Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi

Pascal Mayalla Haya Mataifa hayawezi kuunga mkono juhudi za Mh. Rais, hasa pale ambapo tunaanza kufanikiwa katika kuwabana wanyonyaji wa maliasili zetu. Watakuja na kila aina ya propaganda, na watatumia vyombo na taasisi zao kutuchafua. Mambo ya aina hii yamekua yakitokea sio tu kwa Tanzania, tumeona propaganda za namna hii zikienezwa kwa nchi nyingine zilizokataa unyonyaji wa mataifa ya maghalibi na zilizoamua kusimamia usawa katika kusimamia maliasili za nchi.


Sisi watanzania hatupaswi kurudishwa nyuma na propaganda dhaifu kama hizi, inafaa tusimame kwa pamoja, tumuunge mkono Mh. Rais wetu, na tuendelee mbele. Tanzania ki uhalisia tulihitaji kiongozi wa kaliba ya Mh. Magufuli, sasa tumempata tumtumie katika kipindi hiki cha miaka 10 na tutafikia pazuri.
Nipe jina la kiongozi hata mmoja aliyefanikiwa kwa kwenda against western countries
 
How? wanaomba misaada kwetu? Wana nini wanachokikosa wakiachana na sisi? Jiulize wakisusia dhahabu kuna wa kuzinunua? Remember, Diamonds are forever!
Hawaombi misaada kwetu kwa sababu wanatuibia...WAMESHIKWA VIBAYA MNO NA MAGUFULI....
Possibly hata huyo mwandishi wa HILI GAZETI INAWEZEKKANA KAHONGWA HATA NA ACCACIA
 
Me nadhan issue c kukanusha kwenye vyombo vya habari ila kuangalia wapi tumekosea km taifa tusonge mbele
Mkuu. Hivi unadhani hawa jamaa wanatupenda saaaana! kiasi kwamba wanajisikia uchungu uchumi wetu unaposhuka?
Think twice. Kwangu moja ya indicator kuonesha Rais wetu yupo kwenye mstari sahihi ni hizi kelele zao za maumivu kana kwamba wanatujali saaaana!
 
Mayala hongera kwa kuweka hii thread hapa!Kwanza kabisa naanza na wewe unaonesha bado ni mwandishi mwoga kwa taaluma yako pengine unogopa kutekwa, umeshasema rule ya kwanza ya uandishi wa habari hutakiwi kuwa mwongo!

Mbona unasema waandishi wa economics magazine waoongo!Wameitendea haki taaluma yao vizuri, ulitakiwa uanzie hapo na sio kuwa editor!Ukweli mchungu wako real 100% na ndio ukweli wenyewe our president rogue!He is tunning our country to like be a skunk! Note,'a sunk vessels has no rudder'
Et real 100% ...may be real on lies by 100%
 
Acha upuuzi Hawaombi misaada kwetu kwa sababu wanatuibia...WAMESHIKWA VIBAYA MNO NA MAGUFULI....
Possibly hata huyo mwandishi wa HILI GAZETI INAWEZEKKANA KAHONGWA HATA NA ACCACIA
Kusema wanatuibia nadhani sio sahihi maana tumesaini mikataba ambayo ipo kisheria na sisi kuingia nao ubia tena wanalipa kodi na tozo mbalimbali serikalini sasa utasemaje wanatuibia wakati wanafanya kazi kihalali au maana ya wizi imebadilika mkuu?

Tatizo lipo kwa viongozi wetu tuliowapa nafasi ya kuzisimamia rasilimali zetu hawa ndio sio waaminifu wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi na sio ya nchi

Ndio maana wanaingia mikataba ambayo hainufaishi nchi ila wao na ndio hiyo unasema wanatuibia lkn sio ni mikataba mibovu iliyoingiwa na wenzetu kwa ajili ya kujinufaisha ila ni mikataba halali kabisa
 
Paskali, lazima wasomaji wenzangu tuache papala! Mpangilio wa jarida lazima tuufahamu. Huwa kuna taarifa rasmi za kiuchumi, zinazotokana na uchunguzi wa jarida. Pia kuna taarifa zinazoandikwa na waandishi binafsi kwa mtazamo wao na maomni yao, yaani columnist. Taarifa hii ya Magufuli siyo ya Jarida ni ya columnist. Unaweza ukampuuza tu!

Ukisoma taarifa hii kwa ufahamu, utagundua mwandishi anajaribu kufaidika na uzembe wa wasomaji. Kuna wasomaji wazembe kama unavyoona meseji au maoni ya wasomaji wa JF, wanaoona nafuu kwa kusaidiwa kueleza ubaya wa rais! Taarifa kama hizi huandikwa na watanzania na kuzitoa kwenye majarida kama haya.

Ukiangalia kichwa cha habari kinamzungumzia rais Magufuli na uchumi wa TZ. Lakini ukiangalia baadhi ya mambo mabaya yanayoandikwa ndani ya taarifa hii ni yale ya zamani yasiyomuhusu Magufuli. Lakini kwa msomaji mzembe mwenye kupenda kusikia ubaya wa magufuli, hataweza kuona mchezo na upuuzi wa mwandishi.

Hili ni jarida la uchumi halistahili kupima ubora wa mipango ya serikali kwa kuangalia investors walioingia nchini au walioondoka bila kusema faida gani ilipatikana kwa nchi. Investors ktk nchi hizi ni wale wanaokuja kuchota na mara zote ukiwadhibiti wanaondoka. Eti hilo nalo ndo jambo la kuandikwa na kutumwa the economist. Binafsi naona ni juhudi inayoendelea ili kiongozi atishike na alegeze baadhi ya mambo ya kipuuzi yaliyofanyika miaka ya nyuma yaendelee.

Wale munaoshabikia, nasikitika kuwaambia Ulaya au Amerika hakuna mjomba wa kukupa maendeleo, eti leo hii anasikitika kwamba unakosa njia safi ya kuendelea. Ukikenua meno kwamba umetetewa, baadaye ni mtego wa kukulawiti.
 
Wanabodi.

Hii ni Makala toka jarida la The Economist, linamsakama sana rais Magufuli, katika Makala hii, linahamasisha rais Magufuli adhibitiwe kwa kuwekewa vikwazo vikali kabisa kiuchumi.

Wachumi wetu tusaidieni, ukiondoa hoja za udikiteta, jee kiuchumi rais Magufuli anafanya vizuri?. Kama rais Magufuli anajenga Tanzania yenye neema na ustawi kiuchumi, then tujiulize jee Watanzania tunataka nini?. Tunataka Tanzania masikini yenye demokrasia, au Tanzania tajiri yenye udikiteta?.

Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
Wengine neema hatujaiona,labda weye uliyejikoni!
Vipi Makinikia bado ziko Bandarini kwenye Makontaina??
Vipi Yale matrilioni?

Yako mazuri ya Raisi wa awamu ya Tano kiuchumi lakini mguvu kubwa isiyoakisi hali halisi ya mambo ni njia mmoja kuelekea Njiapanda Kiuchumi. Hili halihitaji Mchumi kuliona. Maneno huumba,na imeandikwa Ombeni nanyi mtapewa! Haikuandikwa muombe mazuri tu!
 
Tupe source ya hii taarifa then tuanzie hapo. Besides that mnapaswa muelewe wazungu tumewashika pabaya...kilichobaki ni kutaka kutuvuruga kupitia machagadema. Mungu yupo upande wetu na kamwe hatuvurugiki. Tunazo taarifa za vikao vyao na tundu lisu huko ubelgiji....hahaha endeleeni kujitekenya tu. Mbona hawaongelei demokrasia ya China?
 
Back
Top Bottom