya na uchafu wote
Tena ningeomaba Magufuri awe Dikteta kweli kweli hili anyooshe nchi
Tuondolee uvivu wenu , mnakaa kwenye Keybord na kujifanya mnaielewa nchi
 
F*ck The Economist. Hawa waandishi uchwara na publications zao wana agenda zao. Wanatumiwa kumchafua Rais wetu mpendwa. Uchumi unakuwa kwa kasi ya ajabu, ajira za kumwaga zinatengenezwa, uzembe serikalini na utumishi wa umma unapunguzwa kila leo, miradi mikubwa inazinduliwa lakini hawa mabangusilo hawaoni. Kazi kurusha matope tu. Kwa sisi waerevu tunaojua mambo ya dunia na nani hasa anaendesha dunia hii, tunaelewa kuwa hizi media ni mouthpiece ya makundi fulani ya watu wenye interests zao binafsi. I repeat, f*ck em!
 
Me nadhan issue c kukanusha kwenye vyombo vya habari ila kuangalia wapi tumekosea km taifa tusonge mbele
Kweli mkuu, kuna mambo Magufuli kayapatia kabisa na anastahili pongezi.
Ila the macro~economics za nchi ziko matatani.
Biashara zinafungwa kwa harrassment ya TRA, watu wanakosa kazi ni kiujumla mazingira kibiashara ni tete.
Hata hivyo nina support SGR, Stieglers Gorge Powe Plant na hata bomba la gesi.
Hii ndiyo itakuwa legacy ya Magufuli.
 
Heri maskini mwenye furaha na amani kuliko tajiri asie na furaha na amani.Tumwambie ukweli umoja wa Taifa letu ndio nguzo yetu,na tutaweza mengi kwa kasi zaidi pamoja. Bado nashuhudia ushamba uchama ktk mikutano rasmi ya serikali! Ni dhambi kutumia njaa za watu ,eti sharti avae kijani ndio apate riziki ,huu ni ukoloni mwingine wa kishamba zaidi karne hii.Watu wanavaa nje ila mioni mwao wanajua wanachokiamini.Tanzania ni kubwa zaidi ya yeyote
 
kama uchumi uko vibaya kwanini washawishi vikwazo na hata vikwazo vikiwekwa watakaoumia ni wananchi wa kawaida angalia Tundu Lissu yeye anatibiwa ulaya kuna wananchi wangapi wamepigwa risasi wanatibiwa wapi kama tuna matatizo nchini mwetu wa kuyatatua ni sisi wenyewe wala sio wanaotoka nje watatutatulia
 
Back
Top Bottom